John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 713
- 1,246
- Thread starter
- #41
John Mnyika,
Mkuu hapa utakuwa unakosea kwani hata Marekani chini ya States hakuna wizara hizo. Ni muhimu tuelewe kazi za wizara na Taasisi zinazohusiana na biashara moja kwa moja....
Jimbo la Marekani ni serikali nzima ya Tanzania... na hata hizo States haziwezi kuweka Utalii chini ya serikali kwa hiyo tunachozungumzia sisi ni kutazama umuhimu wa wizara hiyo ktk mazingira yetu. Sii lazima tuwe kama wao lakini ni muhimu zaidi kuiweka serikali yetu iweze kufanya kazi kirahisi na sisi tuwe washindani bora ktk dunia hii ya Utandawazi.
Ndio maana nimepinga sana Azimio la Zanzibar ambalo ktk kuangalia Utandawazi wamefikiria kwanza nafasi ya viongozi badala ya kufikiria nafasi ya serikali ktk dunia ya Utandawazi na soko huria...Kama alivyosema Rev. Kishoka kazi za serikali zinahusiana na kusimamia as regulator na sio mwendesha Taasisi nzima ya vitu kama Utalii, biashara, masoko na kadhalika..Ndio maana tunashindwa hadi leo kupata soko la mali zetu kwa sababu ya Ukiritimba wa wizara zetu.
Mfano mmoja mdogo sana majuzi nilikutana na mmoja wa viongozi wa Loblaws Inc ambao wako interested sana na kahawa yetu hasa baada ya kuiona Africafe....sikufahamu nimwambie nini ikiwa mimi hapa nilijaribu kuitangaza TZ ktk Luninga hapa nimekosa kupata mtu anayehusika na matangazo ya nchi yetu zaidi ya kuambiwa ni ofisi ya rais...
Hii ndio taabu kubwa kuwapa wanasiasa nafasi ambazo zinahusiana na maamuzi ya haraka yasiyohitaji siasa ila akili ya biashara....
Hata hivyo kwa mwenye kuhitaji soko la Kahawa yetu please call this number. 1 888-495-5111 jina la kampuni ni kama nilivyoliandika hapo juu. Wasiliana nao moja kwa moja they are interested.
Mkandara
Soma tena post yangu. Sijasema kuwa hizo Wizara ziko kwenye ngazi ya states- nilichosema ni kuwa federal government inashughulikia masuala mapana. Ndio maana inaweza kuwa na wizara chache tu. Lakini kuna mambo mahususi ambayo usimamizi wake unafanyika kwenye ngazi ya states pekee.
Nakupongeza kwa initiative yako kuhusu soko la kahawa!
Ni kama Tanzania na Zanzibar- utaambiwa hili ni suala la muungano, hili silo hivyo Zanzibar wanawizara zao katika masuala ambayo si muungano. Kama kungekuwa na serikali ya Tanganyika; ni wazi serikali ya Muungano ingekuwa na Wizara chache tu za masuala ya Muungano. Mambo mengine yote mahususi Tanganyika na Zanzibar wangejiamulia wenyewe kila mmoja kivyake. Sasa ile miundo ya usimamizi ya state level, si lazima iitwe wizara- wanaweza kuwa makatibu au makamishna nk. La msingi ni mgawanyo wa majukumu kati ya federal government na state!
Hayo ya Azimio la Zanzibar na masuala ya utandawazi ni mjadala mwingine.
JJ