Sijui kama huu sio utumiaji mbaya wa madaraka. Mh. Majaliwa ni waziri mkuu (nafasi ya kiserikali) na hana uongozi katika CCM (kama mwenyekiti msaidizi, katibu, mwenezi nk).
Kutumia rasilimali za taifa kufanya kampeni za chama si jambo sahihi. Mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa uchaguzi ndiye anayetekeleza takwa la chama cha siasa, huku akitarajiwa kuwa na usawa kwa wagombea wengine. Lakini kwa kuwa wengi hatuwazi nje ya box la siasa, hatuwezi kuona hili!!
Points nzuri kabisa za kufungulia shitaka baada ya uchaguzi!!