Barcelona tunakwama wapi?!

Barcelona tunakwama wapi?!

Shooter Again

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
5,603
Reaction score
9,263
Hii ni moja ya timu yangu pendwa sana ila nashangaa Sasa hivi sijui ndio pesa hamna aisee yaani huyu mtoto Nico Williams anatutoa jasho aisee haya mateso ya hii klabu yangu kutoka moyoni yataisha lini? Mahasimu wetu wanajaza watu tu kama hawajachukua UEFA mwaka jana sisi hata huyu Nico Williams mtoto anaitaka Barcelona ila bado tunaongea sana wiki ya tatu hii.

Mwenye kujua tatizo la Barca lipo wapi naomba atujuze maana naona wanasajili makinda tu wakati sisi tunaitaka UEFA muda mrefu hatujaishika

Inauma sana aisee yaani sisi wa kusajili vifaranga tupu! FORCA BARCA
 
Kumbe na BONYOKWA culers wapo. Eti barca tunakwama wapi?????
Papa PEREZ nahisi ndo anawahujumu kuna double agents wa madridsta mtakuwa nao kama directors wenu. Kiasi kwamba kila mbinu safi mbinu chafu zinawekwa wazi.
 
Bora wachukue damuchanga na kikubwa zaidi wasifikirie VIKOMBE mapemaa misimu mitatu ya MWANZO .
 
Sababu pekee Arsenal hatujamchukua Nico na Zubimendi ni kwakua wanasema wanataka kwenda Barcelona. Means mchezaji angekua hana mapenzi na timu angekua kanyakuliwa kwingine
 
Kila sajili mnatia huruma naona viongoz wenu n mafisadi haiwezekani kila mwaka hamna ela
 
Jibu unalo mkuu, Barca tuna hali mbaya sana kiuchumi skuhizi. Wachezaji kama Gundogan, Felix na Lewa unaona kabisa walikuja kwa mapenzi yao na Barca. Lakn tukiambiwa mchezaji anauzwa Euro 50M tunaanza kutia huruma, Ndomaana tunakimbilia Academy yetu coz NO fucki g way. Baadhi ya watu wanadai tulianza kutumba baada ya kumuuza Neymar na kushindwa kupata replacement yake. Maana tukaanza kununua Expensive Flops kina Dembele Raphinha n.k
 
Sababu pekee Arsenal hatujamchukua Nico na Zubimendi ni kwakua wanasema wanataka kwenda Barcelona. Means mchezaji angekua hana mapenzi na timu angekua kanyakuliwa kwingine
Yaan Barcelona saiz tunapata mchezaji mzuri kwa mapenzi yake sio pesa tena. The same na kwa Gundogan, Joan felix na Lewandosk
 
Jibu unalo mkuu, Barca tuna hali mbaya sana kiuchumi skuhizi. Wachezaji kama Gundogan, Felix na Lewa unaona kabisa walikuja kwa mapenzi yao na Barca. Lakn tukiambiwa mchezaji anauzwa Euro 50M tunaanza kutia huruma, Ndomaana tunakimbilia Academy yetu coz NO fucki g way. Baadhi ya watu wanadai tulianza kutumba baada ya kumuuza Neymar na kushindwa kupata replacement yake. Maana tukaanza kununua Expensive Flops kina Dembele Raphinha n.k
Inauma sana aisee yaani hata kesho yetu hatuioni
 
Tatizo ni pesa mkuu inabidi kubalance kile unachoingiza na unachotumia viwiane ndio maana utaona wanahangaika katika sajili zao, na kuna kipindi baadhi ya wachezaji walilazimika kupunguza mishahara ili kubalance matumizi.
 
Sema tutaanza kuwaka mda si mrefu, yajayo yanafurahisha. Lakn ndohvo ni project ya mda mrefu sio sasa.
Sizani maana kama ndio mchezo wenyewe huu Kila msimu kupandisha watoto tupu aisee ni hatari maana hata hao watoto wengine nao lazima watakua hamna kitu mbeleni
 
Yaan Barcelona saiz tunapata mchezaji mzuri kwa mapenzi yake sio pesa tena. The same na kwa Gundogan, Joan felix na Lewandosk
Yeah, mna historia nzuri kidunia. Manunuzi ya wakina Coutinho, Dembele ili kutaka kwenda msuli kwa msuli na Madrid, mshahara wa kumtuliza Messi na ufisadi wa Rais aliyepita yamechangia kiuchumi kushuka.
 
Back
Top Bottom