Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Kwa uelewa wa maandishi kama yatakuwa hivyo ni kuwa Sheria ya madini 2010 na marekebisho yake 2017 inaeleza kuwa kwa Mgodi wowote unaoanza serikali itakuwa na hisa bure(Free) 16% na Mwekezaji 84% hii ni kuwa uendeshaji na shughuli zote zitakuwa za muwekezaji bila serikali kuweka chochote, ila serikali inauhuru wa kuongeza umiliki mpaka 50%, na hii 50/50 ni mgawanyo wa faida baada ya kutoa gharama za uendeshaji. Kama itafanyika hivyo kweli itakuwa faida kwa nchi
Hii faida itapatikanika kama tufikiriavyo? Isije jirudia ile ya kila wakati kutangaza hasara au faida kiduchu
 
Hii faida itapatikanika kama tufikiriavyo? Isije jirudia ile ya kila wakati kutangaza hasara au faida kiduchu

Natumaini itapatikana kwa sababu zifuatazo:
1) Kwenye Management watakuwa wote Serikari na Barrick na pia kila mmoja kuweka wawakilishi katika kampuni hiyo Mpya Twiga, hivyo maamzi yoyote pande zote zinakuwepo
2)Natumaini pia kwa wafanyakazi mbalimbali watakuwepo wanaoiwakilisha serikali waziwazi na sirisiri
3)Ukaguzi wa mahesabu na manunuzi ukizingatiwa vizuri na kwakuwa makao makuu yatakuwa Mwanza itakuwa rahisi kusimamiwa
 
Huyu majicho kabudi sio wa kumuamini. Nikikumbuka habari ya kampuni ya Indo Power kutoka Kenya, sina imani naye kabisa.
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie

Hapana.

Nadhani kuna mengi tusiyoyaelewa bado katika makubaliano hayo, na yanahitaji kuelezwa kwa njia rahisi kwa wenye ufahamu wa mambo kama haya.

Bila shaka ufafanuzi mzuri wa makubaliano haya yatakuja kuelezwa, ama na wahusika wenyewe ndani ya serikali, kuwajulisha wananchi tulichopata, au na wabobezi wa lugha hizi za kimikataba.

Kwa mtu kama mimi asiye na uelewa mkubwa wa 'jargon' hizi zinazotumika, kama "a free carried shareholding," au kitu kama "An annual 'true-up' mechanism," kidogo ninafarijika kwa kujua kuwa hali kidogo si haba; sio kama ilivyokuwa wakati wa Acaccia, ambapo hata hiyo namba tu ya 16% ilikuwa haionekani popote.

Utofauti unazidi kujitokeza ninaposoma vitu kama, "The GoT will 'participate in all cash distribution made by the mines and Twiga."
Au, 'statements' kama: "Twiga...will give the government 'full visibility of and participation in operating decisions made for and by the mines..."

Haya yote sio ya kubeza hata kidogo, na hayakuwepo kabisa enzi za Acaccia, na sijui kama yamo katika mikataba ya makampuni mengine nchini.

TAHADHARI ni moja tu. Sisi wenyewe kuyatimiza hayo ipasavyo. Tukimpa Karamagi ayasimamie hayo atayafanya kwa uaminifu, uzalendo wa nchi yake. Huo ni mfano tu, maanake huko ndiko tulikoanzia hadi hapa tulipofika leo.

Kwa hiyo, kwa maoni yangu, tusibeze tulichopata, hata kama sio chote tulichonuia. Ni makosa tuliyafanya huko nyuma kuwapa hawa watu mali zetu kama hatuna akili kichwani.

Napongeza yaliyofanyika, hata kama yalifanyika kwa vurugu. Sikupenda kamwe kuitana majina kama "Wasaliti" kwa vile tu hao wanaoitwa 'wasaliti' wanayo mawazo tofauti.

Palikuwa pia na upotoshaji ambao haukuwa wa lazima. Yale makinikia hata siku moja yasingeweza kuwa na thamani yaliyodaiwa kuwa yanayo. Ndio maana waliohusika katika upotoshaji huo wakapewa jina stahiki kabisa la "Profesorial Garbage,' hata kama ninaelewa sababu iliyowafanya kujidhalilisha vile kama wataalam wetu.

Nimalizie kwa kusema kwamba siijui misimamo ya vyama vya upinzani, hasa CHADEMA kuhusu mali zetu za taifa kama madini. Je, wao wangekuwa madarakani wangefanya nini ili taifa linufaike na hizi mali?

Msimamo wa Zitto Kabwe, ambao pengine ndio msimamo wa ACT-Wazalendo unafahamika, kuwa unaegemea katika mapendekezo ya Tume ya Bomani.

Yote tukiyaweka kwa pamoja, walichofanya CCM (Magufuli) ni sehemu ndogo tu ya kuanzia. Inabidi , kama bado tunayo madini mengine ambayo bado yamo ardhini na hatujayauza kwa wawekezaji, inatubidi turudi kule kule kwenye dira ya waasisi wetu kuhusu madini haya.

Kiasi cha uwezo sasa tunacho cha kujitegemea na kunufaika zaidi na mali hizi alizotujaalia Mwenyezi Mungu. Tuache kuzitapanya ovyo kama akili kichwani hatuna.

Ile Helium kule Rukwa, ije itengeneze ma - mashine ya kupimia wagonjwa hapa hapa kwetu, tuwauzie waafrika wenzetu. Nchi zaidi ya 50, na mahospitali yote yale hatuwezi kukosa wanunuzi. Tuwaite Siemens, Philips, GE, waje wawekeze hapa, hata kama ni kuyaunganisha tu hayo ma-mashine na kuyajaza Helium yetu hapa hapa Tanzania.

