Barcelona yafuta ‘Uteja’ kwa Real Madrid baada ya miaka 88

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Ushindi wa goli 1-0 wa Barcelona dhidi ya Real Madrid ukiwa ni ushindi wa pili ndani ya siku 3, unaifanya Barcelona kuwa timu ya kwanza katika Historia ya Ligi Kuu nchi Uhispania kushinda mechi nne mfululizo katika dimba la Santiago Bernabeu



Kutokana na goli pekee lililofunga na Kiungo Ivan Rakitic, Barcelona sasa inaendelea kuongoza ligi ikiwa na alama 60, alama 10 zaidi ya Atletico Madrid iliyo nafasi ya pili na alama 12 dhidi ya Real Madrid iliyo nafasi ya tatu

Ushindi huo unaifanya Barcelona kuongoza kuifunga Real Madrid kwa mara ya kwanza kwa miaka 88 katika michezo yote waliyocheza ambapo sasa imeshinda michezo 96 huku Madrid ikishinda michezo 95



Aidha, Kocha wa Madrid, Santiago Solari anakuwa Kocha wa kwanza kuinoa klabu hiyo na kushindwa kushinda katika michezo yake mitatu ya mwanzo dhidi ya Barcelona(L2 D1) tangu Leo Beenhakker aliposhindwa naye mwaka 1987(D2 L2)

 
Miaka 88 au 87?!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiachana na hiyo Baloteli aliwahi sema kuwa "Barcelona ndo club pekee ambayo ina viwanja viwili,camp nou kwa ajiri ya mazoezi na Santiago bernabeu kwa ajiri ya machi"
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…