SI KWELI Baraza la mitihani (NECTA) limetangaza marekebisho ya vyeti kupitia shirika la BABU LEO LTD

SI KWELI Baraza la mitihani (NECTA) limetangaza marekebisho ya vyeti kupitia shirika la BABU LEO LTD

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
NECTA21JUL2025.jpg
 
Tunachokijua
Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa sheria mwaka 1973 ikiwa na jukumu la kusimamia mitihani ya taifa nchini Tanzania.

Kabla ya mwaka 1973, mitihani yote ya taifa ilikuwa ikisimamiwa na Kitengo cha Mitaala na Mitihani kilichokuwa chini ya Wizara ya Elimu baada ya Tanzania Bara kujiondoa kwenye Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki mwaka 1971.

Baada ya kuanzishwa kwa NECTA, jukumu hilo lilihamishiwa rasmi kwao, lakini masuala ya mitaala yaliendelea kushughulikiwa na Wizara ya Elimu pamoja na Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam hadi pale taasisi nyingine huru, yaani Taasisi ya Maendeleo ya Mitaala (ICD), ilipoanzishwa mwaka 1975, ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) mwaka 1993.

Tangazo kwa umma linalosambazwa kuhusu NECTA

Katika mtandao wa Facebook, ipo taaria inayosambazwa kuwa NECTA kwa kushirikiana na NACTE na TCU wametoa mkataba kwa shirika binafsi BABULEO LTD kufanya marekebisho ya majina kwenye vyeti vya shule ya msngi, sekondari, vyuo na NIDA.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani haijatolewa na Baraza la mitihani Tanzania (NECTA)

Aidha Aprili 02, 2025 NECTA ilikanusha taarifa ya Aprili 01, 2025 ambayo inafanana na taarifa hiyo ambayo inathibitika kuwa imeghushiwa na wapotoshaji wenye nia ovu kwani Baraza hilo halitumii mawasiliano binafsi kuwasilisha maombi hayo.

Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani hushughulikia maombi ya marekebisho ya majina ya watahiniwa yaliyokosewa kuandikwa katika mitihani ya Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu, ambapo ufuatao ni utaratibu unaotumika katika kuwasilisha maombi na kufanya marekebisho,


MASHARTI YA MAREKEBISHO YA MAJINA

(a) Maombi ya marekebisho yawasilishwe katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja baada ya matokeo ya mtihani kutolewa.

(b) Marekebisho ya jina ni lazima yawe na lengo la kufanya jina linalohitajika lifanane na jina lililotumika katika mtihani wa sifa (awali).

(c) Marekebisho yanayokusudia kuongeza jina jipya au kuondoa/kubadilisha jina (Mfano: Magina kuwa Madoba) hayaruhusiwi.

(d) Marekebisho yanayolenga kuboresha herufi zisizoathiri Matamshi ya jina linapotamkwa yanaweza kuombwa kufanyika.

(e) Msingi pekee wa marekebisho ya jina ni mtihani wa sifa (awali) na sio jina lililopo katika viapo vya mahakama, vyeti vya ndoa, ubatizo n.k.

(f) Cheti halisi chenye jina lilikosewa ni lazima kirudishwe NECTA kwa ajili ya mchakato wa marekebisho.


HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA MAOMBI

(a) Fungua tovuti (Website) ya NECTA (www.necta.go.tz)

(i) Chagua na ubonyeze huduma mtandao (E-services)
(ii) Ingiza Nambari ya simu ili kupata nambari ya uthibitisho (code number)
(iii) Ingiza nambari ya uthibitisho (Code) uliyopokea kwenye simu yako (tarakimu nne [04])
(iv) Ingiza barua pepe yako.

(b) Namna ya kufanya malipo kwa kutumia ‘Control Number’
(i) Ingiza majina ya mwombaji kama yalivyoandikwa kwenye cheti / Hati ya matokeo.
(ii) Ingiza tena nambari yako ya simu
(iii) Ingiza tena anwani yako ya barua pepe
(iv) Chagua huduma (Correction of Names)
(v) Tengeneza control number (Generate Bill).
(vi) Lipia ada ya marekebisho ya jina ya Tsh.35, 000/= (kwa cheti kimoja) kupitia benki au mitandao ya simu kwa kutumia ‘Control number’ uliyotengeneza.

(c) Baada ya kufanya malipo
(i) Bonyeza Marekebisho ya Majina (Correction of Names) na ufanye maombi (Apply/New)
(ii) Ingiza nambari ya simu ya mkononi na nambari ya malipo (Control Number).

(d) Jaza fomu ya maombi mtandao (Online Application Form) kisha Wasilisha ombi kwa kubofya ‘Submit’.

MAJIBU KWA MTEJA
Baada ya marekebisho kufanyika, Hati ya Matokeo (Results Slip) au cheti kipya chenye marekebisho kitatumwa kwa mkuu wa shule au kwa mtahiniwa (endapo si mwanafunzi).​
Back
Top Bottom