Baraza Dogo la Mawaziri na Muundo wa Wizara

Unaleta unazi hata kwenye serious issues ?John ame suggest na wewe unaweza kusema yako hajakulazimisha wala JK hajapewa amri.Why jump to conclude ?

HUYU PUNDAMILIA NAYE NA MAMBO YAKE YA VYAMA!

Wakuu Lunyungu na jmushi1
Najua ninyi ni wepesi wa kujibu lakini ninawashauri pia muwe wepesi wa kuelewa mambo.
Swali langu ambalo nilikuwa ninahitaji ufafanuzi nililielekeza mahususi kwa John na amelitolea majibu mazuri kabisa.
Next time mjitahidi kusoma na kuelewa.
 
Nakubaliana kabisa na nia za kuwepo kwa baraza dogo la mawaziri. Kwa kweli JK alichemsha alipounda baraza na kuongeza ukubwa. Kwa hiyo tuki rudi kwenye muundo unaopendekezwa na JMnyika, bado nina matatizo na wizara kadhaa
Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma! Huyu waziri hana kazi, kwani hakuna siasa kwenye utumishi wa umma. Hotuma yake ya bajeti ni mishahara ya watumishiwa umma! Ilichofanikiwa kufanya ni kuua nguvu za vyama vya wafanyakazi. Hii irudi iwe Idara chini ya ofisi ya Rais.

Wizara za maji, mazingira, maliasili na ardhi. Hakuna sababu zozote za kufanya ziwe tofauti. Shughuli nyingi za wizara ya ardhi zinafanywa na halmashauri wizara inaongeza urasimu na kupeleka huduma mbali na wananchi. Wizara hizi zote zina jihusisha na menejimenti ya ardhi na kunaoverlap na migongano mingi. Wazuri mmoja ataweza kuweka muelekeo na haswa kupeleka shughuli nyingi za wizara halmashauri
 
Aisee Mnyika,pongezi nyingi zikufikie kwakua umesema kitu ambacho hata mimi nilikifikiria.Utitiri wa mawaziri sio uwezo suala ni uwezo wa hao walioteuliwa kutatua matatizo ya watanzania. CHONDE JK,PUNGUZA HILO BARAZA LIJALO.
 
Nakubaliana kabisa na nia za kuwepo kwa baraza dogo la mawaziri. Kwa kweli JK alichemsha alipounda baraza na kuongeza ukubwa. Kwa hiyo tuki rudi kwenye muundo unaopendekezwa na JMnyika, bado nina matatizo na wizara kadhaa
Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma! Huyu waziri hana kazi, kwani hakuna siasa kwenye utumishi wa umma. Hotuma yake ya bajeti ni mishahara ya watumishiwa umma! Ilichofanikiwa kufanya ni kuua nguvu za vyama vya wafanyakazi. Hii irudi iwe Idara chini ya ofisi ya Rais.

Wizara za maji, mazingira, maliasili na ardhi. Hakuna sababu zozote za kufanya ziwe tofauti. Shughuli nyingi za wizara ya ardhi zinafanywa na halmashauri wizara inaongeza urasimu na kupeleka huduma mbali na wananchi. Wizara hizi zote zina jihusisha na menejimenti ya ardhi na kunaoverlap na migongano mingi. Wazuri mmoja ataweza kuweka muelekeo na haswa kupeleka shughuli nyingi za wizara halmashauri na sekta binafsi
 
Mh Ukweliii, unajua hata huyu aliyekua waziri wa ajira,kazi na maendeleo ya vijana hatakiwi kurudi kwani alichowafanyia wafanyakazi Tz sio kizuri.
 
Yohana wa Mnyika,

Je umeridhika na muundo huu mpya? Je kipaumbele kwa 80% walioko vijijini kwa kuwa na wizara takribani tatu kuangalia maswala yao ni bora?

Binafsi kuweka msukumo kwenye Kilimo na Chakula, Mifugo na Uvuvi na Maji na Umwagiliaji ni ishara kuwa JK anaweza kuwa anabadilisha mwelekeo na kurudi kwenye Uchumi asili wa Uzalishaji mazao ambao Watanzania wengi watachangia uazalishaji mali na kunufaika.

