Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Masikini Barnaba! Bora ungebaki na hili jambo moyoni tu maana wenzio huku tuna maadui wengi sana kisa kusema ukweli kua Diamond sio mwanamuziki na hajui kuimba!
Hahaha, ni kweli mkuu. Ila usichukie, vumilia tu. Ndio Seleburiti wetu namba moja, hakuna jinsi!
haya makasheshe na wanawake yatampoteza dogo, badala ya kuwaza muziki ye anawaza kushindana na watalaka wake na scandal zao, mara bifu na alikiba, pia naskia ana nyodo sana now days hasa katika malipo ya show zake, naliona anguko lake
Nimesoma comment za wengi... karibu wote hawafahamu mwanamuziki hasa ni nani na muziki hasa ni nini! Hata Barnaba mwenyewe anachanganya kati ya professional musician na ordinary musician na hata maelezo yake yanaelezea unprofessional and professional musician. Na katika muziki, kutokujua kuimba wala sio kigezo cha kutokuwa mwanamuziki na hata kama una sauti mzuri kuliko watu wote duniani na unaimba vizuri kuliko wote duniani bado hicho peke yake hakiwezi kuwa kigezo cha kuwa professional musician or professional singer! Watu hawajui kwamba hata akapela peke yake ni muziki!!Kama sio mwanamziki ni mwana nani? Barnaba hajui aina za muziki zilizoko duniani ndio maana kasema hivyo, kuna siku atasema hata Saida karoli si mwanamziki kwa kuwa kakulia shamba.
Kuna mziki wa kufundishwa kidigitari,
Kuna mziki wa mapokeo yaani umejikita kwenye jamii husika bila kuusisha vifaa vya technologia ya kizungu. hivyo basi huenda barnaba hajui mziki kwani analazimika kutumia vyombo zaidi vya kumsaidia kuimba.
usiogope najua maisha magumu ndo tatizo lako
Mimi bado S ijaelewa mwanamuziki ni yule anayejua kuimba kwa noten if my spelling is correct au yule mwenye sauti Nzuri hata kama ni cabbo snoppy yule chizi wa Angola.?
Haya makasheshe na wanawake yatampoteza dogo, badala ya kuwaza muziki ye anawaza kushindana na watalaka wake na scandal zao, mara bifu na alikiba, pia naskia ana nyodo sana now days hasa katika malipo ya show zake, naliona anguko lake
Bila kumtaja Diamond wanajua interview itaishia kwenye matundu ya masikio ya watu....
Chibu oyeeeeeeeeee wapelekesheeeeeeeeeeeeee
Lazima huyu anatumia Chibu keshokutwa tutasikia anatoa nyimbo mpya
Bila shaka unafahamu mwanamuziki anatokana na muziki? SWALI: MUZIKI ni nini? Kutokana na maelezo yako nina mashaka ukiwa unafahamu nini maana ya muziki kwa sababu, ala ni sehemu moja ya muziki kati ya sehemu kuu mbili za muziki ambazo ni vocal na instrumental... muziki ni ama vocal au ala au mchanganyiko wa vyote kwa pamoja! ukisema kigezo kimoja wapo cha kuitwa mwanamuziki ni kujua kupiga ala ni kwamba unataka kubadili tafsiri ya nini maana ya muziki na kuondoa kile kipengele cha "ama vocal" na kubakiza vocal na instrumental... na kwa maana hiyo, wapiga ala wote ambao wengi wao sio waimbaji unataka kusema nao sio wanamuziki unless kama tubadilishe tena definition ya muziki kutoka kuwa vocal na instrumental na kubaki kuwa instrumental peke yake!!!kigezo kikubwa kimojawapo cha mtu kuitwa mwanamuziki ni kujua kupiga ala za muziki primarily piano na gitaa.
ukiachana na hilo, mwanamuziki inabid aweze kusoma nota za muziki kwenye karatasi na kuuimba hata kama aliyeandika nota hizo ni mtu wa taifa lingine anayetumia lugha tofauti na yake.
si lazima awe na uwezo wa kutunga wala kuwa na sauti nyororo.
tukija kwa domond, yeye ni just a msanii tu na wala sio mwanamuziki kutokana na kutokuwa na qualification za pale juu.
kwa bongo wanamuziki wapo wachache sana mfano mzuri ni BANANA & BARNABA, at least hao ndio waliokuja kichwan fasta.
View attachment 238365
Jana, Wakati akihojiwa na Mwanadada Shadee kwenye Kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, Msanii 'Fundi wa Muziki' kutoka nyumba ya vipaji THT, Barnaba Elias 'Barnaba', pamoja na mambo mengi aliyozungumzia, alitoa maelezo kuhusu wasanii watano anaowakubali na sifa zao Kimuziki ambapo alimtaja Msanii wa BongoFleva Diamond Platnumz kuwa sio 'Mwanamuziki' mwenye kujua kuimba muziki kiufundi.
Akifafanua kauli yake kwa mapana , Barnaba alieleza kwamba Diamond hajui kuimba kufuatana na alama zote muhimu za muziki, bali hutumia mtindo flani wa kuimba 'kiujanja', mtindo ambao kwa wanaojua kuimba muziki technically huwa wanautumia pale wanapofeli kufuata kanuni za uimbaji wakati wakiimba.
Hata hivyo, alimsifia kwa kuwa 'mjanja' na kuweza kufanya muziki wake kuvutia na kuleta ladha.
Orodha ya wasanii ambao aliwatolea maoni na kusema ni wasanii anaowakubali sana ni pamoja na, Diamond, Ally Kiba, Ditto, Amini na yeye mwenyewe.