1. Hata hospitali za umma wametoa maagizo hakuna mtu kuingia maeneo yao bila barakoa.
2. Barakoa ni nzuri na zinahitajika wakati huu. Zingekuwa hazina msaada basi madaktari na wauguzi wasingekuwa wanazitumia.
3. Katika hali iliyopo sasa hivi, ili covid19 isisambae, wenye ugonjwa, na wasio na ugonjwa, wanatakiwa wavae barakoa.
4. Barakoa zikiwa fashion au utamaduni wetu itakuwa vizuri zaidi. Hata tukiendelea na utaratibu wa sasa wa kuosha mikono itakuwa jambo jema vilevile. Tutafanikiwa kupunguza magonjwa mengi yanayosambaa kwa pumzi, au yanayosambaa kupitia mikono michafu.