Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BARAZA LA WAZEE WA TANU 1954 - 1963
Mara tu baada ya kuundwa kwa TANU mwaka wa 1954 Baraza la Wazee wa TANU liliundwa katika makao makuu, New Stret Dar es Salaam.
Baraza hili lilikuwa na takriban wajumbe 170.
Ilikuwa ni kamati ya wazee wa mji wa Dar es Salaam na kitu kimoja ni kuwa wajumbe wake wote walikuwa Waislam.
Sheikh Suleiman Takadir ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Wazee wa TANU.
Kamati kama hii iliundwa Tabora mwaka wa 1956, Mwenyekiti wake akiwa Mzee Fundi Muhindi mwanasiasa mkongwe, muasisi wa African Association Tabora mwaka wa 1945 na muasisi wa TANU mwaka wa 1954.
Kwa nini kamati hizi zilikuwa na wajumbe Waislam watupu?
Kleist Sykes katika mswada wake wa kitabu alioandika kabla ya kufariki mwaka wa 1949 anasema kuwa waasisi wa African Association (AA) mwaka wa 1929 wengi wao walikuwa Waislam na sababu ni kuwa Wakristo walikuwa wakikatazwa na Kanisa kujiingiza katika siasa.
Katika hali kama hii hata mwakilishi wa Waafrika alikuwa Father Gibbons kutoka MInaki Misheni hii yote ilikuwa katika juhudi ya kuwaweka Waafrika chini na kuwakaia kichwani.
Kleist alipoanza harakati za kuasisi AA waliojotokeza kumuunga mkono walikuwa jamaa zake wanamji kama yeye.
Hivi ndivyo ikaja kuwa mjini Dar es Salaam waasisi wa AA wengi wao wakawa jamaa zake wanamji kama yeye wanaojuana kwa miaka kama Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, na wakajaungwa mkono na Cecil Matola Raikes Kusi, na Rawson Watts.
Hawa watatu wa mwisho walikuwa wageni mjini Dar es Salaam.
Hapa ndipo tunaweza kuanza kuangalia asili ya Baraza la Wazee wa Dar es Salaam ndani ya AA kisha TAA pale AA ilipobadili jina na kuitwa TAA.
Lakini ili kufika hapo inabidi uangalie taasisi nyingine ambayo iliundwa ndani ya AA mwaka wa 1933 na tujue sababu za kuundwa kwake.
Mwaka wa 1933 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa AA Cecil Matola nafasi yake ikajazwa na Mzee bin Sudi.
Ikawa baadhi ya mambo ya Waislam kwenda serikalini yanapitishwa kupitia AA hili likaonekana ni tatizo kwani AA ilundwa kwa nia ya kuwaunganisha Waafrika wote wa Tanganyika bila ya kujali dini wala kabila zao.
Ndipo mwaka wa 1933 ikaundwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Mzee bin Sudi akiwa President na Mzee bin Sudi Secretary nafasi ambao pia walikuwa wamezishikilia katika AA.
Hii ndiyo ikawa sababu kubwa sana kwa siasa za za mji wa Dar es Salaam naharakati za kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika zikawa zimetawaliwa na Waislam.
Hii ndiyo sababu Baraza la Wazee wa TANU lilipokuja kuundwa mwaka wa 1954 wajumbe wa baraza zima karibu 170 wakajikuta watu wa imani moja.
Hawa ndiyo waliojulikana kama Baraza la Wazee wa TANU.
Baraza hili lilivunjwa mwaka wa 1963 kwa kutuhumiwa kuwa, ‘’linachanganya dini na siasa.’’
Wakati linavunjwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU alikuwa Mzee Iddi Tulio.
Picha ya kwanza ni Baraza la Wazee wa TANU na ya pili ni Wazee wa Dar es Salaam na watu maarufu ilipigwa Shambani wa Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo mwaka wa 1956.