In fact kupelekwa Mwandosya, Magufuli na hata Msolla, kunania tumaini!
 



kwa kweli kazi ya kugawa wizara kwa nchi maskini na zenye diversity kibao ni kazi ngumu sana!!!hata hiyo classification ya Yohana haiwezi kukidhi mahitaji ya watu kama mnavyo isisifu. kwa nchi kama yetu ugawaji wa wizara hauzingatii majukumu ya serikali peke yake, ila sababu zingine nyingi na muhimu kama uwakilishi wakigeographia, makundi pamoja na misukumo ya kisiasa iliyopo. jaribuni kupitia kitabu cha Richard, Scott huyu ni classical writter wa public administration na amejishughulisha sana na structure of governmnet.

kwa kifupi bidii hii ya kutaka kuwa na wizara fixed ni nzuri ila kwa watanzania naona muda bado. ....... we have a long way to go before comparing our bureaucracy with the old bureaucracies of the developed world. sisi public administration yetu bado iko mbali kutoka ile ya weberian ambayo kwa kiasi kikubwa ndio iliyoshamiri kwenye nchi zilizo endelea.
 
Hapa tunakumbuka shuka wakati tayari kumekucha, kwani JK kasheamua kugagana vyeo na kuendelea kutupa mzigo mzito sana .

Nafikiri hapa jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa tunalijadili baraza hili na mafisadi wote wawekwe hadaharani na wawajibike ama wawajibishwe na nguvu ya ummma .
 
Msingi wa utendaji bora wapasa kuwa kwenye kurugenzi imara ambazo huundwa kuzingatia umuhimu wake na vigezo maalum. HIzi lazima zijengewe hoja bungeni na kupitishwa kisheria kama tukiwa na bunge makini. Kadhalika wizara zipi zisimamie kurugenzi zipi lazima zipendekezwe, zijadiliwe na kupitishwa bungeni. Waziri ana kazi ndogo sana kama mshauri wa kabibu wa raisi katika maswala ye sekta husika kama kurugenzi imara zipo na zinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kisheria. Ufisadi wooote tunaoshuhudia ni matokeo ya mawaziri kujigeuza wakurugenzi kila wanavyojisikia kwa maslahi binafsi. Tukiwa na kurugenzi makini idadi ya wizara twahitaji ndogo sana. 15 ni nyingi.

Ikumbukwe mfumo wetu wa utawala huwapa mawaziri maslahi ya juu na kupita watendaji wote na pia mamlaka na nguvu kisheria ya kuingilia na kuvuruga utendaji wa kurugenzi. Baraza likiwa dogo inapunguza idadi ya wavurugaji.

Kama kweli mawaziri ni washauri wa raisi wa karibu basi wanapaswa kuwa wachache ili aweze kushauriana nao kikamilifu. Wakiwa wengi raisi anakuwa na mawaziri ambao hushauriana nao na wengine humuona tu kwenye vikao na wengine wanaanza hata kuingilia utendaji wa wizara nyingine. Matokeo ni ufisadi kutukuzwa.

Kila muundo mpya wa baraza hufuatwa na kipindi kirefu cha kujipanga na matumizi hovyo ya pesa kujenga au kukarabati majengo na ununuzi wa samani ambavyo hutoa mwanya wa ufujaji na utapeli. Mara nyingi wizara zimeundwa kwa sura ya kumpatia mtu wadhifa na ulaji badala ya utoaji huduma. Hii inaletapelekea wizra moja kuwa na manaibu waziri kadhaa(mzigo usio lazima)Mfano unakuwa na wizara za kilimo lakini na chakula, mifugo, umwagiliaji badala ya moja tu yenye kurugenzi imara zinazosimamia utendaji kitaaluma. Kilimo wanahimiza matumizi ya samadi na kutumia wanyama kazi bila kuwa na wataalamu wa aina ya wanyama na matunzo yake. Tuanjenga tu mivutano. Kilimo anataka kumwagilia lakini mifugo wanataka njia kwenda malishoni na wa umwagiliaji wanasema sasa hivi tunashughulikia ukanda fulani tu kitaifa. Baada ya muda mfupi tunapangua na kuanza tena moja. Hapna tuache. Raisi abaki na uhuru wa kuteua mawaziri lakini idadi ya wa aina ya wizara ziamulike Bungeni kwa kuzingatia usharui wa wataalamu husika kisheria.
Kisingov
 
