Baraza la sanaa(BASATA) lasitisha usajili wa Msanii Dudubaya

Baraza la sanaa(BASATA) lasitisha usajili wa Msanii Dudubaya

Tanzania bwana,sasa wanamfungia kafanya kosa gani?
Hakuna nchi hatari kwa kuishi kama nchi za kiafrika ndiyo maana likaitwa bara giza. Ukiwa kwenye bara giza ww jali mambo yako maana ukijifanya unajua sana watakuua, kukufunga au kukufanya chochote kile hata kama hakipo kwenye sheria. Wengi wametendewa vibaya na lugha lkn unakaa kimya tu kuangalia maisha yako.
NCHI ZA KIAFRIKA SIYO SALAMA KUISHI.
 
''Tunakufungulia dunia kuwa unacho taka", kachagua mwenyewe kuwa baya, mpuuzi...avune alichopanda.
 
.
Nimeona tamko, na ningependa kufanya comment mstari baada ya msitari kama ifutavyo:

Mosi, BASATA wanasema:
View attachment 1034718

Aya hii ni taarifa, na haina lolote la kujadili kwani mamlaka hayo yako ndani ya uwezo wa kisheria wa BASATA.

Pili, BASATA wanasema:

View attachment 1034719

Hapa kuna kuna tatizo. Kukamatwa na Jeshi la Polisi ni kutuhumiwa. Kutuhumiwa sio kuhukumuiwa. Katiba ya nchi inasema kila mtu anayo haki ya kuhesabiwa mwenye haki mpaka mahakama inapomtia hatiani. Dudubaya hajatiwa hatiani na mahakama. Kwa hiyo, uamuzi wa BASATA unaweza, na unapaswa kufanyika, baada ya hukumu ya mahakama na sio kabla yake. Kwa hiyo, aya hii inamaanisha kuwa BASATA wamefanya maamuzi yanayokiuka Katiba ya nchi.

Tatu, BASATA wanasema:

View attachment 1034720
Aya hii inaendeleza kosa lililofanyika aya ya hapo juu. Kwamba Dudubaya ni "raia mwema" au kinyume chake ni suala la kuamuliwa na mahakama na sio vingnevyo. BASATA walipaswa kusbiri maamuzi ya mahakama ili wachukue hatua hii. Lakini wameitangulia mahakama. Wamekosea.

Na nne, BASATA wanasema,

View attachment 1034721

Aya hii imekaa kiswahili kweli kweli. Kwamba kuna Watanzania wengi "waliojitokeza kukemea kitendo cha Msanii Dudubaya" kwa sababu wanaona "hakifai," haimaanishi kwamba mahakama imetoa hukumu ya kisheria. Kisheria tunasema "plausibility does not always imply validity." Kwa hiyo, BASATA wametumia sheria za mitaani kana kwamba ni sheria za kimahakama. Wamekosea.

Hivyo, naona kwamba, BASATA wanaendeleza utamaduni mpya wa baadhi ya vyombo vya serikali "kufanya kazi kwa mujibu wa matamko ya wakubwa" badala ya kuangalia sheria inasema nini. Utamaduni huu haukubaliki kwa Watanzania wanaojua na kuheshimu kanuni za utawala bora.

Kanuni moja ya utawala bora ni kanuni ya usawa mbele ya sheria.
Yaani, "the same law should apply to like persons in like circumstances."
BASATA wamezingatia kigezo hiki ? Hapana

Na bahati nzuri ni kwamba, Waziri wa Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe, ni Mwanasheria Nguli. Nimesoma PHD Thesis yake yote. Yuko safi kichwani. Pia ni mlokole mzuri. Wengi tuliona alivyousindikiza mwili wa hayati Samwel Sitta kwa mbwembwe tosha za machozi ya Kilokole. Tunataka imani yenye vibwagizo vya matendo.

Ama sivyo, tutahitimisha kwamba ulokole ule ulikuwa ni usanii, na usanii sio taji lenye heshima kwa mtu mwenye umri kama wa Dr. Harrison Mwakyemba.

Mama Amon.

View attachment 1035179
Asante Mama Amon barikiwa na Mungu wa mbinguni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo basata wanataka kutuaminisha kuwa mtu akikamatwa na jeshi la polisi na biashara yake inafutwa, pia wakumbuke kuwa kukamatwa sio kutiwa hatiani wangesubili kwanza lakini hawa jamaa wameandika kwa mihemko tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jam
Basata wanazingua tu. Kama wangekuwa serious na kazi sidhani kama huu mziki wa kusifia ngono na wanawake ungekuwepo maredioni mpaka sasahivi. Asiyeweza kuimba vitu vyenye mantiki na kuburudisha aache usanii nchini.

Sahivi tuna kizazi cha ajabu kupata kutokea katika sanaa ya mziki ikiwa sie tulipokea mziki kutoka kwa akina Msondo, DDC, TOT na wengineo ukaja kwa akina Rip Banza, Mwinjuma muumini Ally Choki ukiwa salama kabisa . Angalia kina Feruzi, Prof. Jay, Afande Sele, Juma Nature wote waliendeleza burudani huku wakiimba vitu vinavyogusa jamii na maisha kwa ujumla.

Sahizi ni upumbavu wa kusifia ngono kwa mafumbo tu, paka mate niteleze. Blah blah kibao. Kwanza mziki hauna vionjo asilia vya kibongo umekaa ki Nigeria sana makelele mengi. Hamna ujumbe mwishowe tunakuza vizazi vya malaya na mashoga tua sasahivi. 80% ya nyimbo inazungumzia nipe vya chumbani...aargh.

Kama nyie BASATA kweli kazi mnaiweza ondoeni upupu unaozagaa maredioni na kwenye TV. Bring back the 1998-2007 bongo flava back. Wekeni katiba inayolinda na kusimamia haki za msanii na mtayarishaji nyimbo. Inasikitisha sana wasio na vipaji leo wanatajirika tu ilihali waasisi wa bongo flava wapo na wanakufa na unga kwa kukoseshwa Airtime. Eti ni wasanii wa zamani...so Ridiculous. Fanyeni vitu vionekane kweli, sio kujihusisha na kesi za kitoto!
Jamaa umeongea kweli lkn wenye matimu watakuletea povu!
 
Back
Top Bottom