Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Maneno yako mazito green naamini JK atayapata kabla hajalala usiku huu . Ndiyo maana naipenda JF .
 
Kwa upande wangu sikuwa dissapointed na hili baraza kwa sababu tangia mwanzo sikuwa na mategemeo ya kitu kipya. Kifupi I had no legitimate expectations kwamba JK will make a meaningful changes. Kuna wale watakofikiri kwamba tunaponda tuu hatusemi mazuri kwa muungwana, lakini ukweli unabaki pale pale na wengine tunaandika hapa simply because hawa mawaziri wanalipwa kodi zetu na wengi wao utendaji wao tunaufahamu. We are the ultimate victims of their incompetence and hopeless decisions. A person like Chenge sioni lolote alilolifanya..a simple test ya barabara ya Sam Nujoma ambayo ni KM hazifiki tano mpaka leo inaingia mwaka wa tatu haijaisha...sasa jamani ataweza kutengeneza ya Lusahunga to Kasulu/Kibondo? ambako sidhani kama ameshawahi hata kufika?, si Raisi anatudanganya? au?

Well, he knows better as he or his apologetics would want us to believe, but if this is the so called "dream team" I honestly dont see any hope for the future! Mwinyi ni daktari..leo yuko Ulinzi..kweli with critical shortage ya madaktari are we not under ustilizing the little we have for political expediency? You guys, Kikwete has had enough experience to know this...we are no longer in the age of trial and error! JK ought to be more serious.

And it seems we dont have consistency in governance..though we had had the same ruling party...this is the man who came to power and established gazillion of ministries...only to find out that it was a futile decisions (he wanted to reward his people?)..sasa leo anazifuta some of those wizara..vipi kuhusu policies ambazo wameshaanza kutengeneza na mengineyo....Jamani sijui when shall we really start working for this country, maana naona kila kiongozi yuko kwenye majaribio..

The good side I see is the exclusion of Meghji, Mwapachu, Mramba, Diallo ET AL! And perhaps with Magufuli incharge of our fish pale home (mwanza)..we are not going to eat MAPANKI anymore..Lol!

By the way Mwanakijiji is Masha a "Dr" I know is the LL.M graduate from Georgetown! When and where did he get his udokta? (atleast this was a more sensible appointment...)

NB: Tuweke CV za hawa wateule tuzichambue na kuangalia record zao....(kwa wale ambao hatuwajui....)

Masanja wasema kweli...wengi wetu tulikuwa tumejitayarisha kwa dissapointment, maana hapa ketegemea miujiza ni sawasawa na kumlinganisha JK na Mahatma Ghandi....very very remote resemblance.

Alichofanya cha maana ni angalau kupunguza msululu wa wizara kibao ambazo kwa kweli hazina kichwa wala miguu! Labda kuwekwa kwa Mh. Masha kunaweza kuashiria some changes....let's see.

All in all, hawa wazee walojitoa (au kuondolewa), ni bora tu. Meghji being outis a great relief!
 
..kwa haraka haraka, niko-disspointed na wizara ya fedha. kwa kweli tunahitaji a reputable technocrat with international exposure kuongoza hiyo wizara. nilitegemea atateuliwa mtaalamu anayeweza kwenda pound-for-pound na watu kama Dr.Ndulu wa BOT, Dr.Dau wa NSSF, na Dr.Mboya wa CMSA.

..wizara ya utalii na maliasili nayo inahitaji watu energetic na creative kuitangaza Tanzania ktk mazingira ya utandawazi. pia panahitajika mtaalamu wa masuala ya wanyama na conservation kama naibu waziri. sidhani kama Raisi amelizingatia hilo.

..kuna mawaziri/naibu wenye sifa kama Dr.Kawambwa,Prof.Mwakyusa,Martin Chikawe,Chrisptopher Chiza[mtaalamu wa irrigation], Mary Nagu[ukiondoa udaktari feki].

..halafu Balozi Kagasheki si alikuwa na matatizo ya tuhuma za rushwa geneva? JK amemteua wa nini kuwa naibu waziri mambo ya ndani?

..Dr.Hussein Mwinyi amepewa wizara nyeti. nadhani huyu anaandaliwa kwa nafasi kubwa zaidi. Huenda akamrithi Karume au Kikwete.

..viongozi wa CCM wa baadaye ni kama Dr.Laurian Masha,Dr.Hussein Mwinyi, Dr.Deusdedit Kamala,Dr.David Mathayo,Dr.Ngeleja,Dr.Adam Malima,Dr.Cyril Chami. hawa ndiyo watakaopambana na kina Mwanakijiji,John Mnyika,Kitila Mkumbo, na Zitto Kabwe.
 
