Inauma kwasababu kelele za watanzania zimezoeleka, tunapiga kelele weeee alafu tunanyamaza wanaume wanaendelea na kuinyonya nchi
Ndiyo maana nimesema something must be done!
Hawa viongozi tulio nao hawajaonja nguvu ya wananchi hata siku moja. Something must be done wananchi.
Hizi kelele tunazopiga wameshazizoe ndio maana wanasema huo ni upepo.
Wanafahamu kuwa Watanzania hawana utamaduni wa kuwaadabisha viongozi wao! Something must be done!
Tatizo la umeme limekuwepo kuanzia Kikwete akiwa waziri wa nishati. Alipoingia madarakani alikuta tatizo ni kubwa.
Kwa miaka sita Rais Kikwete hana suluhu ya muda mfupi au muda mrefu. Amekaa pembeni wezi wakiwapora Watanzania kwa kupitia wizara ya nishati na Tanesco,IPTL aliyosaini, Richmond aliyoshirikiana na PM lowassa na madudu mengine.
Madudu yote yaliyofanywa na akina Lowasa,Karamagi, msabaha akina Mboma na juzi akina Mhando, juzi kumefichuliwa ufisadi wa kutosha, serikali imekaa kimya kana kwamba haina Viongozi.
Rais Kikwete anafahamu fika kuwa mgao ni njia ya kuuza mafuta achilia mbali majenereta.
Anafahamu kuwa bila nishati ya uhakika hakuna mwekezaji anayeweza kuchukua risk ya investment.
Kila kukicha yupo New york akigonga kengele za DOW JONES eti anatafuta wawekezaji.
Kama kuna kiongozi anayelitia taifa hili umasikini licha ya ule uliopo, historia haitakamilika endapo jina la Kikwete halitatajwa.
Rais amekaa kimya nchi inaporwa, kana kwamba nchi haina uongozi! something must be done.
Huko migodoni ni wizi tu na kuwaachia wananchi mashimo na mercury ili wafe taratibu.
Hakuna kiongozi anayeshtuka. Kikwete analiangamiza taifa hili.
Ujanja wa kutumia tume za kuchunguza umekwisha, sasa hivi wanatumia bunge kama kichaka cha kurahisisha masuala ya kitaifa ili wapate nafasi ya kupora huku wakirithisha watoto wao uporaji kule Uswiss. Something must be done dudes.
Watanzania muda wa kulalamika umekwisha sasa, hivi ni muda wa kutenda, hii nchi ni yetu si yao.
We must stand and do something! something must be done.
Tutawaachia watoto wetu umasikini kutokana na utajiri wa kundi dogo sana. Something must be done!
Tusiposimama na kuwapa ujumbe mahususi na wenye funzo, basi wake zetu na dada zetu wataendelea kujifungulia juu ya baiskeli na matenga. Tutaendelea kufa bila matibabu huku wake zao na familia zao wakitibiwa Appolo.
Watoto wetu watakatwa vitovu kwa kutumia chupa za soda huku wake zao wakitibiwa chunusi South Africa.
Watoto wetu wataishia kukaa katika mawe tukiambiwa shule za kata, watoto wao watasoma ng'ambo ili warudi kurithi viti vya baba zao.
Umasikini wetu si rasilimali, ni umasikini wa akili zetu zinazoamini wanachosema hawa waporaji.
Ufakara wa akili zetu unaotutuma tuamini kuwa Kusimamia rasilimali zetu ni kuvunja amani na utulivu.
Wenye amani na utulivu ni Serikali na Wabunge, wewe na mimi hatuna amani tuna woga!
Ni woga wetu umetufikisha mahali tunapowalipa mshahara ili wafanye kazi za kuteteana kwa hoja za kipuuzi bungeni na kwingineko.
Ni woga wetu nunaotufikisha hapa, ni woga unaotudhalilisha kiasi hiki.
Woga waliouita amani na utulivu unatutokea puani kila uchao huku tukiangalia ndugu zetu wakikata roho bila matibabu, watoto wakiwa wezi kwa kukosa elimu, wengine wakifanya umalaya ili kujikimu kwa dhiki.
Katika nchi tajiri kama Tanzania watu wa kulaumiwa si genge la serikali au wapiga soga bungeni, ni sisi wananchi kwasababu tumeshindwa kujitetea, kutetea nafsi zetu, kulinda rasilimali zetu na tumewapa haki na hati miliki ya nchi yetu.
Sisi ndio wa kulaumiwa si wao. Unless we do something these gangstars will treat us like dogs!
Something must be done! Watanzania something must be done now!
muda wa kulalama umekwisha sasa ni muda wa kutoa ujumbe kwa hawa wezi na kundi liwalindalo.
Something must be done!