GE2025 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo wa TEREMSHA BUNDUKI wa Roma Mkatoliki

GE2025 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo wa TEREMSHA BUNDUKI wa Roma Mkatoliki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo mpya wa msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki, uliopewa jinala “Teremsha Bunduki”, ikiwa ni siku chache tangu ulipotoka rasmi.

Taarifa ya BASATA ya leo Oktoba 21, 2025, imesema wimbo huo umevunja kanuni za Baraza, na kwa hivyo umezuiliwa kutumika kwenye vyombo vya habari na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii hadi pale utakapofanyiwa marekebisho yanayokidhi masharti ya Baraza hilo.

Pia Sikiliza: Wimbo wa Roma Mkatoliki -Teremsha Bunduki 🎵🎶

Wimbo Wa maandamano ndio kwanza wameupa kiki
 
Hivi huwa mna maana gani kuandika habari ndani ya habari ya mtu mwingine? Kwanini usichangie maoni yako au kuanzisha thread nyingine ktk Uzi wako ili kuondoa unnecessary information ambazo zimeshaelezwa na mwenye Thread husika?
Hiyo comments ni independent thread mode wameiunganisha.

Ili kuondoa nyuzi nyingi zinazoongelea jambo moja
 
Ipo kwenye simu waje kufungia na huku, hawa jamaa wanaishi sijui wapo karne gani sijui mtihani
 
Hivi huwa mna maana gani kuandika habari ndani ya habari ya mtu mwingine? Kwanini usichangie maoni yako au kuanzisha thread nyingine ktk Uzi wako ili kuondoa unnecessary information ambazo zimeshaelezwa na mwenye Thread husika?
Ni kwa kuwa nchi hii imejaa machawa na uchawa wa mafisadi wanamtandao na majizi,hivyo mawazo ya hovyo na uonga ya kiachwa hatimaye utakuwa utamaduni wa taifa hili hivyo kunyooshana ni jambo barabaraaa!
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo mpya wa msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki, uliopewa jinala “Teremsha Bunduki”, ikiwa ni siku chache tangu ulipotoka rasmi.

Taarifa ya BASATA ya leo Oktoba 21, 2025, imesema wimbo huo umevunja kanuni za Baraza, na kwa hivyo umezuiliwa kutumika kwenye vyombo vya habari na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii hadi pale utakapofanyiwa marekebisho yanayokidhi masharti ya Baraza hilo.

Pia Sikiliza: Wimbo wa Roma Mkatoliki -Teremsha Bunduki 🎵🎶

Hawa mazafakaz wanasigina constitutional rights za watu. Where’s the freedom of speech?
 
Hivi huwa mna maana gani kuandika habari ndani ya habari ya mtu mwingine? Kwanini usichangie maoni yako au kuanzisha thread nyingine ktk Uzi wako ili kuondoa unnecessary information ambazo zimeshaelezwa na mwenye Thread husika?
Bora umesema maana huwa naona ni kero kweli.
 
Nyimbo za mashoga zinaachwa watoto wadogo mtaani wanaimba...
Nchi hii inawapa kipaumbele mashoga kuliko marijali
Wanataka wote muwe mashoga ili wawatawale vizuri, ndio maana wanasema hio 29 October hakuna wa kuandamana sababu wanajua wanaongoza mashoga wasioweza kufanya lolote, nchi imejaa bajaj na bodaboda kila seehemu na viongozi wanajisifia kwamba wanafanyaje?
 
Mimi binafsi mtazamo wangu uko tofauti kidogo.. hivi unaposema umeufungia wimbo na wakati umeshasambaa mitaani unakua una lengo la kuufungia au ku promote? Maana hata asiye uskia utautafuta Ili auskie

Kwa Nini hao basata wasiwe na mfumo kama wa TFDA kwamba kabla ya msanii yeyote hayatoa kazi yake katika jamii wakague kwanza ndipo apewe kibali?? Na iwekwe Sheria kwamba msanii haruhusiwi kutoa kazi yeyote bila kibali Toka BASATA nafkiri hii mbinu itasaidia sana kupunguza au kuokoa watoto wetu dhidi ya maudhui ya hovyo yanayoendelea mitandaoni
 
Back
Top Bottom