Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) limesema ili kuhakikisha wananchi wanaitumia kikamilifu haki yao ya kuweka viongozi wanaowataka ni lazima kuwe na mfumo wa wazi, wa haki na unaowajibika katika kusimamia zoezi la uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini, kwani madhara ya kukosekana kwa uchaguzi huru kunasababisha madhara makubwa.
Hayo yameelezwa na Rais TEC Askofu Wolfgang Pisa OFMCap alipokutana na wanahabari leo, Ijumaa Novemba 15.2024, jijini Dar es Salaam ambapo ameelza kuwa kwa muda mrefu hapa nchi watu wengi wamekuwa wakilalamikia michakato ya chaguzi mbalimbaliKuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 TEC imesema wananchi wameshuhudia jinsi zoezi zima la uandikishaji wa daftari la mkaazi lilivyoendeshwa hovyo ikiwa ni pamoja na kutokutolewa kwa vitambulisho vya wapiga kura ikifuatiwa na upendeleo wa wazi na usio wa kificho uliofanywa na watendaji/ wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua kwa wingi wagombea wa vyama vya upinzani nchini.
"Jambo hilo limetia doa kubwa sana Taifa letu na hata pale kiongozi mwenye dhamana (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI) alipoamua kutoa muda zaidi wa kukata rufaa bado haikuondoa doa hilo kwa uchaguzi wa mwaka huu, unaotarajiwa kufanyika Novemba 27.2024" -TEC.
Aidha, TEC imesisitiza kuwa uchaguzi pekee unaoheshimika ni ule unaoendeshwa kwa misingi ya uhuru, haki, uwazi ambao haupendelei upande wowote, uchaguzi unaoheshimu ukuu wa mamlaka ya wananchi juu ya viongozi wao wanaopatikana kwa njia ya kura.
Imetumia nafasi hiyo kutoa msisitizo kwa OR-TAMISEMI kuwa inapaswa kufahamu jukumu kubwa ililonalo la kuhakikisha zoezi zima la upigaji kura linafuata misingi ya demokrasia, na kwamba wale walioshinda kihalali ndio wanaopaswa kutangazwa kuwa viongozi halali wa maeneo husika.
"Tunasisitiza tena kwamba lazima wasimamie uchaguzi kwa misingi ya haki, wasipendelee chama chochote kwa namna yoyote ile, ukiukwaji wa matakwa ya wananchi hupelekea kuwa na viongozi wasio chaguo la watu, kiongozi anayepatikana kwa mabavu, kwa uongo, kwa kutangazwa bila kupata kura nyingi husababisha kutokuaminika na kukiukwa kwa misingi ya demokrasia" -TEC.
Pia, TEC imesema nguvu inapotumika kwenye misingi ya kidemokrasia na ulaghai katika michakato ya kutafuta viongozi ni lazima matokeo yake ionekane kiongozi huyo anatumia nguvu na ulaghai katika kuwaongoza watu katika kipindi chake chote cha uongozi jambo ambalo halikubaliki.