Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
"Leo (Jumatatu, Septemba 30.2024) Bawacha tumewaita (wanahabari) hapa (makao makuu ya zamani ya CHADEMA) kufanya tukio la kuonyesha hasira zetu dhidi ya Rais (Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), mwaka jana tarehe 3/8/2023 BAWACHA tulimualika kwenye kongamano la siku ya mwanamke Duniani, kwa upendo kabisa tukitegemea mabadiliko chanya kwenye Taifa letu, tulimpa changamoto tisa za wanawake na Watanzania kama vile uboresha huduma za afya hususani kwa kina mama na watoto, kupunguza kodi na tozo kwa wafanyabiashara wadogo ambao wengi wao ni wanawake na vijana, kupunguza gharama za maisha, kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wetu, na kurejesha mchakato wa Katiba mpya" -BAWACHA
"Changamo nyingine ni pamoja na kutatua kero ya maji hasa maeneo ya vijijini maana waathirika wakubwa ni kinana, kuwaondoa 'COVID 19' (Wabunge 19 wa Viti maalum walioko Bungeni wakiongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa BAWACHA Halima Mdee ambao wanatajwa kuwa hapo kwa baraka za CHADEMA) Bungeni, kuboresha mfumo wa elimu kwa watoto wetu, kurejea sheria kandamizi kwa wanawake na watoto hasa sheria ya ndoa, katika kongamano hilo tulimpa zawadi ya tuzo ya demokrasia na maridhiano na yeye akatupa zawadi ya vitenge" -BAWACHA
"Hata hivyo hakuna jambo hata moja ambalo Rais Samia amelifanyia kazi, hii ni dharau kwa BAWACHA na dharau kwa wanawake wapenda haki na maendeleo ya Taifa lao, hivyo basi leo tumewaita hapa ili kuonyesha hasira zetu dhidi ya Rais Samia kwa kukokuchukua hatua yoyote dhidi ya mauaji, utekaji na kupotea kwa vijana wetu, BAWACHA Kanda ya Pwani leo tutaenda kuchoma vitenge alivyotupa Rais kama zawadi siku ya mwanamke Duniani mwaka jana" -BAWACHA
Ni sehemu ya yale aliyozungumza Mwenezi wa BAWACHA Taifa Aisha Machano mbele ya wanahabari leo, Jumatatu Septemba 30.2024
Pia soma
- BAWACHA watangaza kuchoma vitenge walivyopewa kama zawadi na Rais Samia mwaka jana