BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mkurugenzi Mtendaji wa Simba SC, Barbara Gonzalez ametangazwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Vilabu vya CAF na Usimamizi wa Mfumo wa Leseni za Klabu
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameteuliwa kuwa mjumbe kwenye Kamati mbili.
Kamati hizo ni ya Maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) pamoja na Kamati ya Fedha.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani ameteuliwa kwenye Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer).
Mjumbe katika Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya CAF kutoka Tanzania ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha.