John,
Hivi unataka kusema Rais aunde wizara kwa kufuata manifesto ya CHADEMA na wala siyo yale ambayo anataka kuyatelekeza kwa mujibu ya manifesto ya Chama chake?
Tafadhali naomba ufafanuzi.
Rev. Kishoka,
Mapendekezo yako ya wizara yametulia sanaa yaani mkuu umekaa chini vizuri sana....kama kawa umefunika!
John Mnyika,
Mulifanya kazi nzuri, nakubaliana na wewe kwa asilimia kama 70%, lakini asilimia 30% hapa...nitaijibu kwa kuweka mbadala wake....
Mapendekezo yangu ni Haya
ORGANIZATION OF THE GOVERNMENT OF THE REPUBLIC OF TANZANIA
-Ofisi ya Rais
-Ofisi ya Makamu wa Rais
-Ofisi ya Waziri Mkuu
-Wizara ya TAMISEMI ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Mwanasheria Mkuu [State Law Office)
-Wizara ya Fedha
-Wizara ya Mipango na Uwezeshaji [Planning and National Development]
-Wizara ya Afya
-Wizara ya Uchukuzi, barabara na Ujenzi
-Wizara ya Elimu na Ufundi
-Wizara ya Elimu ya Juu, Science na Technologia
-Wizara ya Kilimo
-Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi (Livestock and fisheries development)
-Wizara ya Mambo ya Nje
-Wizara ya Regional Affairs (East Africa and SADC)
-Wizara ya Justice and Constitutional Affairs (ikumbukwe uendeshaji wa mahakama administratively uko hapa)
-Wizara ya Jinsia, Michezo, Utamaduni na Ustawi wa Jamii
-Wizara ya Habari na Mawasiliano (Information anc Communications)
-Wizara ya Nishati na Madini
-Wizara ya Utalii na Wanyama Pori
-Wizara ya Maji na Umwagiliaji (Water and Irigation)
-Wizara ya Ushirika, Biashara na Masoko (co-operatives, industry and trade)
-Wizara ya Mali asili na Mazingira (Natural resource and Environment)
-Wizara ya Ardhi na Nyumba
-Wizara ya Kazi na Ajira (Labour and Human Resources Development)
-Mahakama (Judiciary)
-Tume ya Uchaguzi [National Electrol Commission]
-Tume ya Haki za Binadamu
-Tume ya maadili ya viongozi na utawala bora [commission for national ethics and good governance]
-Tume ya Utumishi [comming soon to Tanzania]
-Mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali [National Audit General Office]
-Bunge la Jamhuri [National Assembly]
-Taasisi ya PCCB
Maelezo ya Ziada
-Ustawi wa Jamii umepelekwa kwenye gender, sports, cultural and social affairs
-Mawasiliano imeondolewa kwenye miundo mbinu kwa kuwa kwa mfumo wa sasa haitendewi haki, information [maelezo] imeunganishwa na mawasiliano kuunda wizara.
-Hakuna waziri utawala bora, bali kuna tume ya maadili na utawala bora
-Hakuna waziri anayehusika na Utumishi, kwani kutaundwa tume ya utumishi wa umma.
-Wizara ya Maji, imewekewe na Umwagiliaji
-Wizara ya Kilimo ni wizara likubwa mno limebaki lenyewe
-Mifugo imeongezewa Uvuvi kwa ajili ya ku-take advantage ya mali asili hii tunayoichezea.
-Utalii na Wanyama Pori [Tourism and Wildlife Development], Mali asili sio mahali pake.. Utalii ili upate msukumo... ukiangalia vizuri uvuvi umeondolewa hapa.
-Mali asili sasa iko na Mazingira... in short... unatakiwa kumtoa Mh. Mark Mwandosya kutoka kwenye makamu wa raisi umpe mazingira na mali asili.
Niko tayari sasa kuchukua maswali yenu.
John,
Hivi unataka kusema Rais aunde wizara kwa kufuata manifesto ya CHADEMA na wala siyo yale ambayo anataka kuyatelekeza kwa mujibu ya manifesto ya Chama chake?
Tafadhali naomba ufafanuzi.