Rev Kishoka,
In fact kupelekwa Mwandosya, Magufuli na hata Msolla, kunania tumaini

Hata mimi nilifikiria hivyo mwanzoni lakini nikajirudi baada ya kugundua kwamba watu hawa hawa walishindwa kukamilisha waliyopewa mwanzo kwa sababu pakacha letu linavuta sehemu muhimu zaidi.. Wizara ya fedha, Benki kuu, TRA, Bandari, Utalii, Madini na kadhalika. Hizi ni sehemu zinazotuingizia fedha sana na ndizo pekee zinazo weza kutupa mtaji wa kufufua KILIMO...
Sasa basi ikiwa utawaweka wataalam ama watu unaowaamini ktk sehemu zinazotegemea zaidi uimara wa wizara na Taasisi zinazoendesha mtaji wetu sidhani kama dhana yake itamfikisha popote!..
.
Kuwaachisha kazi viongozi kina Lowassa, Mama Meghji na kadhalika sio somo kabisa kwa hawa waliopo leo madarakani isipokuwa inatia moyo zaidi wa CHUKUA CHAKO MAPEMA...
Hawa pia watachukua chao na kufungua Biashara kabla ya miaka mitatu ijayo wakiwa na hofu ndogo ya kujiuzuru ama kuwekwa pembeni 2010...
Kwa hiyo swali kubwa la viongozi (from CCM) ni, umeweza chukua nini ktk wakati uliopewa?...Hapa hakuna cha kilimo wala mjomba wake.
 
Marekebisho kidogo ktk usemi wangu uliotangulia..
Naposema CHUKUA CHAKO MAPEMA sina maana ya viongozi wazuri kama kinndosya na Magufuli ila nina maana ya kuwa wale waliopewa nafasi za wizara ama Taasisi ambazo ndizo zinaingiza fedha zaidi... Ni hatari kubwa sana kwa viongozi kuendelea kufanya biashara chini ya kivuli cha Azimio kwani ni wachache watakao kuwa na moyo wa Uzalendo hasa pale wanapoona kina Lowassa na wengineo wamepita salama na sasa hivi wamejituliza Beach huko Zenj wakitumbuizwa na Sauti za Busara.
Kwa raha zao..
 

Bob Mkandara,

Mara nyingine, inabidi tujiulize viranja wanaweza kufanya kazi vizuri zinazoonekana kuwa njema ikiwa Kiranja Mkuu ni mbabe na kila siku kufukia sauti za viranja wengine kwa Mwalimu Mkuu?

Mwandosya na Magufuli, ni wachapa kazi. Sina uhakika sana na Msolla kutokana na kushindwa kuongoza Wizara iliyopita. Swali ni hivi, ukiondoa utashi wa siasa na woga wa kuvuma kwa hawa jamaa kisiasa na utendaji, Wizara walizopewa ni muhimu sana kwa Taifa letu na nashukuru Mungu kuwa wamepewa hawa jamaa na si wababaishaji wengine.

Uvuvi na Mifugo, Maji na Umwagiliaji na Kilimo na Chakula. Hizi ni wizara nyeti sana kwa maendeleo ya Taifa na nina matumaini makubwa kuwa in long term, tutaona mafanikio ya utendaji na uongozi wa hawa jamaa kwa hizi wizara.
 