Kama hawataki, tuwaite marafiki zetu waChina. Wao wanakopi kila kitu, watashindwa kuyafurumua na kuyaunganisha tena upya , wakitumia mali ghafi zetu wenyewe hapahapa!

Halikadhalika, sijui ni kwa nini tunatupa "Graphite" yetu nzuri kwa bei chee, huku mChina akihodhi ya kwake.
 
Kwa mtu kama mimi asiye na uelewa mkubwa wa 'jargon' hizi zinazotumika, kama "a free carried shareholding," au kitu kama "An annual 'true-up' mechanism," kidogo ninafarijika kwa kujua kuwa hali kidogo si haba; sio kama ilivyokuwa wakati wa Acaccia, ambapo hata hiyo namba tu ya 16% ilikuwa haionekani popote.
Tatizo liko hapa,hii jargon ni ya kitalaamu kwa kiasi kikubwa sasa kuna wanaotaka kutuaminisha wanajua maana yake kumbe sivyo kwani ukisoma maelezo yao yanatia shaka. Bahati mbaya wengi wetu tunasoma au kueleza mambo haya tukiwa tumevaa miwani za KISIASA - yaani moja kwa moja tunataka tu pambe au tupambue. Kuna hii nmeikuta hapa inafikirisha ingawa imetumia lugha ya malkia na kisheria kwa kiasi fulani (THE DOWNFALL OF ACACIA MINING PLC IN TANZANIA”: WILL TANZANIA GET A BETTER DEAL?).
 
Hiyo 50/50 ni zile kodi,tozo mbalimbali,CSR etc ndiyo hiyo 50/50.Na bado pia itapata stahiki za 16% kutoka kwa Twiga.
Nakukumbusha hiyo 50/50 siyo kwenye FAIDA bali ni kwenye ECONOMIC BENEFITS. Hivyo basi, it could also be NEGATIVE.
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie

Hiki ni chanzo cha mgogoro
 
Tusijisahaulishe kwamba na huyo mbia mwenye 16% makato hayo yanamhusu... maana shareholder hugawana faida na hasara
No share holder anapata dividend. Hiyo ni baada ya makato yote. Sidhani kama kuna hasara hapo. Labda igunduliwe njia nyingine ya kutengeneza dhahabu badala ya hii ya kuchimba!
 
4% to 16% unaona ni hatua kubwa sana? Kivipi ni hatua kubwa?

Madini ni yenu mnanyanyaswa then unajisifia kwamba ni hatua kubwa hiyo.

Kwanini Tanzania asimiliki asilimia 50 ya hisa na 50 zingine apewe Barrick?
Suala kusema kwamba hamna capital or teknolojia hizo ni lame arguments na ni ugonjwa mbaya sana kwenu nyie maana bila kujiongeza mtazidi kuonewa tu.
Tanzania ina migodi mingi ila bado umasikini unawasumbua sana.

Kwanini msibinafsishe hata migodi miwili tu kwa masharti kwamba wawape mashines za kila aina za kuchiba na kuchakata madini hapa hapa Tanzania?
Unajua wanao miliki biashara ya madini duniani? Hawa jamaa unatakiwa ushindanie nao kiakili, ukijifanya mjuaji sana wakati hata mapembe huna watakupiga vikwazo mpaka utatoka nyongo.

Hiyo jeuri tungojee mpaka 2040s huko wakati China na India watakapo kuwa nao wameota ndevu, kwa sasa inabidi twende hivyo hivyo.
 
Hiyo 16% haikuwepo awali, hivyo ni hatua nzuri, ndio mara ya kwanza Afrika kwa nchi kuingia mgawano wa pasu kwenye faida baina yake na mabeberu, Magufuli ametengeneza historia mpya.
 
Nakukumbusha hiyo 50/50 siyo kwenye FAIDA bali ni kwenye ECONOMIC BENEFITS. Hivyo basi, it could also be NEGATIVE.

FAIDA ni mojawapo tu wa ECONOMICS BENEFITS zipo nyingi, acheni kutafuta mchawi kwa kupindisha pindisha, hapa Magufuli kaweza, cha msingi ni ile kwamba amefaulu kuingiza kichwa, huko mbele ya safari kutakua na mbanano wa utakaongeza mazuri.
 
Serikali
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
Serikali INA his a makampuni mengi na ieleweke pia kuwa mwanahisa siyo kukas na kusubiri mgao was faida. Kuna majukumu
 
wewe ndo uamke ama uniambie kampuni gani EA imepewa 16% without putting up a cent and sharing revenues 50-50!
Barrick ndio wenye usemi pale, Tz govt Ni puppet wa barrick Ila nyie wananchi mnafumbwa tu macho huku mkiliwa na mabeberu. Ndio ukweli lakini utakuja na maneno ya CCM kuwapumbaza wenzako and btw how is this Kenyan news?
 
Unajua wanao miliki biashara ya madini duniani? Hawa jamaa unatakiwa ushindanie nao kiakili, ukijifanya mjuaji sana wakati hata mapembe huna watakupiga vikwazo mpaka utatoka nyongo.

Hiyo jeuri tungojee mpaka 2040s huko wakati China na India watakapo kuwa nao wameota ndevu, kwa sasa inabidi twende hivyo hivyo.
Si nyinyi Ni mibabe mbona msichukue hayo madini mara moja na yako ndani ya Nchi yenu?
 
Ujerumani inakopesha nchi wanachama wa EU zenye matatizo ya Kipesa, Tanzania tunataka kutumia rasilimali zetu ili kuzikopesha nchi za EAC zitakazopata matatizo ya kipesa.
Nyinyi mnaosamehewa Madeni 😂😂😂 Kweli viwonder mnachekesha.
 
Back
Top Bottom