Barakoa zipi zivaliwe na wanafunzi mashuleni?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nimeona shule wakishona barakoa au kuwaagiza wazazi wazazi kushonea watoto wao barakoa zinazofanana na sare ya shule husika. Hivyo wanashona kitambaa Cha kaptura au Cha shati ya shule.

Shida Ni kwamba vitambaa vinavyotumika kwa sare vingi vyao sio pamba baoi Ni polyester. Je, kitambaa Cha polyster kinafaa kwa barakoa?
 
Unachofanya wewe unarudia ishu zilizo jadiriwa kipindi Corona inaingia yaani sio wakati wakuuliza swali kama hilo unless uwe ulilala miezi yote ukaamka leo.

Short: suala la kitambaa kufaa au kutofaa lilijadiriwa sana likafikia hitimisho kitambaa kinafaa ila katikati ya barakoa kuwe na Sponge/layer yoyote ile na hiki liliongelewa kila sehemu wizara, WHO nk.

Nashangaa unauliza tena maswali yaleyale tulojiuliza miezi kadhaa nyuma.
 
Ila barakoa zitawaumiza sana watoto maana kuvaa barakoa kila siku Massa 11 ni hatari sana.

Kipindi maalumu cha kuvaa barakoa hasa maeneo ya baridi lakini eneo la Joto barakoa kwa kweli itawaumiza watoto kwa sababu watakua wanavuta hewa yenye Joto na unyevu unyevu muda wote.

Nadhani pawe na ubunifu tu wa kukaa umbali wa mita mja na usafi wa kunawa na kuoga Mara kwa Mara kwa wale wa Bweni.

Madawati yawe yanasafishwa kwa mapovu Mara kwa Mara na maeneo yote kama milango na madirisha kwani wingi wa wanafunzi unatosha kufanya usafi hata kila baada ya masaa manne maeneo yote ya Shule.
Lakini barakoa ni shida kuivaa muda wote kwa masaa 11.
 
Wakati wa likizo watoto wamecheza sana,wamechanganyika sana tu,,
Inasemekana,convid haiathiri sana watoto,,yaani wanaweza kupata ila ikaishia kuwa mild,,yaani vikohozi vya hapa na pale kisha kimya,
Kesi ya watoto kuugua duniani ni 1 in 100000
 
TUMESHAJIAMINIAHA AIPO
BARAKOA ZANN KWA WATOTO SASA
 
Nimeona shule wakishona barakoa au kuwaagiza wazazi wazazi kushonea watoto wao barakoa zinazofanana na sare ya shule husika. Hivyo wanashona kitambaa Cha kaptura au Cha shati ya shule.

Shida Ni kwamba vitambaa vinavyotumika kwa sare vingi vyao sio pamba baoi Ni polyester. Je, kitambaa Cha polyster kinafaa kwa barakoa?
Vaeni hata za vitenge , mkubwa kishasema
 
[emoji116][emoji116][emoji116]
IMG-20200629-WA0000.jpg
 
Ila barakoa zitawaumiza sana watoto maana kuvaa barakoa kila siku Massa 11 ni hatari sana.

Kipindi maalumu cha kuvaa barakoa hasa maeneo ya baridi lakini eneo la Joto barakoa kwa kweli itawaumiza watoto kwa sababu watakua wanavuta hewa yenye Joto na unyevu unyevu muda wote.

Nadhani pawe na ubunifu tu wa kukaa umbali wa mita mja na usafi wa kunawa na kuoga Mara kwa Mara kwa wale wa Bweni.

Madawati yawe yanasafishwa kwa mapovu Mara kwa Mara na maeneo yote kama milango na madirisha kwani wingi wa wanafunzi unatosha kufanya usafi hata kila baada ya masaa manne maeneo yote ya Shule.
Lakini barakoa ni shida kuivaa muda wote kwa masaa 11.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom