Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 17, kifungu cha 267 kifungu kidogo cha 1 kinasema kutakuwa na Baraza la Usalama la Taifa na wajumbe wafuatao:
a) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio
Mwenyekiti
B) Makamu wa kwanza wa Rais
C) Rais wa Zanzibar na Makamu wa pili wa Rais
D) Waziri Mkuu
Kifungu kidogo cha 2 :Mwenyekiti anaweza kumualika mtu yoyote kushiriki katika kikao cha baraza la usalama
Kifungu kidogo cha 3
Kinasema kutakua na Sekretarieti ya baraza la Usalama la Taifa itayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi
Majukumu ya baraza ni
Kuunganisha sera za ndani, sera za nje na za kijeshi kuhusiana na Usalama wa Taifa ili kuwezesha taasisi za kiulinzi
kushirikiana kikamilifu
B) Kupokea na kutathimini taarifa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Taifa na taasisi za serikali kuhusiana na usalama wa nchi
C. Kutekeleza majukumu mengine yoyote kama Rais atakavyoagiza.
My take:
Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama huingia kwa nafasi zao