Hili Baraza bado linatoa ajira ya kudumu hapa JF.
Wana JF, kuna uchafu mwingi tu kwenye hili Baraza. Watu kama malima wamepelekwa kule kubariki project zao za wizi kwenye Gas ya Mkuranga.

Kweli Membe sijaona tatizo kwenye ufisadi lakini, domo lake litamponza siku moja.

Chenge ndani ya nyumba???!!
Huyu ni Fisadi anatafuta nini bado kwenye Baraza?

Kuna huyu jamaa anaitwa Mustafa Mkullo.
Huyu ndo yule alikuwa NSSF?
Huyu alifanya malolosa mengi sana akiwa kule Akiba ya Wafanyakazi kwa kuchezea fedha za wafanyakazi.
Kumpa wiazara ya Fedha ni kumruhusu kucheza na fedha za wananchi wote.
Mbuzi mwenye njaa kaachiwa mkeka, utapona kweli?
Kabla hata hajaanza hiyo kazi yake tayari Mustafa Mkullo anaharufu ya Ufisadi.
Ana uwezo wa kufanya kazi ndiyo , lakini ni Kibaka mwenye kila dalili ya kulinda na kuwa Fisadi.
Hatutaki majangiri kwenye baraza la mawaziri.

Tanzania kuna watu kibao, lakini ndani ya SISIEMU hakuna watu kabisa, kuna wezi vibaka,wazinzi, mafisadi, wauaji,majangiri, mamluki, mahabithi, wenye mioyo ya korosho, waongo,wagomvi na wazee walo jaa mvi kibao na wenye tamaa kumzidi Fisi.

Nyani ataendelea kukomwa hapo jirani mikumi kama kazi.

Masha huyu ni kijana wa Mixed interests.
Ni kijana, ndiyo, lakini nadhani analipiza hata yale wazazi wake waloyakosa kwa kukimbia nchi yeye akiwa kichanga.

Shule ipo lakini hatusaidii.

tatizo la SISIEMU kuwa na Wabunge CRIMINALS wengi linafanya iwe kazi kweli kweli kuchagua Mawaziri. Lakini hata hivyo kuna watu wengi wenye uwezo wa kushika madaraka wameachwa kwa sababu ambazo JK mwenyewe anajua.

Sura nyingi za wabunge wa SISIEMU ni za wizi wizi tu.

CV zao ndo kichekesho kweli, fikiria hata safari za kwenda kushangaa majuu wameziweka kwenye CV??? Ha! ha! haha ha!

Hakuna haja ya kusubiri utendaji wao ili tujue uwezo wao.Baraza hilo litasusua litatapatapa ili mradi kipindi cha miaka 2na miezi 8 ipite uchaguzi mwingine uje.

JMK bado anaendelea kutunywesha Gongo la Bagamoyo kwenye chupa ya Konyagi.
 
Ngoja niwape muda kidogo nione utendaji wao.

Hata hivyo serikali hii bado ni kubwa sana. Nadhani waliotuletea majina labda kuna makosa kidogo kwa vile sioni mantiki ya kuwa na wizara mbili zifutazo, kwangu mimi hii ingekuwa wizara moja ambayo ningeiunganisha na madini, kwa vile madini nayo ni sehemu ya maliasili. Tumezowea kudhani kuwa maliasili ni wanyama pori na misitu tu na kusahahu kuwa madini nayo ni mali asili.

4. WIZARA YA UTALII NA MAZINGIRA DK. BATILDA BURIANI
19. MALIASILI NA UTALII WAZIRI NI SHAMSA MWANGUGA NAIBU EZEKIEL MAIGE

Halafu baada ya kutenganisha nishati na mdini, ningeunganisha maji, nishati na miundo mbinu kuwa wizara moja.

15. WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI WAZIRI PROFESA MARK MWANDOSYA NAIBU ENG. CHRISTOPHER CHIZA
22. WIZARA YA NISHATI NA MADINI WAZIRI WILLIAM NGELEJA NAIBU ADAM MALIMA

Kwa vile mawasiliano ni sehemu ya miundombinu, hakuna haja ya kwa na wizara inyojitegemea kushughulikia mawasiliano. Badala yake tungeendelea kuwa na Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kama kawaida

11. WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA WAZIRI SHUKURU KAWAMBWA NAIBU NI DK. MAUA DAFTARI

Ofisi ya Rais yenyewe ni kubwa, kwa hiyo kuipa mawaziri wawili tena ni mzigo zaidi kwa wananchi. Sioni mantiki ya kuwa na mawaziri wafuatao:

1. WAZIRI OFISI YA RAIS (UTAWALA BORA SOFIA) - Sophia SIMBA
2. WAZIRI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UMMA) HAWA GHASIA

Vile vile mambo ya tawala za mikoa yanatakiwa yawe chini ya ofisi ya Waziri Mkuu; hili ndilo jukumu namba moja la ofisi hiyo. Kwa hiyo wizara hizi mbili ni redundant:

5. WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA NA URATIBU WA BUNGE) WAZIRI PHILIP MARMO
6. WIZARA YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA WAZIRI STEVEN WASSIRA NAIBU SELINA KOMBANI

Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ni sehemu ya mambo ya nje, kwa hiyo wizara hizi mbili zilitakiwa ziunganishwa.

21. WIZARA YA MAMBO YA NJE USHIRKIANO WA KIMATAIFA WAZIRI NI BENARD MEMBE NAIBU SEIF ALI IDDI
25. WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI DK. DEODATUS KAMALA

Sana sana, ndani ya Wizara ya mambo ya nje kungekuwa na idara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, labda kukiwa na naibu waziri.

Wizara ya kilimo haina uhusiano kabisa na mambo ya ushirika. Katika mfumo wa kibepari tuliojenga, hakuna haja ya kuwa na idara inyohusika na ushirika. Kama ni lazima kwa vyama vya ushirika kusimamiwa na serikali, basi shughuli hiyo iwe chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Baada ya hapo, wizara hizi ziunganishwe:

16. WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA, USHIRIKA WAZIRI PROF. PETER MSOLLA, NAIBU DR. MATHAYO DAVID MATHAYO
18. WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI WAZIRI JOHN POMBE MAGHUFULI NAIBU JAMES WANYANJA

Halafu kuwepo kwa wizara za sheria na mambo ya ndani kweli huwa ni kujipa mzigo tu. Ningeshuri kuwa wizara hizi ziunganishwe:

20. WIZARA YA MAMBO YA NDANI DR. LAWRENCE MASHA NAIBU NI HAMISI KAGASHEKI
23. WIZARA YA SHERIA NA KATIBA MH. MATHIAS CHIKAWE

Wizara zifuatazo zinajitosheleza kwa hiyo hazihitaji kuundwa tena.

7. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAZIRI MUSTAFA MKURO NA MANAIBU NI JEREMIH SUMARI NA OMARI YUSUF MZEE
8. WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAZIRI PROFESA DAVID MWAKYUSA NAIBU NI AISHA KIGODA
9. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WAZIRI JOHN CHILIGATI
10. ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI WAZIRI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE NAIBU GAUDENSIA KABAKA NA MWANTUMU MAHIZA
13. WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO WAZIRI KAPT. GEORGE MKUCHIKA NAIBU JOEL BENDERA
14. WIZARA YA KAZI, AJIRA NA MAENDELEO YA VIJANA WAZIRI PROFESA JUMA KAPUYA NAIBU HEZEKIA CHIBULUNJE
17. WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO WAZIRI MARGARETH SITTA NAIBU NI DR. LUCY NKYA
24. WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DK. HUSSEIN MWINYI NA NAIBU EMMANUEL NCHIMBI
26. WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO DK. MARY NAGU NAIBU CYRIL CHAMI

Kufanya hivyo, Rais atapunguza idadi ya Mawaziri kutoka hao 25 hadi 17. Hiyo ni nafuu sana kwa mwananchi.

Manaibu waziri wengi ni redundant. Ni Wizara chache sana zinazohitaji kuwa na Naibu Waziri, kwa mfano Wizara ya mambo ya nje itahitaji naibu waziri ambaye atashughulikia swala la Afrika ya Mashariki tu.
 
Shukran,Mheshimiwa Rais-kipindi chakulipa fadhila kimeisha sasa nikazi mbele kwambele.
Tulizoea sura ya Mwapachu na Mh.Kingunge naleo umechagua wachapa kazi wengine.
Alokutangulia(BM) hao aliwaita ASKARI WA MIAVULI sassa sijui wewe utawaitaje labda tuwaite JESHI LA UOKOVU.
 
