Barua kutoka kwa mume wa Florah Mbasha kwenda kwa mchungaji Gwajima

Barua kutoka kwa mume wa Florah Mbasha kwenda kwa mchungaji Gwajima

Naweka nafasi nitakuja baadae..................................................!
Nimepata point ya kwanza
===>Haya makanisa haya yenye wachungaji wa darasa la tatu yana kazi kweli,mwenye CV ya Guajaroor atuwekee hapa tuanze kazi.
 
Nimesoma hii barua hadi imenitoa macho,hakika nimekubali yale maneno yasemayo usimwamini binadamu yoyote zaidi ya mama yako.
Hawa jamaa sikufikiria kama wangefikia hapa,ila mwanamke amekuwa natamaa ya pesa za haraka.soon huyo Frola pesa zitamtokea puani.
Emmanuel simama hadi upate haki yako,ila ningekuwa mimi huyo mwanamke ndiyo kwa heri.

mwanamke ana bebea mimba miezi tisa, anazaa anaweka mtoto kwenye rambo anatupa road/or choo cha shimo? bado huamini tu si wakuchezea?
 
eish!,hii barua si tayari ilishaletwa hapa na The bold via uzi mwingine?.mbasha na "masnura" yako, acha kujaza server ya jf kwa vitu ambavyo ulishavileta na wadau wakachangia.
 
Last edited by a moderator:
Palipo na ukweli uwongo hujitenga
 
Kweli Emanuel Mbasha umekwisha kabisa kabisa. Unadhani kuanika nguo zako za ndani kwenye kioo cha dala dala ndio zitakauka upesi? Huo sio msaada bali wajiletea aibu juu ya kichwa chako mwenyewe. Yupo muimbaji mmoja wa Bongo fleva aliimba akasema "Kuchapiwa ni siri ya ndani" weye sio wa kwanza kunyang'anywa mke.
Malalamiko yako kuwa ukifungwa watoto watapata taabu hayo ni mawazo finyu saana. Kulalamika kwako kuwa Flora kaupata utajiri wa haraka nayo yaonesha ulivyoshindwa kumtunza wenzako wakaonesha kuwa hukumstahili. Ulikuwa unamvua nguo bureee ati ni mali yako, wenzako wakamfungua macho kuwa anastahili kutuzwa, kila siku anapewa mamilioni. Weye unapoenda kuchunguza ati zimetoka wapi, nani kazideposit ni ili iweje?
Emanuel, usipojiangalia, siku si nyingi utaokota makopo. Wadhani unapambana na Gwajima kumbe wajitia wendawazimu mwenyewe.
Ushauri wangu; Mwachie Mungu yule uliyesema alikuokoa. Yeye ndiye atakupa uwezo wa kumsahau Flora na maisha yataenda mbele tuu. Si lazima ule jasho la mkeo. Jitafutie taratibu, utapata tu kwani rizki hugawa na Mungu si Gwajima wala Flora.
Huoni ajabu, wote wawili wamekudharau wala hakuna anaye bishana na weye humu JF?? Pole Bro. Angalia mbele, mlilie huyo shem, akuhurumie tuuu usiende Segerea. Ninavyomfaham yule ni mama huruma tu ukimtumia ujumbe mzuri, atakusamehe na kesi itafutwa.
Kama miye ni weye, huo ukoo ningeusahau kabisa mpaka hata mkoa wao nisingelifika huko tena. Kwa heri acha kulalama humu JF unajiaibisha sana. Yaonesha bila Flora hata ch.oo huendi
 
Tuliona Hii barua Jana; hata hivyo pamoja na maneno makali ya hisia bwana mbasha umeshindwa kuthibitisha kama mke wako anatembea Na Mchungaji mbali ya kuishia kwenye hisia.

Mfano; mkeo kurudi hotelini kwake Na taxi usiku Wa manane si uthibitisho Wa kuchukuliwa Na Mchungaji.

Na tunavyojua huko Morogoro walikuwepo wachungaji wengi Na hata mke Wa Mchungaji alikuwepo Na akilala chumba kimoja Na muwewe.
 
Huyu Mbasha anachachawa nini kwenye media kila siku?Ajibu hoja za kubaka,tunataka tusikie akijenga hoja za kuonyesha na kutuaminisha kuwa hajabaka,ye kila siku Gwajima!Gwajima!Anajidhalilisha tu sio sifa mtoto wa kiume kulalamikalalamika kuchapiwa mkeo unajidharaulisha chukua sheria kiunoni na wewe tafuta pesa usichapiwe,Huyo Flora ana uzuri gani mpaka wewe ufungwe kwa ajili yake does it make sense kweli?Acha kumtumia Gwajima kuonyesha watu unaonewa wenzako wamepeleka ushahidi polisi wewe tueleze kivipi hukubaka hao watoto bali unasingiziwa.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kweli Emanuel Mbasha umekwisha kabisa kabisa. Unadhani kuanika nguo zako za ndani kwenye kioo cha dala dala ndio zitakauka upesi? Huo sio msaada bali wajiletea aibu juu ya kichwa chako mwenyewe. Yupo muimbaji mmoja wa Bongo fleva aliimba akasema "Kuchapiwa ni siri ya ndani" weye sio wa kwanza kunyang'anywa mke.
Malalamiko yako kuwa ukifungwa watoto watapata taabu hayo ni mawazo finyu saana. Kulalamika kwako kuwa Flora kaupata utajiri wa haraka nayo yaonesha ulivyoshindwa kumtunza wenzako wakaonesha kuwa hukumstahili. Ulikuwa unamvua nguo bureee ati ni mali yako, wenzako wakamfungua macho kuwa anastahili kutuzwa, kila siku anapewa mamilioni. Weye unapoenda kuchunguza ati zimetoka wapi, nani kazideposit ni ili iweje?
Emanuel, usipojiangalia, siku si nyingi utaokota makopo. Wadhani unapambana na Gwajima kumbe wajitia wendawazimu mwenyewe.
Ushauri wangu; Mwachie Mungu yule uliyesema alikuokoa. Yeye ndiye atakupa uwezo wa kumsahau Flora na maisha yataenda mbele tuu. Si lazima ule jasho la mkeo. Jitafutie taratibu, utapata tu kwani rizki hugawa na Mungu si Gwajima wala Flora.
Huoni ajabu, wote wawili wamekudharau wala hakuna anaye bishana na weye humu JF?? Pole Bro. Angalia mbele, mlilie huyo shem, akuhurumie tuuu usiende Segerea. Ninavyomfaham yule ni mama huruma tu ukimtumia ujumbe mzuri, atakusamehe na kesi itafutwa.
Kama miye ni weye, huo ukoo ningeusahau kabisa mpaka hata mkoa wao nisingelifika huko tena. Kwa heri acha kulalama humu JF unajiaibisha sana. Yaonesha bila Flora hata ch.oo huendi

