Bariadi: Meya aeleza kwanini Stendi ya Mizigo eneo la Kidulya haikusanyi mapato tarajiwa

Bariadi: Meya aeleza kwanini Stendi ya Mizigo eneo la Kidulya haikusanyi mapato tarajiwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mstahiki Meya wa Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, Elias Masanja anaaelezea kinachoendelea juu ya mradi huo:

“Waziri Mkuu alikuja hapa akatoa tamko kuhusu maboresho ya Stendi hiyo ya mizigo, kwanza sehemu ya kuegesha magari haijawa na miundombinu mizuri, pia hakuna ghala la kuhifadhia mizigo, ikitokea mvua ikanyesha kama ni mizigo wa kuharibika utaharibika.

“Ujenzi wa Stendi ulikamilika Mwaka 2021, kazi zinafanyika lakini si kwa kiwango ambacho kinatakiwa kufanyika. Hasara ipo kwa kuwa matarajio hayajawa kama ilivyotarajiwa, hatujakidhi malengo ambayo tulijiwekea.

“Mkandarasi alijenga kama alivyotakiwa kwa kuwa mkataba wake haukuwa na vipengele vya kuongeza hivyo vitu ambavyo vinatakiwa kuogezwa.

“Kwa sasa mipango ya Mamlaka ya Mji ni kuwa tunaendelea kujipanga kwa kukusanya nguvu kabla ya kuanza kuitanua stendi kwa kuwa pia bado hatujapiga hesabu ya kiasi ambacho kinahitajika ili kukamilisha upanuzi na maboresho mengine.”

Bariadi.png

Pia soma: Stendi ya Mizigo Bariadi ya Tsh. Bilioni moja, inakusanya Tsh 0 Mwezi mzima | JamiiForums
 
Back
Top Bottom