Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,630
- 4,253
Baraza la Mawaziri limekuwa gumzo hasa; nasikia JK anafanya mawasiliano na Wapinzani kuwa ndani ya Baraza, sijui ni za kweli soma Tanzania Daima ya leo.
Ndo taarifa nilizopewa na 'mwandishi wetu' aliye Dodoma. Inashangaza RTD nasikia wao wanadai 'taarifa za baraza jipya la mawaziri zitawajia pindi tukipata mawasiliano na Dodoma'.
Ingependeza mheshimiwa Rais angeweka pembeni tofauti na akaangalia ndani ya wapinzani wale wanaotufaa kuwa mawaziri na akawapa fursa ya kuwatumikia watanzania. Huo ndio uzalendo! Siamini kama wapinzani hawawezi...
Ni fursa nzuri sana kwa JK kurekebisha makosa

Swafi kabisa Mr ZeroSasa akichukuwa upinzani nani atapiga kelele bungeni. Hawa jamaa wa CCM wanatufanyia mazingaombwe tu. Akina Anna Kilango-Malecela sasa wanatafuta ujiko. Wakati Kabwe na Silaa wanawasha moto wao walikuwa wapi? Wanataka kusema hawakuwa wanazijua hizi skandali. Bado kuna ufisadi mkubwa unaendelea TZ, hivyo wapinzani wazidi kufichua.
Hapana invisible, sidhani kama chama tawala kimeishiwa watu hadi kufikia kuhitaji kukopa kutoka kwa wapinzani! Naamini CCM inao watu wa kutosha na waadilifu wa kupewa hizo nafasi za uwaziri. Wapinzani waendelee kufanya bidii, na siku moja inshaallah watashinda nao wataunda serikali yao. Mazingira ya sasa hivi hayatoi sababu yoyote ya kuunda serikali ya mseto, CCM ni chama tawala na kina asilimia kubwa sana ya wabunge. Upinzani ndio minority Bungeni. Sasa kama Rais atachukua tena hao minority awape uwaziri, atakuwa amezidi kufifisha upinzani. Awaache wapinzani waendelee kuisahihisha na kuikosoa serikali bungeni.
Baraza la Mawaziri limekuwa gumzo hasa; nasikia JK anafanya mawasiliano na Wapinzani kuwa ndani ya Baraza, sijui ni za kweli soma Tanzania Daima ya leo.
mi naona kazi ni ngumu kwani kumtemesha mtu chakula ni ngumu sana,ila ngoja tusubili tuone.JK naye akichagua sana hawezi kuwapata mawaziri walio timilika kwa sababu kila waziri anatuhumiwa kwa njia moja au nyingine kuhusika na ufisadi
Kuna taarifa kule Rock City eti watu wameandaa party Diallo akimwagwa wafanye sherehe ng'ombe zimeandaliwa watu wale nyama. Hawa naona wana matatizo na wivu binafsi Huyu EL kaiba hela hatuoni kaziivest wapi? na yule mtoto wake akitanua tu lakini Diallo kaleta ndege hadi nauli zimekuwa nafuu bora!!! WIVU TU

Inaelekea kazi ya panga pangua imekuwa ngumu kutokana na kuwa rais anatakiwa kuhakikisha hawapi nafasi tena wanao-hisiwa (ama kutambulika kwake) kuhusika na ufisadi wa aina yoyote. Kumbuka ripoti ya BoT anayo na anawajua wahusika kadhaa wanaoguswa nayo.
Ni mawazo tu
Swafi kabisa Mr Zero
Hao kina Malecela nd'o wanaitwa 'Johnny-come-lately'.Yaani wakisema hawakujua hizo skendo ni kama kututusi sie wabongo.Wewe na mie tunazijua na wao wakubwa wetu hawajui?Isshhhhhhhhhhhhhhh!!!!Huo ni uongo ulioje jamani?
Wivu tu? are you sure? Sasa wewe ndugu una hakika huyo jamaa hizo pesa amepata kutokana na mshahara wake au biashara zake halali? Unajua kama kusingekuwa nan ufisadi Tanzania hali isingekuwa ovyo kama ilivyo sasa? Ni hakika watu wa mwanza si wendawazimu wameurahie mabaya yanapomfika mwanamwanza mwenzao!