Baraza la mitihani Tz kutoa namba ya mtahiniwa badala ya jina ina maana gani?

Baraza la mitihani Tz kutoa namba ya mtahiniwa badala ya jina ina maana gani?

Nasema hivi kwa kuwa miaka yote ya nyuma ilituwezesha kujuana ktk uwezo wetu darasani na ilikuwa sio rahisi kumubeba mwanafunzi asiye jiweza darasani. Sasa kwa staili hii ya kuandika no pekee inaweza kuwafanya watumishi wa Baraza kuweka hata watoto/ndugu zao ambao hawakufaulu. Au hili swala limejitokeza kwa vile mwaka jana mtoto wa Rais alikuwa wa mwisho shule nzima kwa kupata dv 4. Ili tusijue aliye faulu alikuwa na uwezo gani darasani? Naomba nifafanuliwe ili nijue kuna siri gani iko hapo.

Siri ni kuwa wale wanaocheat kwenye mtihani huku wakiwa na vichwa vibovu hadi wanasahau namba zao za mitihani wakose matokeo
 
Kuweka majina inasaidia wale majuha kuvuna walicho panda. Na sidhani kama jibu lako ni sahihi kwani ukisoma unatakiwa usaidie jamii nzima sio familia yako tu. Kumbuka kodi ya watanzania ndo iliyo kusomesha. Naomba utafakari kabla.

sio kosa lako
 
Kuna wanafunzi wameamua kuficha no zao kwa wazazi/walezi ili wasiangalie majibu yao. Na kama ingelikuwa ni jina mzazi angefahamu kijana wake amepata Division gani bila kumuuliza. Hili swala limeleta usumbufu sana huku kwetu.
 
Wamefanya vizuri sana kwani kelele za UAMSHO zimepungua sana hawawezi kusema wameonewa
 
Nasema hivi kwa kuwa miaka yote ya nyuma ilituwezesha kujuana ktk uwezo wetu darasani na ilikuwa sio rahisi kumubeba mwanafunzi asiye jiweza darasani. Sasa kwa staili hii ya kuandika no pekee inaweza kuwafanya watumishi wa Baraza kuweka hata watoto/ndugu zao ambao hawakufaulu. Au hili swala limejitokeza kwa vile mwaka jana mtoto wa Rais alikuwa wa mwisho shule nzima kwa kupata dv 4. Ili tusijue aliye faulu alikuwa na uwezo gani darasani? Naomba nifafanuliwe ili nijue kuna siri gani iko hapo.
Huwezi angalia matokeo ya mtu bila idhini yake, nchi zngine kila mtahniwa anayafikia matokeo kwa namba yake maalua(pasword).
Hili ni jambo muafaka katika tasnia ya elimu na limekuwepo miaka mingi pia ni mfumo unaotumika na taasisi nyingi za kielimu nje na ndani ya nchi. Ila tu we kwa ugeni wako katika nyanja hii ndo maana unaona ajabu. Ndio maana watahiniwa hutumia namba badala ya majina kufanya mtihani ili kuwadhibiti watu kama wewe wenye tafsiri hafifu. Hakuna mtahiniwa anaye athirika na utaratibu huu zaidi ya kulinda heshima yake. Kama una ndugu mtahiniwa shart upate idhini yake kuangalia matokeo yake kwa kumwomba namba.
 
Kuna wanafunzi wameamua kuficha no zao kwa wazazi/walezi ili wasiangalie majibu yao. Na kama ingelikuwa ni jina mzazi angefahamu kijana wake amepata Division gani bila kumuuliza. Hili swala limeleta usumbufu sana huku kwetu.

yani mwanao ushindwe kumfanya akupe namba, basi we umeshindwa uzazi
 
issue ya mwanaasha unafikir ilikua ndogo oh!

Wamenikata stimu.......nilikuwa nataka kujua matokeo ya mtoto wa jirani yangu.....na alivyokuwa na nyodo.......
.ama kweli umbea umeniisha.....
 
Nasema hivi kwa kuwa miaka yote ya nyuma ilituwezesha kujuana ktk uwezo wetu darasani na ilikuwa sio rahisi kumubeba mwanafunzi asiye jiweza darasani. Sasa kwa staili hii ya kuandika no pekee inaweza kuwafanya watumishi wa Baraza kuweka hata watoto/ndugu zao ambao hawakufaulu. Au hili swala limejitokeza kwa vile mwaka jana mtoto wa Rais alikuwa wa mwisho shule nzima kwa kupata dv 4. Ili tusijue aliye faulu alikuwa na uwezo gani darasani? Naomba nifafanuliwe ili nijue kuna siri gani iko hapo.

Kwa maelezo yako inaashiria wewe ni miongoni wa watu wabwatukaji humu JF, hujui mambo kazi kufikia hitimisho tu, wewe aliekwambia utaratibu wa namba umeanza kwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2012 ni nani? Nenda kaangalie matokeo ya wahitimu wa mwaka 2008 ambayo yalitoka 2009.

Fanya kwanza tafiti ndio ufikie hitimisho.
 
Mie naona huo ni utaratibu mzuri sasa fikiria haya matokeo umefanya kama private lakini wewe ni kibosile mahali halafu umezungusha zero, hapo vipi?
 
Majina ndy ilikuwa nzuri
Najua siri ni wakati kufanya mtihani lkn ht matokeo ni Aibu.
 
Mie naona mpango huo uendelee na uwape chachu wazazi ya kufuatilia mambo ya shule ya watoto wao ikiwa ni pamoja na kujua namba zao za mitihani mapema
 
Nimetonywa kuwa wale wazee wa "Takbiir" hupatia data hapo na kuongoza maandamano.SO wameficha ili kila mtu abebe msalaba wake.
Si unajua watoto wa siku hzi hawapendi kujulikana kama wamefeli.
 
walijua ya kuwa matokeo siyo mazuri ndio maana waliamua kutoa namba za mtihani na wala siyo majina
 
Matokeo ya mtu yanamhusu yeye peke yake na hayakuhusu kama huna "haja ya kujua". Na kama una "haja ya kujua" unaweza kumuomba mwenyewe namba yake akakupatia.

Tamaduni zote zinazothamini faragha ya mtu binafsi zitaona habari hii ya kutoka kwenye majina kwenda kwenye namba ni ushindi kwa wapenda faragha.
 
Me mbona cjaona mnabishania nn maana ht km wametoa no tu mbona imejulikana mabaya 60% zero ss hamna tatizo ni stail 2!
 
Hoja nzuri wachangiaji ni dhaifu je mwenye usahihi atwambie wizara imetoa kauli gani kuhusu hilo nahisi kuna siri nzito
 
Back
Top Bottom