Kampuni ya Twiga Minerals Company Limited ni alama ya ushindi kwa Rais wetu John Pombe Magufuli katika vita ya kiuchumi dhidi ya Mabeberu.
Na; Fahami Matsawili.
Miaka miwili iliyopita Rais wetu John Pombe Magufuli alitangaza vita ya kiuchumi ya kulinda rasilimali za Watanzania dhidi ya Mabeberu wa ndani na nje ya nchi yetu.
Alianza kwa kuzuia Makinikia ya mchanga bandarini ili kujua kinachosafirishwa ndani kina uhalisia na makubaliano ya mikataba yetu na Malipo kwa Taifa, akaunda Tume 2 za Madini kuchunguza, mwisho akapeleka mswaada wa Sheria 2 za Madini na rasilimali za Taifa bungeni kwa hati ya dharura....
Kama kawaida yao Mabeberu wakawatumia Zitto na Tundu lissu kupiga kelele ili kuupotosha Umma wa Watanzania kwa Hatua alizokuwa anachukua Rais wetu John Pombe Magufuli dhidi ya Mabeberu hawa ona sasa Leo wameufyata hawa watu hatuna budi kuwatangaza kama maadui wakubwa wa Taifa letu na Watanzania.
Leo hii tunayo Sheria ya Madini ambayo imezaa matunda ya kampuni ya Twiga Minerals Company Limited baada ya serikali na Kampuni ya Barrick kukubaliana hivyo hii ni kampuni itakayosimamia Migodi 3 Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu Migodi hii ilikuwa chini ya usimamizi wa kampuni ya Acacia kabla ya kufutwa na Hisa zake kununuliwa na Barrick sasa imezaliwa rasmi kampuni ya Twiga minerals company limited kampuni ambayo serikali ya Tanzania itamiliki Asilimia 16% na kampuni ya Barrick Asilimia 84%....
Mwaka jana, Bunge lilipitisha sheria mbili za madini ambazo pamoja na mambo mengine, zinaipa Serikali umiliki wa asilimia 16% kwenye kila mgodi uliopo au utakaoanzishwa nchini.
lengo la Sheria hii ni kuona Watanzania wananufaika na rasilimari zao na kuona Sekta ya Madini inatoa mchango unaostahili katika pato la Taifa kutoka asilimia 4.8 iliyopo hadi asilimia 10% kama Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano unavyosema.
Sheria mpya ya madini ya mwaka 2017 inakwenda kurudisha uchumi kwa Mwananchi wa Tanzania,
“Sheria mpya ya madini ya mwaka 2017 inataka kurudisha uchumi wa madini kuwa uchumi fungamanishi kwa sekta nyingine. Tulikuwa na Migodi ndani ya nchi ambayo ajira zote na Teknolojia zinapelekwa nje ya nchi kupitia huduma mbalimbali....
Sasa Sheria ya Madini no 5 ya mwaka 2017 ijulikanayo kama The written laws (Miscellaneous Amendments) Act 2017 iliyoanza kutumika 7/7/2017 Sheria hii imeleta mapinduzi katika sekta ya Madini ambapo Sasa
1. Malipo ya Mrabaha yatapanda kutoka Asilimia 4% hadi 6% kwa Madini ya Metali (dhahabu, shaba, fedha)
2. Kuongezeka kwa Malipo ya Mrabaha kutoka Asilimia 5% hadi 6% kwa Madini ya Vito (Tanzanite, Rubby, n.k)
3. Madini yatakaguliwa na kuthaminishwa nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi kwa gharama ya Asilimia 1% ya thamani ya Madini hayo (Clearing fees)
4. Mchimbaji mdogo anayeuza Madini kwa broker au kwa Dealer atakatwa Asilimia 5% ya thamani ya Madini kama withholding tax...
5. Sheria hizi zinatoa fursa kwa serikali kupitia upya mikataba yote ya madini na kutilia mkazo kwa kampuni shughuli za uchakataji madini kufanyika nchini.....
6. Sheria hizi pia zimebainisha wazi kwamba rasilimali madini ni mali ya taifa yatasimamiwa na serikali kwa niaba ya Wananchi, kinyume na ilivyokuwa hapo awali ambapo hakuna sheria iliyokuwa imeweka wazi umiliki wa Madini kwa Taifa...
Sheria Mpya ya Madini pia imetungiwa kanuni na wizara kanuni hizi mpya ambazo, zinatoa kipaumbele si tu kwa taasisi za fedha na huduma za kisheria za Kitanzania lakini pia ajira kwa Watanzania....
7. Kuhusiana na huduma za kifedha, kanuni mpya zinataka makampuni ya madini kufungua akaunti na kuweka fedha zao katika benki za wazawa.
"Benki ya wazawa ni ile inayomilikuwa na wazawa kwa asilimia 100 ama ile ambayo Watanzania wanamiliki hisa nyingi zaidi", mfano CRDB, NMB, DCB, POSTA BANK, n.k
Hii inaziengua benki kadhaa za kigeni kufanya biashara katika sekta ya madini. Baadhi ya benki za kigeni zinazofanya kazi nchini ni pamoja na Stanbic, Barclays, Standard Chartered na ile ya Afrika Kusini ya First National Bank (FNB), KCB n.k
8. Kanuni zinataka pia utoaji wa leseni za uchimbaji madini utoe kipaumbele kwa kampuni za kizawa....
9. Kanuni za Sheria mpya ya Madini zinaelekeza kuwa huduma za chakula na Ulinzi kwa mgodi wowote zinapaswa kutolewa na Watanzania kwa Asilimia 100% na hili wanufaika wakubwa ni sisi Vijana wa kitanzania kanuni inasema itakapobidi kampuni ya kigeni inaweza kutoa huduma hizo lakini ni lazima iingie ubia na Mtanzania....
10. Kanuni mpya pia zinataka, mwenye leseni anapaswa kuwasilisha mpango wake wa utoaji huduma kwa jamii (CSR) kwenye Halmashauri husika ili iuthibitishe mpango huo kabla ya Utekelezaji wake. Tofauti na huko nyuma Utaratibu uliokuwepo wa kampuni ya Madini inajifungia ofisini yenyewe, inakuja na mpango wa kuwajengea shule pasipo Serikali ya kijiji au Wilaya kujua huo utaratibu mfu umefutwa na kanuni hii...
11. Kanuni zinaelekeza kuwepo ajira za staha kwenye Migodi (Decent work) wanufaika wakubwa na hili ni Vijana, pamoja na faida nyingine nyingi zaidi zilizomo kwenye Sheria mpya ya Madini na kanuni zake hizi ni sehemu tu ya faida zilizomo ndani....
Vijana wa Tanzania tuna kila sababu ya kujivunia Rais wetu John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo sisi wenyewe tutakuwa wanufaika wa juhudi anazozifanya na vizazi vyetu vijavyo, tuendelee kumuombea Mwenyezi Mungu ampe nguvu Zaidi ili akamilishe Maono yake ya Kuijenga Tanzania Mpya....
Fahami Matsawili.
Mjumbe Wa Baraza kuu Uvccm Taifa.