Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Dickson Samson Makwaya (Bambo)
Baraza la sanaa linashindwa vipi kumuita na kumuonya Bambo aache kuharibu lugha ya kiswahili kwa makusudi.
Huyu kijana nje ya kuharibu lugha yetu ya kiswahili sidhani kama ana kitu anachochekesha.
Ifike mahali sasa aonywe ikiwezekana afungiwe kabisa ,nakumbuka hata wimbo wa Sumalee (Hakunaga) ilibaki hati hati kufungiwa kwa kosa la kuharibu lugha .
Yeye kama msanii ni kioo cha jamii hivyo anatazamwa na wengi, sasa kama yeye anaanza kuharibu lugha inamaanisha wengi atawapoteza haswa kwa wale wageni wasiofahamu vyema lugha ya kiswahili na Wana nia ya kujifunza.