Barnaba: Diamond sio Mwanamuziki

Barnaba: Diamond sio Mwanamuziki

Lol taarabu na kibao kata kama kawa kumekucha....umeumia roho tu sie tutasikiliza na kudansia

Kizuri sifia nawe utaona mazuri kwako.

Vipi wewe ulisifia mwimbo wa kiba au wanjera hahaha mi si mkata viuno bana twaaarab no no no nimekuachia weye mpenda majungu
 
Vipi wewe ulisifia mwimbo wa kiba au wanjera hahaha mi si mkata viuno bana twaaarab no no no nimekuachia weye mpenda majungu

Mpenda majungu ni wewe unaye quote na kuandika ----- au nyie mlio na majungu Tanzania style ya kutungia mtu uongo na pia kulazimisha maneno.

Sasa kiba kaingiaje....

Haya mbele elekea....
 
namuunga mkono barnaba pale kwa chibu hakuna mziki ndio nilisema juzi kuwa anabebwa na mapromo tu watu wakanishambulia hatari,nikasema aende kwa KIBA afundishwe mziki bado nikashambuliwa haya sasa barnaba nae kasema mshambulieni nae

Hahahaaa ulivoongea utadhani Barnaba ndo Mungu akiongea lake basi halibadilishwi tulichukue lilivyo kama maneno ya msaafu. Mfyuuuuuuuuuuuuu
 
Haya makasheshe na wanawake yatampoteza dogo, badala ya kuwaza muziki ye anawaza kushindana na watalaka wake na scandal zao, mara bifu na alikiba, pia naskia ana nyodo sana now days hasa katika malipo ya show zake, naliona anguko lake

We mgeni Tanzania eeh? No wonder bado unatabiri anguko la Diamond, wenzio wameanza kupiga ramli since 2010. Kiko wapi? Chukueni vigoda mkae msubiri.
 
fatilia maelezo yangu kwa makin
Nimekusoma maelezo yako mwanzo hadi mwisho... kwanza umechanganya vitu viwili... mosi, umechanganya kama ambavyo watu wengi wanavyochanganya kwamba kuwa mwanamuziki ni kufahamu kupiga ala... hiyo sio tafsiri sahihi ya mwanamuziki... hapo unamzungumzia instrumentalist! Muziki unaundwa ama na vocalist au instrumentalist or both wakati wewe tafsiri yako umemu-exclude vocalist moja kwa moja.

Kingine ulichochanganya ni kati ya professional musician and unprofessional musician. Kuna post moja nimeeleza hili kwa kirefu. Professional ni yule anayefahamu staffs, clefs na notes pamoja na application zake na matawi yake yote. Na ndio maana nikamalizia kusema, katika hilo sidhani kama kuna mwana-bongo flavor tunayeweza kumuita professional musician including huyo Barnaba.

Tofauti kubwa ya Barnaba na wengine ni kwamba, wakati majority ya musician wetu wanabaki kama vocalist peke yake Barnaba ni vocalist na pia ana "idea" na upande mwingine wa muziki, yaani upande wa ala! Nasema ana "idea" coz' huwezi ukaita instrumentalists Tanzania halafu Barnaba nae akawa mmoja wao!

But all in all, ukisoma kwa makini maeleozo ya Banarba yanaonesha wazi anazungumzia suala la professional na unprofessional musician na kwa maana hiyo, message yake ni kwamba Diamond sio professional musician na kwa maana hiyo sio professional singer vile vile... na hapo yupo sahihi kwa 100%.
 
Masikini Barnaba! Bora ungebaki na hili jambo moyoni tu maana wenzio huku tuna maadui wengi sana kisa kusema ukweli kua Diamond sio mwanamuziki na hajui kuimba!
Wewe sasa ndo unataka kuipotosha kauli ya Barnaba ili watu wamuone mbaya! Barnaba amesema Diamond hajui kuimba au amesema hajui kuimba kiufundi? Sasa kama hajui kuimba inakuwaje tena anasema miongoni mwa wasanii anaowakubali ni pamoja na Diamond?

Maelezo ya Barnaba kama unaifahamu taaluma ya muziki anachomaanisha ni kwamba Diamond sio professional musician na hata kama tutamuita singer, vile vile sio professional singer... na hapo Barnaba yupo sahihi! Tunaposema professional musician/singer ni yule anayefahamu kitu kinachoitwa music language... anafahamu staffs, clefs pamoja na notes including mambo mengine yanayoendana na hayo! Katika hili, hakuna mwana-Bongo Flavor hata mmoja unayeweza kumuita professional musician au professional singer kwa sababu sidhani kama kuna anayeifahamu hii lugha ya muziki!

Tofauti ya Barnaba na wenzake ni kwamba yeye ni vocalist (one part of music) na pia ana idea ya some of the instrumentals (second part of music) wakati waliobaki wengi ni just vocalists/singers na wote sio professional vocalists/singers.

Chukua hiyo mtoto mzuri ili siku nyingine usije ukaniabisha walipo watalaamu wa muziki kwa kushindwa kutofautisha kati ya professional na unprofessional singers/musician!
 