Nakusikia mkuu wangu na nakubaliana na maneno yako isipokuwa labda sikueleza vizuri hapo mwanzo...
Chukulia hili sakata la Richmond na BoT yote yamewahusisha viongozi MAWAZIRI... ambao baada ya kuiba pengine kila mmoja wao ni Millionea leo hii kwa kuhujumu uchumi wa nchi..Tazama adhabu zao basi?... Wamestaafishwa kazi!...lakini watakula ruzuku zao kama kawaida.
Kwa hiyo, hawa wote waliochaguliwa sasa hivi watakuwa na funzo moja kubwa sana nalo ni chukua chako mapema kisha ukikamatwa utastaafishwa kazi bila kufika mahakama wala kupoteza mamillioni uliyopoteza..
Hivyo basi kila mmoja wao atajaribu kuchuma mapema kabla ya 2010, na hao mawaziri wazuri kama Magufuli na huyo Mwandosya watapata wapi fedha za kuendeleza miradi hiyo unayoisema?...
Bila kuwaadhibu viongozi waliotuibia badala yake JK kawatetea kuwa walikuwa ni viongozi wazuri sana maneno mazito na tofauti kabisa na ilani ya chama chake wala ya Kitaifa... Hapo uncle bado una tegemeo na hawa watu wawili sijui watatu ambao wamewekwa kama kichombezo?
 

Mnyika wasalaam

Kwanza nakupongeza kwa kujaribu kuibua mjadala huu kwani ndo wakati wenyewe.Tunapokua na mawaziri wengi automatically gharama za kuendesha wizara hizo ni kubwa na cha kusikitisha hapa kwetu haziendani na matunda ya wizara husika.Naunga mkono tuwe na wizara chache makini na mawaziri wenye wito kweli wa kutumikia wananchi.Unaweza pia kuwa na wizara chache but mambo yasiende kama mawaziri hawatakua commited vya kutosha.
 


Wizara ya Mambo ya ndani na usala wa raia hujaitaja au macho yangu??????????
 
Wooote mna mawazo madogo baada kusema kurekebisha mawaziri kwanza huyu hafai huyu anafaaa matokeo yake mnapanga wizara hii kazi siyo yenu ni ya waziri mkuu na mkuu wa nchi.
 
Kama watu wanaofanya kazi za umma wengi wangekuwa proactive katika kutimiza wajibu wao, basi idadi ya mawaziri ingeweza kuwa ndogo bila tatizo lolote.Isipokuwa pia ni lazima tukumbuke kuwa wengine wapo ndani ya nafasi ambazo zimetengenezwa ili baadhi ya waliohadiwa hafasi hizo wapate kazi
 
Hoja ni nzuri sana ila naelewa kwamba baraza la mawaziri siku zote litaendana na ilani ya uchaguzi ya chama kilichoshinda uchaguzi.serikali ipo kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama kilichochaguliwa na wananchi.
 


Hii nimeikubali mkuu. Sasa tuangalie vichwa vitakavyopewa ulaji kwenye hizi wizara zako

1-wizara ya uchumi na mapato ya taifa-Waziri Kihiyo Mkulo
2-wizara ya rasilimali na maliasili-Anaweza kupewa Makamba
3-wizara ya demokrasia na muungano-Nasikia Tambwe atagombea ubunge anaweza kuzawadiwa hii nafasi

4-wizara ya sheria na haki- Rosti hamu Aziiiiiiii-ziiiii

5-wizara ya ulinzi-Serukamba
6-wizara ya miundo mbinu-Stella Manyanya
7-wizara ya uwezeshaji na uwekezaji- Sofia Simba
8-wizara ya chakula na afya- Aisha Kigoda
9-wizara ya mambo ya kimataifa-Membe
10-wizara ya mafuta na umeme-Mwangunga
11-wizara ya elimu na tekinolojia-Lau Masha
12-wizara ya utamaduni na michezo-Kama kawaida Nchimbi
13-wizara ya kazi na maendeleo ya vijana-Zitto Kabwe (Endapo mpango wake wa kuhamia CCM utakamilika mapema)
14-wizara ya jamii na watoto-Kweygir
15-wizara ya mambo ya ndani-Adam Malima

Manaibu mtanisaidia.............
 
Kazi nzuri sana Kaka yangu Mnyika na pia itakuwa ni vizuri kama mapendekezo kama haya ungeandika kwa rais ay barua kwake ile mwakani mtu yoyote yule anaweza kufanya mambo kama haya kuliko na kuwa baraza au yote haya yaingie kwenye katiba ya Taifa ya nchi maana kila mwaka tumeona kuwa mambo yanabadika kila siku na kufanya au kupoteza resources za taifa la Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…