..kwa haraka haraka, niko-disspointed na wizara ya fedha. kwa kweli tunahitaji a reputable technocrat with international exposure kuongoza hiyo wizara. nilitegemea atateuliwa mtaalamu anayeweza kwenda pound-for-pound na watu kama Dr.Ndulu wa BOT, Dr.Dau wa NSSF, na Dr.Mboya wa CMSA.

..wizara ya utalii na maliasili nayo inahitaji watu energetic na creative kuitangaza Tanzania ktk mazingira ya utandawazi. pia panahitajika mtaalamu wa masuala ya wanyama na conservation kama naibu waziri. sidhani kama Raisi amelizingatia hilo.

..kuna mawaziri/naibu wenye sifa kama Dr.Kawambwa,Prof.Mwakyusa,Martin Chikawe,Chrisptopher Chiza[mtaalamu wa irrigation], Mary Nagu[ukiondoa udaktari feki].

..halafu Balozi Kagasheki si alikuwa na matatizo ya tuhuma za rushwa geneva? JK amemteua wa nini kuwa naibu waziri mambo ya ndani?

..Dr.Hussein Mwinyi amepewa wizara nyeti. nadhani huyu anaandaliwa kwa nafasi kubwa zaidi. Huenda akamrithi Karume au Kikwete.

..viongozi wa CCM wa baadaye ni kama Dr.Laurian Masha,Dr.Hussein Mwinyi, Dr.Deusdedit Kamala,Dr.David Mathayo,Dr.Ngeleja,Dr.Adam Malima,Dr.Cyril Chami. hawa ndiyo watakaopambana na kina Mwanakijiji,John Mnyika,Kitila Mkumbo, na Zitto Kabwe.

Jokakuu,

Mkuu hii analysis yako imeenda shule kichizi. I wish hii post yako angeiona JK kabla ya kutangaza baraza lake lakini wapi water under the bridge....

Huko nyuma tuliwahi kupiga kelele sana kuwa tatizo sio tu ufisadi bali kufuja pesa za umma, kushindwa kumpanga mtu kwa nafasi yake nako kuna tugharimu sana.

Huna haja ya kwenda mbali kuliona hili kila mtu anajua utendaji wa Sarungi pale afya, Maghufuri pale ujenzi to mention the few.

Nachelea kusema mengi kuhusu baraza hili jipya lakini honestly kwa maoni yangy kuna mkorogo mwingi lakini hili la Mkulo kuwa Fedha, kurudishwa kwa Chenge, Msola, Kapuya nk nina cast big doubt lakini lets wait and see
 
Masatu to wait and see ni jambo zuri lakini tutajikuta katika gharika kama hili la juzi hata Spika anataka kurusha chin josho .Do we need that again?
 
Masatu,

..I was hoping for a "DREAM TEAM". I dont think i can refer this cabinet as such.
 
Hongera sana mh RAIS kwa barza lako ila kumuweka ndani ya baraza lako mh MARMO umechafua kabisa ,sikulaumu ila nadhani haukushauriwa vyema,MARMO ni FISADI,aliuza hadi mbuga ya wanyama ambalo ni eneo la WAHAZABE,na kuwauzia mtoto wa mfalme wa SAUDIA na kupew pesa nyingi tu kwa ajiri ya UCHAGUZI wa ubunge na kujikampenia katika jimbo lake, na USHAHIJI ninao,pia ni mtu anayependa hata pesa ndogondogo,za dili na waharifu,na hata kama umepewa UWAZIRI, chonde chonde MH WAZIRI MKUU MTEULE MIZENGO PINDA mwangalie MARMO kwa jicho la TOFAUTI tena katika UANGALIZI MKUBWA,asikuchafulie ofisi,aidha nakushauri fuatilia DATA zake UTAKUBALIANA NAMI.
 
Jokakuu...

mwenzako hapa nimekosa kabisa cha kusema ila tu ninafurahi Mramba ametoka na labda watanzania watapumzika kula nyasi!

Anti:

Mramba anatoka kwenye mojawapo ya majimbo ya watu waliosoma sana Tanzania. Kuna watu kutoka jimboni kwake hapa JF ambao hawataki yeye kuwa kwenye baraza la mawazari lakini wanamchagua kuwa mbuge. Je huoni kuwa matatizo mengine yako-down kwa sisi wananchi?
 
