Baraza ka Kiswahili (BAKITA) badilisheni rangi zenu zinatuchanganya

Baraza ka Kiswahili (BAKITA) badilisheni rangi zenu zinatuchanganya

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Huko twittani nimekuwa nakumbana na post mbalimbali za Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA). Inaonyesha wanaongeza kasi ya kuonekana katika mitandao. Nawapongeza kwa hilo.

Tatizo moja ninaloliona ni kuwa kila mara nikiziona post zao, mara moja nadhania ni habari kutoka Mamlaka ya Mapato, TRA maana rangi wanazotumia zinafanana sana.

Nadhani kwa BAKITA hizi rangi za njano na nyeusi ingekuwa vyema wangezibadilisha ili kuepuka huu mkanganyiko. Wawaachie TRA maana ndiyo tumeshazoea wao kutumia hizo.
 
Back
Top Bottom