Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Umejitahidi kueleza vizuri na kistaarabu kuliko wale waimba mapambio na kuabudu wanaoishi kuporomosha matusi. Kwa vile bado makinikia yataendelea kupelekwa nje tusitegemee makubwa. Pia tusijitangazie ushindi dhidi ya acacia kwani ni walewale ila wamebadili majina na maelezo kutuweka sawa
 
Na wewe badala ya kumuelewesha tu mwenzako kwa wema kabisa, unakimbilia kwenye hoja dhaifu eti 'vijana wa Zitto"! una uhakika gani kama ni kijana wa Zitto? Mbona wenzako wamefafanua vizuri tu hapo juu!
Huyu ni praise team
 
Unafahamu kuwa faida ni manipulatable?
 
Hapo prof Kabudi alikuwaa anatoa taarifa yaa 84%/16% = 50/50 huku macho yamemtoka hata kiini cha macho havichezi
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
Labda, nasema labda tu...

16% hisa + 4% mrabaha wa madini + 30% corporate tax = 50%
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
Kwa akili zangu ndogo hizi nilizo nazo,najua hisa zikiwa 50/50,faida nayo inakuwa 50/50.Najua pia kwamba ukiwa na hisa kidogo,umiliki wako wa kampuni unakuwa mdogo,kwa hiyo yapo mambo ambayo yatafanyika bila wewe kuhusishwa.Kwa mfano,unaweza usifahamu faida imepatikana kiasi gani hasa,kwa hiyo ukaletewa figa yeyote ukaambiwa ndio faida, sasa kwa kuwa hukuhusika kwenye kuikokotoa hiyo faida, itabidi ukubali.Huo ni mfano tu,lakini kama unamiliki hisa kidogo yapo maeneo mengi mengine ambayo inawezekana usihusishwe.Anayemiliki hisa nyingi kiukweli ndiye pia anayefanya maamuzi mengi na ya msingi.Kama kweli tumeambiwa tutamiliki 16% of the shares,ila tutagawana faida 50/50 ni kiini macho.Na scenario hiyo sijawahi kuisika anywhere else,I think it is only possible in Tanzania.
 
Naona kikubwa kilicho ongezeka ni hiyo asili mia kumi na sita (16%), kwa kifupi hivyo vyote vingine kama alivyoweka #94 havina mabadiliko ni kodi na tozo nyingine zile zile. "Economic benefit inajumlisha pia hiyo 16% na SIYO FAIDA baada ya kutoa gharama. Wataalamu wa HAKIRASILIMALI (#82) wameielezea kwa nini BARRICK wameiweka hivyo. Wanasema hii itahahakisha kuwa hata kama mapato/faida itaongezeka progressive taxation haiwezi kuruhusu Serikali ipate zaidi ya 50% ambayo kama kipengele hiki kisingekuwepo hilo lingewezekana.
 
It's funny how Kenyans are trivialising this barrick issue and yet they have not even decolonised the fertile farms held by Britain and their black collaborators. Bure kabisa. Watu wa njaa kila mwaka.

Minerals are on another level harder than land issues!
 
Sioni tofauti ya kikokotoo cha mafao ya kujitoa, heavy zake zinalandana
 
Kama kweli tumeambiwa tutamiliki 16% of the shares,ila tutagawana faida 50/50 ni kiini macho.Na scenario hiyo sijawahi kuisika anywhere else,I think it is only possible in Tanzania.
Mkuu 50/50 maana yake ni tutakacho pata ni hiyo 16% pamoja na kodi + tozo nyingine na hivyo visizidi 50% ya hizo economic benefit. Matokeo yake ni kwamba hata shares zetu ingawa sheria inaruhusu kuziongeza hadi 50% makubaliano haya na BARRICK hayataruhusu kwani kwa kufanya hivyo itabidi mgawane 50/50 lakini hapo hujaweka kodi na tozo nyingine ambazo mgao wa GoT utavuka 50%. BARRICK wamejilinda au wamelindwa na serikali hapo kitu ambacho wataalamu wa HAKIRASILIMALI wanasema ni kinyume na sheria zetu wenyewe. Hivyo lugha hiyo kwa sisi tusiofahamu ni mziki mtamu kisiasa kama wengi wanavyofurahia hapa. Kitu pekee cha kufurahia ni hiyo 16% from ZERO (0) %.
 
