baraza la katiba CHADEMA mjini Sumbawanga, Mh. Mbowe na Mh. Lissu

baraza la katiba CHADEMA mjini Sumbawanga, Mh. Mbowe na Mh. Lissu

fukujima

Senior Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
109
Reaction score
36
tarehe 21\08\2013 saa 11:40 jioni katika Viwanja vya Kizwite ni jinsi baraza la Katiba la Chadema lilivyopokelewa mjini Sumbawanga na kuungwa mkono.
Ilikuwa Hoja kwa Hoja: na Hoja kwa Hoja kweli si mchezo. Unaiona Kazi nzuri sana kwa Msaada wa Mungu kupitia Chama cha Chadema na Makamanda wasiochoka watu wanapata darasa la kutosha. SI MCHEZO.
 
Napendekeza katiba ijayo iweke kikomo cha safari kwa viongozi wa kitaifa ili kuepuka hii hali ya viongozi wetu kujiamria safari ambazo hata kwenye bajeti kuu ya serikali zinasababisha ongezeko kubwa la pesa ambazo badala ya kupelekwa sehemu zingine zenye mahitaji muhimu zaidi kama afya, elimu, maji na kilimo
 
Nawaomba sana Chadema mchague mgombea makini sana wa ubunge hapa Kahama ikiwezekana hata Zitto Kabwe kwa kuwa alishawaahidi wana Kigoma kwamba hatagombea ubunge kwenye jimbo lake la Kigoma kaskazini na ninaomba sana wagombea wenu wote wa ubunge waanze kupitapita kwa wananchi hasa katika majimbo yanayoshikiliwa na CCM
 
Napendekeza kuwe na serikali ya majimbo ili hao viongozi wa majimbo wachaguliwe kwa kupigiwa kura na wananchi wajimbo husika
 
Back
Top Bottom