We mgeni Tanzania eeh? No wonder bado unatabiri anguko la Diamond, wenzio wameanza kupiga ramli since 2010. Kiko wapi? Chukueni vigoda mkae msubiri.
binti kiziwi, trust me my dear, Diamond atawapa watu ugonjwa wa moyo nchi hii. Halafu hakuna kinachonishangaza kama kuona miongoni mwa wengi wanaoumia ni wanaume... yaani mwanaume unakuwa na wivu wa mafanikio ya mwanaume mwenzako... am feeling very sorry for them! Wakati wengine hapa kila cku tunaumiza kichwa, kulala hatulali ili tufike mbali zaidi ya pale alipofikia Diamond kwenye kile tunachokifanya, wengine wanahangaika kusubiri waone fulani na fulani anaanguka!!!
 
namuunga mkono barnaba pale kwa chibu hakuna mziki ndio nilisema juzi kuwa anabebwa na mapromo tu watu wakanishambulia hatari,nikasema aende kwa KIBA afundishwe mziki bado nikashambuliwa haya sasa barnaba nae kasema mshambulieni nae
Twende taratibu kijana... Mosi, Je unaufahamu muziki? Kama unaufahamu, muziki ni nini? Na kwa maana hiyo, mwanamuziki ni nani au tafsiri ya mwanamuziki ni ipi? Tuanzie hapo kwanza!
 
Mara kwa mara watu wanachanganya sana haya mambo kwa sababu wengi wanaongea vitu kwavile walisikia mahali na wala hawana utaalamu wa jambo lenyewe! Katika hili, wengi sana utawasikia fulani sio mwanamuziki bali ni muimbaji! Kwa mtaalamu wa muziki akishakusikia unatoa hiyo hoja moja kwa moja anafaamu kwamba taaluma ya muziki hauifahamu!

Jambo la kwanza watu wanalotakiwa kulifahamu ni kwamba mwanamuziki anatokana na muziki! Kutokana na hilo, mtu anaye-perform muziki ndie anaitwa mwanamuziki! Ukirudi kwenye muziki wenyewe, pia unagawanywa katika makundi mawili makuu, vocalists yaani waimbaji na instrumentalists ambao ni wacheza ala za muziki! Ukitaka kusema mwimbaji sio mwanamuziki ni kwamba unataka kusema mpiga ala peke yake ndie mwanamuziki wakati hata tafsiri rasmi ya muziki ni kwamba "ni sauti/vocal au ala au mchanganyiko wa vyote kwa pamoja..." Kwahiyo hata mtu anayefanya akapela peke yake, kwa kuzingatia tafsiri ya muziki nae ni mwanamuziki na mwanamuziki wala sio kutembea na gitaa!

Aidha, huyu muimbaji hata kama hafahamu kupiga ala bado katika uimbaji wake analazimika kufuata ala za muziki kama ambavyo wakati mwingine mpiga/waiga ala za muziki (w)anapolazimika kutengeneza ala kulingana na uimbaji wa vocalist na ndio maana hata muimbaji akienda studio na hana uzoefu, kitu cha kwanza atakachoambiwa aimbe akapela ili mtengeneza beats afahamu ni beat za aina gani anaweza kwenda nazo! Ni kama ambavyo mpiga tumba, guitar, saxophone, violin, keyboard na kadhalika anapolazimika kubaki kwenye kifaa chake (eneo moja la muziki as instrumentalist) ndivyo muimbaji anapolazimika kubaki kwenye eneo lingine la muziki as vocalist!

Hoja ya Barnaba angekuwa ameongea kitaalamu angesema Diamond sio profession musician na kimsingi, alichokisema Barnaba kinamaanisha hivyo kwamba Diamond sio professional musician kwa sababu kutokujua kuimba sio kigezo cha kutokuwa mwanamuziki! Profession musician ni yule ambae amesomea muziki, anafahamu staff, notes na clefs kwenye muziki na maana na pia application zake! Hizi staffs, clefs na notes nazo zimegawanyika hadi unachanganyikiwa! Na katika hili, I doubt kama kuna mwana bongo flavor tunayeweza kumuita professional musician... katika hili ni lazima uende music school!

Tofauti ya Barnaba na wamamuziki wengine (including Diamond) ni kwamba, tukichukua pande mbili za muziki, kwamba ni uimbaji na uchezaji ala, Barnaba ni mwimbaji na vile vile ana "idea" na baadhi ya ala za muziki wakati wengine wengi ni waimbaji peke yake!

Umemaliza mzazi..very technical information, ndicho hasa wana bongo fleva wengi.wanachokosa...elimu stahiki ya muziki.
 
Kwa hii nasema nawe lazima achukue kumi za Kilimanjaro maana kagusa mioyo ya watanzania wengi
Mwaka 2005 wakati Jakaya Kikwete aliposhinda kwa kimbunga, kuna watu walihojiwa including Profesa Lipumba! Moja ya amazing comments ni pale baadhi ya watu waliposema "huyu Kikwete sijui ana power ya aina gani... manake unakuta mtu unajiandaa kwenda kumpigia kura ya HAPANA lakini unajikuta umemwekea kura ya NDIYO!!!! Haya ndiyo yatatokea kwa Diamond mwaka huu... manake wengine wataanza kutuma message kwa fujo kwa hata wasiostahili ili kura za Diamond zisitoshe lakini watajikuta wanampigia yeye kutokana na kiwewe!!!
 
namuunga mkono barnaba pale kwa chibu hakuna mziki ndio nilisema juzi kuwa anabebwa na mapromo tu watu wakanishambulia hatari,nikasema aende kwa KIBA afundishwe mziki bado nikashambuliwa haya sasa barnaba nae kasema mshambulieni nae

duh! akabane pua au. halafu kina davido mnaona ni wanamuziki sio?
 
ha ha ha Naseeb anatesa sana watu,

Go Chibu go

Wabongo tujifunze kuombeana Mwisho mwema,
Huu Uchawi tunao jipa hauna faida yoyote.
 
Back
Top Bottom