Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika labadilisha mwelekeo wa bara la Afrika

Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika labadilisha mwelekeo wa bara la Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VCG111516245154.jpg


Jarida la The Economist toleo la Mei 13, 2000, lilichapisha makala inayochora picha mbaya ya bara la Afrika, kuwa ni bara lisilo na matumaini, likiorodhesha mambo mbalimbali kama vile kukosekana kwa usalama, magonjwa, hali mbaya ya miundombinu na hata uchumi dhaifu. Ni mwaka huo huo, wakati nchi nyingi za magharibi zikiwa na maoni kama hayo, ndipo Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) lilipoianzishwa, na sura ya Afrika kwa nchi za magharibi imeanza kubadilika.



Katika muda wa karibu miaka 26, ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika umepitia hatua nyingi na kuwa na mabadiliko makubwa. Mwaka 2000 wakati FOCAC inaanzishwa, jumla ya thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilikuwa ni Dola za Kimarekani Bilioni 13.9, na mwaka 2025 thamani hiyo imefikia dola bilioni 300, likiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 20 na kwa kiwango cha wastani cha ukuaji wa asilimia 14.2 kila mwaka.



Mtazamo hasi kwenye makala ya jarida la The Economist kuhusu Afrika mwaka 2000, ulikuwa ni maoni ya nchi za magharibi kwenye maandishi, lakini mtazamo wa China kuhusu bara la Afrika katika wakati huo huo, ulikuwa chanya na kuliona bara la Afrika kuwa ni bara lenye fursa na matumaini, na FOCAC ni ushahidi wa kivitendo kuhusu maoni ya China kuhusu Afrika kwa mwaka 2000.



Katika kipindi hicho cha zaidi ya miaka 25 cha ushirikiano wa karibu kati ya China na nchi za Afrika, mabadiliko makubwa yametokea, na kikubwa kinachoonekana kwenye nchi za magharibi ni malalamiko kuhusu kuongeza kwa nguvu ya ushawishi ya China barani Afrika, ambayo wanaona ni hatari ya kupoteza himaya yao ya muda mrefu.



Sambamba na FOCAC, ushirikiano kati ya China na Afrika chini ya utaratibu wa pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) umekuwa ukilenga moja kwa moja changamoto zinazotatiza maendeleo ya uchumi ya nchi moja moja ya Afrika, na hata bara zima kwa ujumla. Hili linaonekana zaidi kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, mawasiliano na hata kuendeleza viwanda, mambo yanayoendana na Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063.



Kutokana na matokeo ya ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika, na hasa maendeleo yanayoendelea kupatikana kwenye ujenzi wa miundombinu na maendeleo ya viwanda, mtazamo wa nchi za magharibi kuhusu bara la Afrika umeanza kuwa tofauti, na baadhi wanaona uwezekano wa kuibuka kwa bara la Afrika.



Jarida la The Economist toleo la Januari 7, 2025 lilichapisha makala ikisema, “Bara liko kwenye njia panda ya maendeleo, changamoto, na fursa”. Makala hiyo imetaja kuwa kwa sasa bara la Afrika lipo katika wakati muhimu kabisa kihistoria, likiwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na mabadiliko na maendeleo.



Tukifuatilia kwa undani, mbali na juhudi za ndani za serikali za nchi za Afrika kuweka sera na mazingira mazuri yanayochangia kufunguliwa kwa fursa za ukuaji wa Afrika, ni ukweli usiofichika kuwa mchango wa China umekuwa ni msukumo mkubwa kwa maendeleo ya bara la Afrika. Mambo mengi ambayo ilikuwa ni ndoto kwa nchi za Afrika kutekeleza, kama vile ujenzi wa reli, viwanja vya ndege, bandari na hata barabara za mwendo kasi, na hata viwanda sasa yanaonekana katika nchi mbalimbali za Afrika, na China inaendelea kuzipa moyo nchi za Afrika kuwa zinaweza kufanikisha mengi zaidi.
 
Back
Top Bottom