DOKEZO Baraza la Uuguzi na Ukunga halijatoa matokeo ya Uandikishaji na Leseni zaidi ya miezi miwili

DOKEZO Baraza la Uuguzi na Ukunga halijatoa matokeo ya Uandikishaji na Leseni zaidi ya miezi miwili

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Baraza Liliendesha mthiani ya uandikishaji na leseni ya UUGUZI NA UKUNGA kwa NGAZI ya Cheti, Diploma na Degree ya kwanza tarehe 23 august/2024 lakini mpaka muda huu ni zaidi ya MIEZI miwili na wiki moja.

Baraza halijatoa matokeo na taarifa lini yatakuwa tayari au kubainisha ni nini changamoto iliyo chelewesha kwa Umma, hata hivyo Baraza limetoa tarifa rasmi ya kufungua dirisha la maombi ya mthiani mwingine kabla yakutoa matokeo ya mthiani huo.

Hali hii kiukweli inatutia wasiwasi juu ya utendaji kazi wa hili Baraza hili maana mwaka jana pia wamewahi futa matokeo ya mthiani ulio fanyika September 2023, kwa madai ya kuvuja, jambo ambalo walitumia miezi zaidi ya mi NNE kutoa taarifa hiyo.

Hata hivyo, imezoeleka mthiani kusahishwa na kukamilisha matokeo ndani ya siku ZISIZO fika MIEZI 2

Tunaomba serikali iingilie kati kupitia wizara ya afya.

Baraza litoa matokeo ili kama mtu hajapata alama stahiki za kupata lessen awe na sifa ya kuomba nafasi nyingine kama itakavyo Sheria na taaratibu zao. Maana kwa sasa hatuna sifa za kufanya mthiani ya December na mda unazidi kwenda.
 
Back
Top Bottom