Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Kampuni ya Barrick Gold Corporation imetangaza kuanza hatua ya usitishaji wa shughuli zake kwa muda katika mgodi wa Loulo-Gounkoto uliopo nchini Mali.
Hatua hiyo imekuja kutokana na mvutano kati ya kampuni ya Barrick na serikali ya Mali kuhusu taratibu mpya za ugawanaji mapato yanayotokana na shughuli za uchimbaji madini.
Vilevile, serikali ya Mali imeanza kuhamisha dhahabu yenye thamani ya kiasi cha dollar za Marekani milioni 245 kutoka kwenye mgodi wa Loulo- Gounkoto kwenda kwenye mojawapo ya benki jijini Bamako.
Mgodi wa Loulo- Gounkoto ni muhimu kwa kampuni ya Barrick kutokana na kuchangia asilimia 15 ya dhahabu yote inayozalishwa na kampuni ya Barrick.
Katika siku za hivi karibuni, serikali ya nchini Mali imechukua hatua za kuongeza kiasi cha mapato inachoingiza kupitia shughuli za uchimbaji madini kwa kupitia upya mikataba kati ya serikali na makampuni ya uchimbaji madini.
"Barrick - Barrick Provides Further Update on Loulo-Gounkoto Operations in Mali" Barrick Provides Further Update on Loulo-Gounkoto Operations in Mali
"Barrick suspends mining activities after Mali seizes $245 million gold | Business Insider Africa" Barrick suspends mining activities after Mali seizes $245 million gold