Barca inatupa Somo la Uongozi Bora

Barca inatupa Somo la Uongozi Bora

babacollins

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
901
Reaction score
212
Miezi kadhaa iliyopita ilionekana kama mwisho wa enzi kwa Barcelona. Awamu za uongozi wa Sandro Rossel na Bartomeu ziliiacha Barca katika hali mbaya ndani na nje ya uwanja. Kurejea katika uongozi kwa Laporta kumebadilisha kabisa uelekeo wa mambo.

Laporta huyuhuyu ndiye aliyeiacha Barca ikiwa na mafanikio tele ndani na nje ya uwanja. Tayari kwa sasa Laporta amefanikiwa kumpata kiongozi anaeonesha dakika njema ndani ya uwanja, Xavi, na nje ya uwanja tayari Barca inavutia tena uwekezaji na kufanya usajili wenye kuzingatia hali ya kiuchumi kwa sasa na wenye tija kiwanjani.

Kuna jambo kubwa sana la kujifunza kwa klabu zetu, mara nyingi katika mafanikio hata katika soka "siasa safi" na "watu" vipo changamoto kubwa huwa ni "Uongozi Bora".

Mchezaji kiongozi.
 
Xavi bado anahitaji mda kuaminika kwamba Barcelona wamerudi kwenye ubora wao kwani kuna makocha walianza vizuri zaidi yake mechi za mwanzoni ila baadae wakaja kuharibu vibaya sana na kufukuzwa kwenye team.
Ni hao, ila sio kwa mwanakatalunya huyu Xavi.

Unaiona kabisa Barca ilivyo ya ushindani.

Ngoja season mpya ianze akiwa ameweka mawe yake sawa.

Ile barca yao akina xavi,iniesta,messi kampa kampa tena ndo inarudi.
 
Timu kubwa na iliyopata mfanikio makubwa kisha ikapotea kwa muda mrefu ni Ac Milan. Yaani viongozi wake wake wamemchemsha mno
Mwekezeji akiwa mchina au mmarekani kwenye soka usitegemee kusikia klabu inachukua mataji mara kwa mara. Klabu itachukua mataji once in a blue moon. Wao wanapata faida zingine mashabiki mtapambana kivyenu.
 
Huu ni upepo tu. Hicho unachokisema kitakuja kuonekana baada ya mwaka mmoja kama kweli ni uongozi imara au ilikua mvua za rasharasha.

Tuwape muda ni mapema sana kuamini hayo kwa sasa.
 
Xavi amrudishe Messi wetu timu ikamilike...japo iko vizuri for now, lakini kipimo kizuri zaidi ni UEFA....Madrid aliemchapa chelsea goli 3, sisi tumeshampiga goli 4.

Forca Barcaaa
 
msimu wamo

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Hamna kitu hawa, ukizingatia na soka la Italy limeshuka kiwango sio kama zamani ukiona timu inazowakilisha UEFA kutoka Italy ni timu haswa ambazo huwezi kukosa robo au nusu timu moja au mbili. Lakini siku hizi timu zote za Italy ni wepesi sana kwenye champions league. Ac Milan msimu wanachezea shilingi chooni, wamepata pochi mara ya kwanza ya kuongoza ligi kwa gap kubwa huku Napoli na Intermilan wakipoteana lakini cha ajabu kakutwa na kuja kupitwa na Intermilan. Mzunguko wa pili tena anapata tena pochi la kuongoza ligi kwa gap ya point 4 dhidi ya Inter huku ikisalia michezo 8 lakini wanakuja kutoa sare mfululizo na vitimu vidogo.
 
Huyo XAVI anashinda kibahati tu kuna mechi kama 5 hv ndyo alicheza mpira ila nyingine ungaunga
IMG-20220415-WA0010.jpg

Sent from my SM-G935T using JamiiForums mobile app
 
Hamna kitu hawa, ukizingatia na soka la Italy limeshuka kiwango sio kama zamani ukiona timu inazowakilisha UEFA kutoka Italy ni timu haswa ambazo huwezi kukosa robo au nusu timu moja au mbili. Lakini siku hizi timu zote za Italy ni wepesi sana kwenye champions league. Ac Milan msimu wanachezea shilingi chooni, wamepata pochi mara ya kwanza ya kuongoza ligi kwa gap kubwa huku Napoli na Intermilan wakipoteana lakini cha ajabu kakutwa na kuja kupitwa na Intermilan. Mzunguko wa pili tena anapata tena pochi la kuongoza ligi kwa gap ya point 4 dhidi ya Inter huku ikisalia michezo 8 lakini wanakuja kutoa sare mfululizo na vitimu vidogo.

Inter sio timu ndogo, refer inter ya akina Diego milito, zanetti na cambiasso ilikua balaa
 
Inter sio timu ndogo, refer inter ya akina Diego milito, zanetti na cambiasso ilikua balaa
Ndio maaana nikasema timu za Italy zilikuwa ni moto tofauti na sasa soka la Italy limeshuka. Hapo ukizungumzia Inter ya diego milito huku unakutana na Roma ya akina Francisco Toti. Huku kuna Ac milan ya akina Pirlo.
 
Pale kulikuwa na mocha , na sio timu
Naijua Inter sio kikosi wala kocha ilikuwa ni nyota yao kwa mwaka huo, Group stages wakiwa na Rubin Kazan, Dinamo Kiev hawakufurahisha kbsa na mwaka ambao Morinho alisemwa sana ila Bahati ilikuwa yao, na alikuwa na wachezaji mature wenye uzoefu waliopita vilabu bora na wenye njaa na wanaotii maelekezo, wenye bidii ukiongeza na bahati walibeba. Kwanzia kipa Cesor, Maicon, Zaneth, Lucio, uende Mbele Etoo, Milito, katikati Tiago Mota nguvu, fujo, maarifa, utundu, game concentration, marking system, aerial ball, hakika mwaka wa bahati iliopangwa na Mungu, Barcelona, na Bayern zote zilikuwa Kali
 
Back
Top Bottom