Barua" fupi" kwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Magufuli

Kila mmoja ana uhuru wa kutoa mawazo yake ila akipotosha hatuwezi kukaa kimya. Nakuhakikishia umemsingizia Baba wa Taifa huko alipo. Kwa wanao mfahamu Julius Kambarage Nyerere KAMWE ASINGEMUUNGA MKONO Magufuli kwa namna anavyoendesha nchi hususan katika mambo yafuatayo;
1. Utawala wa Sheria, kamwe Nyerere hajawahi kuingilia Uhuru Mahakama pamoja na kuwa alitawala kwenye mfumo wa Chama Kimoja

2. Kupendelea Maendeleo Wilaya yake, Nyerere aliingalia Tanzania nzima kwa uzito ulio sawa katika miaka 25 aliyotawala hata barabara lami Butiama ilikuwa haijajengwa mpaka alipotoka. Huyu miaka 3 tu kapeleka Airport, Mbuga ya wanyama, Hospitai ya Mkoa na Uwanja wa mpira wa miguu uko mbioni

3. Kuua wakosoaji, Nyerere hakuwaua japo aliwaweka kizuizini kwa wakati fulani. Huyu kamuua Ben Saanane, Azory Gwanda, na kmashambulia Tundu Lissu kwa risasi

4. Kubambikiza wakosoaji kesi, wakosoaji kama akina Eric Kabendera, Tito Magoti, Mdude Chadema nk

5. Kuwanyanga'anya fedha matajiri , kama akina James Rgemalira kwa kisingizio cha Plea Bargaining

6. Ufujaji au Ufisadi. Huyu kwa miaka 4 CAG aligundua kuwa fedha zipatzo Tsh 2.4 Trilioni hajulikani ziko wapi

7. Vyama vya upinzani, Nyerere ndiye mwasisi wa vyama vingi na aliviunga mkono. Huyu anataka utawala wa KIDKTETA na hapendi vyama vya upizani kabisa

Nataja hayo machache tu ili kulinda hadhi ya Baba wa Taifa. Niko tayari kuwajibika kwa maneno yangu katika kutetea jina la Baba wa taifa ambalo linachafuliwa makusudi na Deogratias Mutungi
 
Nataja hayo machache tu ili kulinda hadhi ya Baba wa Taifa. Niko tayari kuwajibika kwa maneno yangu katika kutetea jina la Baba wa taifa ambalo linachafuliwa makusudi na @Deogratias Mutungi
Sijaelewa hoja yako ni ipi juu ya dhana ya tuhuma kwangu dhidi ya upotoshaji kwa Mwl. nimenyambua maoni yangu kadiri nionavyo falsafa Bora za Sasa dhidi ya maendeleo ya watu, Kosa liko wapi?
 
Tatizo ni kiongozi kichaa kuongoza wastaarabu
 
Nakushauri tu, bado kijana mdogo tafuta kazi ya kufanya.

Wapo manguli hapa JF kina Mayalla na msukuma mwenzake na bado kavutiwa hand break ndio sembuse Mutungi?
 
Ndugu Matola nia ya andiko langu ni utashi wa kimawazo na si uhitaji wa unachokifikria, Aidha Mayalla ni Mayalla na Mutungi ni Mutungi usituingize fikra tusizo kuwa nazo vichwani mwetu, Nikutakie heri ya Mwaka Mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…