Hongera sana mh RAIS kwa barza lako ila kumuweka ndani ya baraza lako mh MARMO umechafua kabisa ,sikulaumu ila nadhani haukushauriwa vyema,MARMO ni FISADI,aliuza hadi mbuga ya wanyama ambalo ni eneo la WAHAZABE,na kuwauzia mtoto wa mfalme wa SAUDIA na kupew pesa nyingi tu kwa ajiri ya UCHAGUZI wa ubunge na kujikampenia katika jimbo lake, na USHAHIJI ninao,pia ni mtu anayependa hata pesa ndogondogo,za dili na waharifu,na hata kama umepewa UWAZIRI, chonde chonde MH WAZIRI MKUU MTEULE MIZENGO PINDA mwangalie MARMO kwa jicho la TOFAUTI tena katika UANGALIZI MKUBWA,asikuchafulie ofisi,aidha nakushauri fuatilia DATA zake UTAKUBALIANA NAMI.

Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake, kama vipi peleka basi hivyo vidhibitisho basi naye atolewe nduki, sio unakaa chini na kulalama tuuuu!!Safari moja huanzisha nyingine, show us an example for us to later follow on
 
Unajua wakati mwingine ukiwa huna information unaamini ulichonacho ndio BEST.

Kenya na Uganda wana Wizara moja ya Elimu!!! Naomba nikusaidie na hii ya Uganda

Pia kuwa makini kidogo kusikiliza yote kwa makini. Wizara hii ina Manaibu wawili...

1. Kabaka --- ambaye atashughulikia elimu ya juu....
2. Mahiza --- Ambaye atashughulikia elimu ya awali, primary, Sekondari na Ufundi
3. Kila wilaya itakuwa na maafisa Elimu wawili... wa awali na primay... na wa Sekondari na Ufundi... details will follows... later

Sasa wewe umewahi kuona wapi unajilinganisha na wagonjwa wenzako ambao wanaumwa zaidi. Sisi ndio tunaongoza kwa elimu ya juu East Africa halafu unataka kutulinganisha na waganda na wakenya! Haya tuwaambie ile report iliyoletekeza wizara hizi mbili kutenganishwa nini leo kimepungua au kuongeza kiasi kwamba tunarudi miaka 1980? Unaongelea Naibu Waziri, hujui kama mtu kama huyo hata kwenye mikutano ya cabinet haingii? Ninaelewa vizuri sana maana ya elimu na elimu ya juu na ninaongea hili with great intellectual authority wala sihitaji kusubiri maelezo ya ziada ya JK ili kuelewa!
 
Hongera sana mh RAIS kwa barza lako ila kumuweka ndani ya baraza lako mh MARMO umechafua kabisa ,sikulaumu ila nadhani haukushauriwa vyema,MARMO ni FISADI,aliuza hadi mbuga ya wanyama ambalo ni eneo la WAHAZABE,na kuwauzia mtoto wa mfalme wa SAUDIA na kupew pesa nyingi tu kwa ajiri ya UCHAGUZI wa ubunge na kujikampenia katika jimbo lake, na USHAHIJI ninao,pia ni mtu anayependa hata pesa ndogondogo,za dili na waharifu,na hata kama umepewa UWAZIRI, chonde chonde MH WAZIRI MKUU MTEULE MIZENGO PINDA mwangalie MARMO kwa jicho la TOFAUTI tena katika UANGALIZI MKUBWA,asikuchafulie ofisi,aidha nakushauri fuatilia DATA zake UTAKUBALIANA NAMI.

-----------------------------------------------------------------

Very interesting. Pray tell us more. Weka argument na evidence kati ili tuvijadili.
 
Anti:

Mramba anatoka kwenye mojawapo ya majimbo ya watu waliosoma sana Tanzania. Kuna watu kutoka jimboni kwake hapa JF ambao hawataki yeye kuwa kwenye baraza la mawazari lakini wanamchagua kuwa mbuge. Je huoni kuwa matatizo mengine yako-down kwa sisi wananchi?

Nadhani mkuu umechelewa kidogo sana katika hii discussion ambayo iliendelea sana miezi michache iliyopita ambayo iliuliza swali kuwa waafrika ndivyo tulivyo? Ninavyokumbuka hatukufikia mwisho lakini consensus ya wengi ilielekea kwenye conclusion yako!
 
