Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
namuunga mkono barnaba pale kwa chibu hakuna mziki ndio nilisema juzi kuwa anabebwa na mapromo tu watu wakanishambulia hatari,nikasema aende kwa KIBA afundishwe mziki bado nikashambuliwa haya sasa barnaba nae kasema mshambulieni nae
Mara kwa mara watu wanachanganya sana haya mambo kwa sababu wengi wanaongea vitu kwavile walisikia mahali na wala hawana utaalamu wa jambo lenyewe! Katika hili, wengi sana utawasikia fulani sio mwanamuziki bali ni muimbaji! Kwa mtaalamu wa muziki akishakusikia unatoa hiyo hoja moja kwa moja anafaamu kwamba taaluma ya muziki hauifahamu!
Jambo la kwanza watu wanalotakiwa kulifahamu ni kwamba mwanamuziki anatokana na muziki! Kutokana na hilo, mtu anaye-perform muziki ndie anaitwa mwanamuziki! Ukirudi kwenye muziki wenyewe, pia unagawanywa katika makundi mawili makuu, vocalists yaani waimbaji na instrumentalists ambao ni wacheza ala za muziki! Ukitaka kusema mwimbaji sio mwanamuziki ni kwamba unataka kusema mpiga ala peke yake ndie mwanamuziki wakati hata tafsiri rasmi ya muziki ni kwamba "ni sauti/vocal au ala au mchanganyiko wa vyote kwa pamoja..." Kwahiyo hata mtu anayefanya akapela peke yake, kwa kuzingatia tafsiri ya muziki nae ni mwanamuziki na mwanamuziki wala sio kutembea na gitaa!
Aidha, huyu muimbaji hata kama hafahamu kupiga ala bado katika uimbaji wake analazimika kufuata ala za muziki kama ambavyo wakati mwingine mpiga/waiga ala za muziki (w)anapolazimika kutengeneza ala kulingana na uimbaji wa vocalist na ndio maana hata muimbaji akienda studio na hana uzoefu, kitu cha kwanza atakachoambiwa aimbe akapela ili mtengeneza beats afahamu ni beat za aina gani anaweza kwenda nazo! Ni kama ambavyo mpiga tumba, guitar, saxophone, violin, keyboard na kadhalika anapolazimika kubaki kwenye kifaa chake (eneo moja la muziki as instrumentalist) ndivyo muimbaji anapolazimika kubaki kwenye eneo lingine la muziki as vocalist!
Hoja ya Barnaba angekuwa ameongea kitaalamu angesema Diamond sio profession musician na kimsingi, alichokisema Barnaba kinamaanisha hivyo kwamba Diamond sio professional musician kwa sababu kutokujua kuimba sio kigezo cha kutokuwa mwanamuziki! Profession musician ni yule ambae amesomea muziki, anafahamu staff, notes na clefs kwenye muziki na maana na pia application zake! Hizi staffs, clefs na notes nazo zimegawanyika hadi unachanganyikiwa! Na katika hili, I doubt kama kuna mwana bongo flavor tunayeweza kumuita professional musician... katika hili ni lazima uende music school!
Tofauti ya Barnaba na wamamuziki wengine (including Diamond) ni kwamba, tukichukua pande mbili za muziki, kwamba ni uimbaji na uchezaji ala, Barnaba ni mwimbaji na vile vile ana "idea" na baadhi ya ala za muziki wakati wengine wengi ni waimbaji peke yake!
Huhuhuhuhuuu Banaba boy could be very right diamond huenda hana kipaji cha kuzaliwa wala cha THT, lakini msichotaka kukikubali ni fact kwamba diamond anajua kunata na bits, kijana ni mbunifu, anajua kusoma saa ya mshale, kijana ANAJUHUDI za wazi tangible works and thats what we who loves hard working people are mad at, NOTA sijui KEY za mziki bakini nazo nyie akina barnaba sijui nani LAKINI mtaishia kusugua gaga hapa tz miaka nenda miaka rudi, show zenu kubwa zitabaki kuwa fiesta na KLM
Hiyo BET atapigiwa kura na wanaijeria siyo? Tehteh
kumbe unadhania watanzania ni nyie mnaomchukia tuu, sisi tunaompenda tutakuwa wapi???
Haya makasheshe na wanawake yatampoteza dogo, badala ya kuwaza muziki ye anawaza kushindana na watalaka wake na scandal zao, mara bifu na alikiba, pia naskia ana nyodo sana now days hasa katika malipo ya show zake, naliona anguko lake
hahahahahahahaaaaa unaliona anguko lake??? have a sit plzzzz, unatumia kinywaji gani???
hahahahahahahaaaaa unaliona anguko lake??? have a sit plzzzz, unatumia kinywaji gani???
Kama sio mwanamziki ni mwana nani? Barnaba hajui aina za muziki zilizoko duniani ndio maana kasema hivyo, kuna siku atasema hata Saida karoli si mwanamziki kwa kuwa kakulia shamba.
Kuna mziki wa kufundishwa kidigitari,
Kuna mziki wa mapokeo yaani umejikita kwenye jamii husika bila kuusisha vifaa vya technologia ya kizungu. hivyo basi huenda barnaba hajui mziki kwani analazimika kutumia vyombo zaidi vya kumsaidia kuimba.
mimi sijui muziki kiukweli, japo mziki mtamu ninaufeel bila ukakasi, huenda barnaba anaujua mziki, sheria zake kutumia vyombo na vitu kama hivyo, kwa sababu amekuwa trained LAKINI it is very sad kwa kweli kusema as for me hakuna wimbo wa banaba hata mmoja wenye ladha jamani sio ya sukari wala ya chumvi hata utie ndimu nyimbo zake ni flat kama rula.
Huhuhuhuhuuu Banaba boy could be very right diamond huenda hana kipaji cha kuzaliwa wala cha THT, lakini msichotaka kukikubali ni fact kwamba diamond anajua kunata na bits, kijana ni mbunifu, anajua kusoma saa ya mshale, kijana ANAJUHUDI za wazi tangible works and thats what we who loves hard working people are mad at, NOTA sijui KEY za mziki bakini nazo nyie akina barnaba sijui nani LAKINI mtaishia kusugua gaga hapa tz miaka nenda miaka rudi, show zenu kubwa zitabaki kuwa fiesta na KLM
Huyu barnaba akalale mbele wivu tu, yeye anayemjua muziki basi mbona hata hajulikani kama Diamond duniani?
Wivu...
Haya Diamond kashusha mwimbo mpya na Khadija Kopa kasikilize na video juu bomba yaani usikose utapitwa
Ww ndo kama Mondi alowasema Barnaba
Mpe konyagi yenye jina lake pulizzzzzzz 😭😭😭
hahahah au mondi ashakulipa ya kumkatia mauno? Anyway ninunulie chochote beibe na haka kamvua kitashuka muruuuuuaaa
Diamond si mwanamuziki ni muimbaji. kwa hiyo Barnaba is right..