Mara kwa mara watu wanachanganya sana haya mambo kwa sababu wengi wanaongea vitu kwavile walisikia mahali na wala hawana utaalamu wa jambo lenyewe! Katika hili, wengi sana utawasikia fulani sio mwanamuziki bali ni muimbaji! Kwa mtaalamu wa muziki akishakusikia unatoa hiyo hoja moja kwa moja anafaamu kwamba taaluma ya muziki hauifahamu!
Jambo la kwanza watu wanalotakiwa kulifahamu ni kwamba mwanamuziki anatokana na muziki! Kutokana na hilo, mtu anaye-perform muziki ndie anaitwa mwanamuziki! Ukirudi kwenye muziki wenyewe, pia unagawanywa katika makundi mawili makuu, vocalists yaani waimbaji na instrumentalists ambao ni wacheza ala za muziki! Ukitaka kusema mwimbaji sio mwanamuziki ni kwamba unataka kusema mpiga ala peke yake ndie mwanamuziki wakati hata tafsiri rasmi ya muziki ni kwamba "ni sauti/vocal au ala au mchanganyiko wa vyote kwa pamoja..." Kwahiyo hata mtu anayefanya akapela peke yake, kwa kuzingatia tafsiri ya muziki nae ni mwanamuziki na mwanamuziki wala sio kutembea na gitaa!
Aidha, huyu muimbaji hata kama hafahamu kupiga ala bado katika uimbaji wake analazimika kufuata ala za muziki kama ambavyo wakati mwingine mpiga/waiga ala za muziki (w)anapolazimika kutengeneza ala kulingana na uimbaji wa vocalist na ndio maana hata muimbaji akienda studio na hana uzoefu, kitu cha kwanza atakachoambiwa aimbe akapela ili mtengeneza beats afahamu ni beat za aina gani anaweza kwenda nazo! Ni kama ambavyo mpiga tumba, guitar, saxophone, violin, keyboard na kadhalika anapolazimika kubaki kwenye kifaa chake (eneo moja la muziki as instrumentalist) ndivyo muimbaji anapolazimika kubaki kwenye eneo lingine la muziki as vocalist!
Hoja ya Barnaba angekuwa ameongea kitaalamu angesema Diamond sio profession musician na kimsingi, alichokisema Barnaba kinamaanisha hivyo kwamba Diamond sio professional musician kwa sababu kutokujua kuimba sio kigezo cha kutokuwa mwanamuziki! Profession musician ni yule ambae amesomea muziki, anafahamu staff, notes na clefs kwenye muziki na maana na pia application zake! Hizi staffs, clefs na notes nazo zimegawanyika hadi unachanganyikiwa! Na katika hili, I doubt kama kuna mwana bongo flavor tunayeweza kumuita professional musician... katika hili ni lazima uende music school!
Tofauti ya Barnaba na wamamuziki wengine (including Diamond) ni kwamba, tukichukua pande mbili za muziki, kwamba ni uimbaji na uchezaji ala, Barnaba ni mwimbaji na vile vile ana "idea" na baadhi ya ala za muziki wakati wengine wengi ni waimbaji peke yake!