Baada ya hivi karibuni matokeo ya mtihani wa leseni ya wafamasia kuzua mijadala mingi miongoni mwa wadau,baraza la famasi limeamua kufanya siri hata muhutasari wa matokeo hayo kwa hofu ya kujadiliwa,na jamii kwa jinsi yalivyo mabaya.
Sio hivyo tu,bali pia kwa ajili ya kuficha uozo unaoendelea katika kutoa leseni kwa ndugu jamaa na marafiki wa vigogo,ambao wengine hata mtihani hawafanyi kabisa.
Vile vile kuna biashara haram ya kulipisha pesa kwa wanaopata supp ambapo hutozwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na baraza kama la wauguzi.
Baraza hili linapoamua kufanya mambo yake kwa kificho ni kujaribu kuweka mianya ya rushwa na upendeleo kwa baadhi ya watu.
Baraza hili limefanywa kama chombo cha mtu binafsi na kwa hiyo msajili na timu yake wanaamua tu kama vile wanaongoza kampuni binafsi.
Serikali inapaswa kuweka chombo cha kudhibiti ubora katika hizi bodi ambazo zinaonekana hazina wasimamizi na wao hata ada mbali mbali hujipangia tu bila kujali maslahi ya wanachama wao.
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app