Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya (KCCB) wataka sheria ya uhalifu mtandaoni ipitiwe upya

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Kenya (KCCB) limeitaka serikali kufanya mapitio ya haraka ya marekebisho mapya ya Sheria ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Uhalifu wa Mtandaoni pamoja na Sheria ya Ardhi, likitahadharisha kwamba sheria hizo zimepitishwa kwa haraka bila mashauriano ya kutosha na zinaweza kuhatarisha uhuru wa wananchi, faragha, na haki ya ushiriki wa umma.

Akisoma tamko la maaskofu hao jijini Nairobi, Askofu Mkuu Philip Anyolo alisema mchakato wa kutunga na kupitisha sheria hizo haukuhusisha maoni ya wananchi ipasavyo, jambo linalozua hofu kuwa zinaweza kutumiwa vibaya na taasisi za serikali kuminya uhuru wa kujieleza na kuingilia faragha za watu.

“Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu namna marekebisho haya yalivyoandaliwa na kupitishwa kwa pupa. Ni muhimu yafanyiwe mapitio kabla hayajageuzwa kuwa nyenzo za kukandamiza uhuru,” alisema Askofu Anyolo.

Maaskofu wamesema kuwa baadhi ya vifungu vya Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni vinaweza kutumika kama silaha dhidi ya wakosoaji wa serikali, ama hata kuathiri taratibu za uchaguzi na matumizi ya teknolojia kwa uhuru.

Wameongeza kuwa malalamiko yaliyotolewa na wananchi kuhusu sheria hizo hayapaswi kubezwa, bali yazingatiwe kwa makini ili kuhakikisha yanatumika kwa haki na si ukandamizaji.

Marekebisho hayo, yaliyotiwa saini na Rais William Ruto tarehe 15 Oktoba 2025, yanawapa wapelelezi na mahakama mamlaka mapana ya kufuta au kuondoa maudhui mtandaoni yanayoonekana kukiuka sheria, ikiwemo uwezo wa kuzima au kufunga majukwaa ya kidijitali hata kabla ya taarifa kusambaa.

Screenshot 2025-11-13 181123.png
 
View attachment 3501298
Good
 
Back
Top Bottom