Yohana,
Tuangalie Wamarekani, mfumo wao ukoje wa Cabinet? Je udogo wao ni tija au tutadai wao matajiri? je ni lazima kila kitu kiundiwe wizara? hatuwezi kuwa na idara zinazoongozwa na makamishna ambao si wanasiasa?
Nafikiri tatizo letu limekuwa ni huku kudai tunataka kuleta uwiano wa Wateule kufuatilia misingi ya kidini, jinsia, umri na kimikoa (kikabila). Sisi kama Taifa tumepevuka sana na hakuna sababu yeyote kuunda baraza la mawaziri kufuatia hisia kama hizo. Kuendelea kutumia hivo vigezo, ni kukomaza mgawanyiko huo.
Kinachohitajika ni kuunda Baraza dogo ambalo litakuwa makini, fanisi, wajibikaji na adilifu. Unapokuwa na safu kubwa kama iliyokuwepo, kunatoa mwanya wa ubangaizaji na hata kulea mawazo ya hujuma.
Kila wizara iwe na naibu mmoja na ikiwezekana, cheo hiki kisiwe cha kisiasa tena. Nafikiri jambo hili litafanikiwa pindi mabadiliko ya katiba yakifanyika na kuondoa Uwaziri kutoka kwenye Ubunge. Manaibu wasipewe marupurupu sawa na Mawaziri. Manaibu pamoja na makatibu wakuu wawe ni wataalamu wa wizara wanazowekwa na si wababaishaji wa kupiga domo kama Nchimbi (samahani nimeleta jina kama mfano.)
Tukiangalia Wamarekani, baraza lao la Mawaziri huundwa kwa wizara zifuatazo ambazo ni:
source:-http://www.whitehouse.gov/government/cabinet.html
Soma vizuri utangulizi wangu. Sera pekee ya CHADEMA hapo ni kutengeneza baraza la mawaziri dogo lenye ufanisi. Suala la Muundo na mpangilio niliotoa hapo juu ni mawazo yangu binafsi kama mwananchi. Na naamini Rais anawajibu wa kupokea maoni ya wananchi wote tu
JJ
HAYA WAKUU TUENDELEENI KUTUUNDIA BARAZA
SASA MNAUNDA KUTOKEA NA BASIS ZIPI?
JEE MMEPITIA ELIMU YA MAMBO HAYA? AU JUST UTASHI TU?
AU NDOTO ZA ALINACHA?
AU KUBWABWAJA TU?
JEE MSHAWAHI KUPITIA CAUSE HIZI ?
WATANZANIA BWANA KILA MTU MTAALUMA SAWA TUSONGENI BWANA KIWETE NA MIZENGWE NJOONI MCHAGUE SAMPLE MNAYOIONA ITAKUWA SAFI
Unaleta unazi hata kwenye serious issues ?John ame suggest na wewe unaweza kusema yako hajakulazimisha wala JK hajapewa amri.Why jump to conclude ?
REv. Kishoka,
Nakubaliana nawe mia kwa mia hapa mkuu wangu.
Kwanza kabisa pamoja na kutazama mifano ya nchi kama Marekani ni muhimu tujiulize sisi kuwa hivi Tanzania kweli bado ni nchi ya Kijamaa ama tumebadilisha mfumo mzima na kuwa nchi yenye kufuata mfumo wa nchi hizo.
Sasa basi Kama serikali kazi yake ni utunzi wa sheria na kuhakikisha ipo nje ya biashara kama hizi inabidi tutazame ni wizara gani zinazotakiwa kufanya usimamizi badala ya wizara kujihusisha moja kwa moja na Taasisi zinazoendesha biashara nchini kama vile sioni sababu ya kuwa na Wizara ya Utalii ambayo ni biashara badala yake tungekuwa na wizara ya Maliasili na Mazingira. Utalii iwe chini ya Taasisi inayohusiana na masoko na sio Masoko ama Biashara kupewa wizara kamili kwani hapa tutakuwa tunaleta mvutano kati ya wafanya biashara na wizara.