Mitambo na gharama za uendeshaji...60%
Barick....……........................................16%
Tanzania............................................... 16%
Ukarabati wa mitambo na riba za kibenki...8%
 
Licha ya kwamba umeshafanya hitimisho mleta mada unaweza kuwa na hoja yenye mantiki katika mtazamo ufuatao:-

Kila "shareholder"-mwanahisa hupata gawio la faida kulingana na asilimia ya hisa zake ambazo ndio zinaamua kiwango cha uwekezaji wake katika kampuni.
Imezoeleka hivyo lakini haina maana kwamba mara zote huwa hivyo katika kila mkataba.

Sasa turudi kwa kile ambacho Waziri amekisema.
1. Kampuni ya Twiga inaundwa kati ya Serikali ya Tanzania na Barrick Gold.
2. Tanzania ina hisa asilimia 16 na Barrick wanahisa asilimia 84.
3. Mgawanyo wa faida ni 50% kwa 50%

Lakini kabla ya kujiuliza kwa nini hisa 16% zizae gawio la faida 50%. Embu tujifunze kidogo.

Uwekezaji kwenye madini unasimamiwa na sheria ambayo una vipengele vingi vinavyoleta tofauti katika muktadha wa uwekezaji katika nchi husika.
Ukiachilia mbali sheria na kanuni zake bado Waziri aliongeza neno pale ya kwamba "tumekubaliana".
Kabla ya kujadili sana nadhani ni muda sasa kama ambavyo imekuwa ikiombwa na wadau wengi kuwa mikataba ya uchimbaji madini iwekwe wazi.

Mara nyingi tumejikuta tukijadili muhtasari bila kujua hasa "content" nzima ya mkataba husika.

Kinachonisikitisha ni wengi kuleta mada au kuchangia mada kwa nadharia bila kuwa na taarifa sahihi za jambo husika.

Nimalize kwa kusema tu kuwa inawezekana kwa "nature" ya mikataba ya madini kwa "shareholder" mwenye hisa 16% kupata gawio la 50% katika faida kutegemeana na nafasi yake katika mkataba.
Unaweza kujifunza zaidi mikataba katika nchi zenye mafuta. (Africa and Asia Oil Producing Country).
 
Nonsense.

Why do you fear the unknown things?

Temerity is very important in this world when you want to be a successful one. But if you keep cuddling fears, you will not get where you want. Some challenges are there just to make you grow stronger, etc.
 
Uko sahihi sana lakini eleza jinsi Dividend itakavyotolewa kwa wanahisa. Nafikiri ni mpaka kampuni ipate faida ambapo serikali itakula kwanza 30% ya corporate tax and then kama kampuni itaamua kutoa faida mgawanyo kwa wana hisa utakuwaje? Tutazame the end result ya uwekezaji kwamba pamoja na maximize wealth lakini kuna mgawo wa faida mwishoni.
 
I really wonder why Tanzanians have allowed Barrick to control them. But life is all about choice. That's what they have chosen.
Barrick ndio wenye usemi pale, Tz govt Ni puppet wa barrick Ila nyie wananchi mnafumbwa tu macho huku mkiliwa na mabeberu. Ndio ukweli lakini utakuja na maneno ya CCM kuwapumbaza wenzako and btw how is this Kenyan news?
 
Don't defend hogwash brother.

Madini yako tena utoe cent? Hujui kwamba madini tayari ni stock and can be converted into shares?
wewe ndo uamke ama uniambie kampuni gani EA imepewa 16% without putting up a cent and sharing revenues 50-50!
 
Wewe tu ndio hufahamu 8 4:16 maana take ni hivyo hivyo hata kwenye mgawanyo wa faida. Ushawahi kuona biashara ya hivyo hata kama wote hatuna akili
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
Kwa hiyo wewe unaakili sana kuliko wataalamu waliojadili na kufikia matokeo hayo?

Kibaya zaidi unahisi. Wataalamu hawajafanya mambo kwa kuhisi. Kuna wataalamu wa uchumi, mipango na sheria hapo. Wabongo tuache longolongo za kuzungumzia tusiyoyajua kuonesha tunayajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…