I am not overly excited, but I believe this is a good start.
1. Kwanza amewatoa Meghji na Mramba. Mramba amekuwa mzigo kwetu kwa miaka mingi sana. Meghji anahusika na sakata la BOT.
2. Wananchi wamelalamika sana kuhusu ukubwa wa serikali, na imepunguzwa kiasi.
3. Kwa kifupi mafisadi wengi wametolewa, na ninaamini Chenge yuko njiani. kama siyo buzwagi atashikwa tu kwenye maswala ya mkapa

Nadhani si halali kumtegemea Rais afanye mabadiliko yote ambayo kila mtu anataka. Lets give him the benefit of the doubt, na tuone itakuwaje. To start with ninategemea tatizo la maji litashughulikiwa sasa.
Naona watu wanalalamika tu as if kila alichokifanya ni kibaya, i think ni afadhali ku analyze mazuri na mabaya. Tusifie yale mazuri, then tuendelee ku criticize yale mabaya.
Sometimes i get the impression kwamba watu hawatakaa waridhike no matter kitu gani kinafanyika.
 
Embu tuwekee data humu maana hii ni JamboForum, bila ku-back up unachosema inakuwa uzushi tu, weka vielelezo humu, kumbukeni JamboForum ilimuangusha Lowassa siyo kwa maneno tu, ila kwa vielelezo.
 
BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI NI:

Ofisi ya Rais
Utawala Bora-Sophia Simba
Menejimenti ya Utumishi wa Umma-Hawa Ghasia.

Ofisi ya Makamu wa Rais
Muhammed seif Khatib
Mazingira-Dk Batilda Burian

Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri wa Nchi (Sera), Uratibu na Bunge)-Philip Marmo.
Waziri wa Nchi (Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa)-Steven Wassira. Naibu Waziri-Celina Kombani.

Mipango na Fedha
Mustafa Mkullo
Naibu Waziri-Jeremia Sumari
Naibu Waziri-Omar Yusuf Mzee.

Afya na Ustawi wa Jamii
Profesa Mwakyusa
Naibu Waziri-Dk Aisha Kigoda

Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
John Chiligati

Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Profesa Jumanne Maghembe
Naibu Waziri-Gaudensia Kabaka
Nabu Waziri-Mwantumu Mahiza

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Dk Shukuru Kawambwa
Naibu Waziri-Dk Maua Daftari

Mindombinu
Andrew Chenge
Naibu Waziri-Dk Milton Mahanga

Habari, Utamaduni na Michezo
George Huruma Mkuchika
Naibu Waziri Joel Bendera

Kazi, Ajira na Maendeleo ya vijana
Profesa Juma Kapuya
Naibu Waziri-Hezekiah Chibulunje

Maji na Umwagiliaji
Profesa Mark Mwandosya
Naibu Waziri-Christopher Chiza.

Kilimo, Chakula na Ushirika
Profesa Peter Musola
Naibu Waziri-Dk Matayo David Matayo.

Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Margareth Sitta
Naibu Waziri-Dk Lucy Nkya

Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
John Magufuli
Naibu Waziri-Dk James Wanyancha

Maliasili na Utalii
Shamsa Mwangunga
Naibu Waziri-Ezekiel Maige

Mambo ya Ndani
Lawrence Masha
Naibu Waziri-Hamisi Kagasheki

Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Bernard Membe
Naibu Waziri-Seif Ali Iddi

Nishati na Madini
William Ngeleja
Naibu Waziri-Adamu Malima.

Katiba na Sheria
Mathias Chikawe

Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Dk. Hussein Mwinyi
Naibu Waziri-Dk Emmanuel Nchimbi

Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dk. Deodorius Kamala
Naibu Waziri Mohamed Aboud

Viwanda Biashara na Masoko
Dk Mary Nagu
Naibu Waziri-Dk Cyril Chami

Maoni yangu:
1. Miundo mbinu,Nyumba na makazi ilitakiwa kuwa wizara moja
2.Mambo ya ndani,katiba na sheria ilitakiwa kuwa wizara moja
3.Kazi ajira,maendeleo ya vijana,jinsia na watoto hii ilitakiwa kuwa wizara moja
4.Maji,kilimo,umwagiliaji,chakula hii ilitakiwa kuwa wizara moja.

Kwa uchambuzi wangu wa haraka tayari wizara nne hazikuwa na umuhimu wowote kuwepo badala yake zingekuwa vitengo tu ndani ya wizara nyingine.Ila kwa sababu nafasi lazima zitengenezwe ndo maana bado mzigo wa wizara utaendelea hata kama hakuna tija.Nafikiri Mrisho hana nia ya kuwahurumia walipa kodi bali amesukumwa tu kupunguza mawaziri kwa hiyo anajitahidi kuwa katikati 'awalizishe kidogo wabongo-danganyika na pia marafiki wasikose ulaji.Mambo mengine ni longolongo tu
 
Back
Top Bottom