Rev Kishoka na Mkandara
Mfano wa Marekani sio mwafaka wa serikali ya CCM ambayo haifuati sera ya majimbo. Mfano huo ni mzuri chini ya utawala wa CHADEMA. Marekani inawizara chache kiasi hicho kwa sababu federal government inasimamia masuala mapana- masuala mahususi usimamizi wake uko kwenye ngazi ya states.
JJ
So Yohana, we are back to mazungumzo yetu ya Mabadilikoya Katiba! Nilitoa orodha ya Wizara na Mamlaka/Kamisheni. Inabidi kuwe na mfumo wa kuhakikisha kuwa Vibosile wote pamoja na wakuu wa Polisi, Jeshi, Magereza wanapitishwa na Bunge!
Wizara ya Sheria na Katiba inafutwa badala yake majukumu yake ya kiutendaji yanapelekwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni sehemu ya Baraza la Mawaziri. Na majukumu ya Usimamizi wa Sheria yanabaki kwa Mahakama. Majukumu ya kusimamia HAKI, yanabaki chini ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Kweli kabisa. Tunahitaji KATIBA MPYA. Kama tunataka kuruka, lazima tuagane na nyonga!
Kila mjadala tunazunguka lakini tunarudia pale pale, hii yote ni sababu ya kushughulikia athari badala ya vyanzo vya matatizo. Ni ugonjwa wa watu wanaotazama karibu badala ya kutazama mbali. It is a tragedy of thinking short term instead of long term as a nation. CCM's management by crisis and walking around!
JJ
Mnyika, hili theoretically haliwezekani kwani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ni sehemu ya Baraza la Mawaziri lakini siyo Waziri. Na zaidi ya yote yeye anaundwa na sheria tofauti kabisa unless hiyo sheria ibadilishwe kabisa na Mwanasheria Mkuu ndio awe Waziri wa Sheria na Katiba.
Ila kwenye idadi na baadhi ya mergers naalign na wewe zaidi kwani my own take nafikiri lita kuwa kati ya 20 na 23.
Na sitashangaa kuona Usalama na Mambo ya Ndani waunganishwe tena.
Mimi mawazo yangu kabisa tofauti. Ningependa kuona wizara zinaundwa na nyingine kufutwa kama katiba inavyosema, lakini si lazima kuwa na hao wanaoitwa mawaziri. Badiliko ambalo ningeliona bora kabisa ni kwa wabunge wote kurudi bungeni kufanya kazi ya kutunga sheria na kusimamia serikali. Wizara ziendeshwe na makatibu wakuu na wakurugenzi kama zinavyoendeshwa wakati huu ambapo baraza halijatangazwa. Hao makatibu wawe ni watu "waserikali" kweli, watawala na watendaji. Hapo ndio kweli dhana ya bunge kusimamia serikali itakuwepo na kila mhimili wa dola utafanya kazi yake bila mgongano wala maingiliano. Ndiyo, mahakama ziendeshwe na wanasheria (majaji na mahakimu kama ilivyo sasa), serikali iendeshwe na "waserikali", bunge liendeshwe na wabunge (ambao ni wanasiasa wanaotuwakilisha wananchi), na wote kwa pamoja chini ya dola (state) ambayo mkuu wake ni Rais. Sasa hivi tunachokiona ni wabunge kuongoza serikali (katika jina jipya la "waziri"), halafu wakirudi Bungeni wanajisimamia na kujihoji wenyewe (yaani bunge limegawanywa, sehemu fulani ni serikali! Sasa hii haifai). Ilipaswa serikali iwepo bungeni ikiwa kama serikali na si kwa kuchukua sehemu ya wabunge, kama alivyo pale mwanasheria mkuu wa serikali ambaye si mbunge, basi na viongozi wa wizara nyingine ingefaa wakawepo kwa mfumo huo. Kama hili linahitaji marekebisho ya Katiba, JK akileta mapendekezo haya nina uhakika wananchi wengi watayaunga mkono.
Aksante.
Mfano wa Marekani sio mwafaka wa serikali ya CCM ambayo haifuati sera ya majimbo. Mfano huo ni mzuri chini ya utawala wa CHADEMA. Marekani inawizara chache kiasi hicho kwa sababu federal government inasimamia masuala mapana- masuala mahususi usimamizi wake uko kwenye ngazi ya states.