cc Ema Mbasha c/o the Bold! Aibu yako!
 
A great mind! Be blessed!
 
Kuna watu wana vichwa vya kufugia nywele tu
Sent from my RM-846_im_mea3_286 using Tapatalk
 
Naogopa sana ulokole. Bado sijajua kwenye mkutano wa CCM Dodoma kama Flora alitoka bila........
Hapo si ulokole ni tabia ya mtu . Pia ikumbukwe sana taarifa za mwanamke kwa wasomaji wa biblia, matukio mengi ya kuhatarisha amani yamesababishwa na mwanamke na mwanamke huyo huyo akaleta ukombozi. Na Mungu akaendelea kuwasihi wanaume wawapende wake zao lkn mwanamke aliambiwa amtii mume wake kwa sbb gani tafakari msomaji. Pia Mungu alisema kaeni kwa akili sana na hao wake zenu , sbb gani amesema hivyo jibu unalo. Bob Marley aliimba wimbo wa No woman no cry. Ukisikiliza ujumbe utapata picha ukiunganisha utamuelewa mwanamke kiumbe gani. Lkn watu wasisingizie ulokole .
 
Kweli Emanuel Mbasha umekwisha kabisa kabisa. Unadhani kuanika nguo zako za ndani kwenye kioo cha dala dala ndio zitakauka upesi? Huo sio msaada bali wajiletea aibu juu ya kichwa chako mwenyewe. Yupo muimbaji mmoja wa Bongo fleva aliimba akasema "Kuchapiwa ni siri ya ndani" weye sio wa kwanza kunyang'anywa mke.
Malalamiko yako kuwa ukifungwa watoto watapata taabu hayo ni mawazo finyu saana. Kulalamika kwako kuwa Flora kaupata utajiri wa haraka nayo yaonesha ulivyoshindwa kumtunza wenzako wakaonesha kuwa hukumstahili. Ulikuwa unamvua nguo bureee ati ni mali yako, wenzako wakamfungua macho kuwa anastahili kutuzwa, kila siku anapewa mamilioni. Weye unapoenda kuchunguza ati zimetoka wapi, nani kazideposit ni ili iweje?
Emanuel, usipojiangalia, siku si nyingi utaokota makopo. Wadhani unapambana na Gwajima kumbe wajitia wendawazimu mwenyewe.
Ushauri wangu; Mwachie Mungu yule uliyesema alikuokoa. Yeye ndiye atakupa uwezo wa kumsahau Flora na maisha yataenda mbele tuu. Si lazima ule jasho la mkeo. Jitafutie taratibu, utapata tu kwani rizki hugawa na Mungu si Gwajima wala Flora.
Huoni ajabu, wote wawili wamekudharau wala hakuna anaye bishana na weye humu JF?? Pole Bro. Angalia mbele, mlilie huyo shem, akuhurumie tuuu usiende Segerea. Ninavyomfaham yule ni mama huruma tu ukimtumia ujumbe mzuri, atakusamehe na kesi itafutwa.
Kama miye ni weye, huo ukoo ningeusahau kabisa mpaka hata mkoa wao nisingelifika huko tena. Kwa heri acha kulalama humu JF unajiaibisha sana. Yaonesha bila Flora hata ch.oo huendi

Wewe ni Flora au ndugu wa upande wa akina Flora
 
Walokole wengi ni wanafiki na waizi wakubwa wanatumia ulokole kama mwamvuli na wanakera sana ukiwaoba wenyewe wakinena utasema roho mtakatifu amewashukia kumbe ni fiksi tu wamekremisha maneno ooo shabarabara Katika Katika shantakakuntakintr kintoshabalalata labaaskrimu za azamtamu.... Wiziii mtupppuu
 
BONGOLALA vitu serious kama hivi vinahitaji strong verifications.
Kama hautajali utuambie imepatikana wapi?
Halafu kuna mtu ana contact ya Emma? FB au email or whatever?
Nina neno nae!
 
Last edited by a moderator:
Walokole wengi ni wanafiki na waizi wakubwa wanatumia ulokole kama mwamvuli na wanakera sana ukiwaoba wenyewe wakinena utasema roho mtakatifu amewashukia kumbe ni fiksi tu wamekremisha maneno ooo shabarabara Katika Katika shantakakuntakintr kintoshabalalata labaaskrimu za azamtamu.... Wiziii mtupppuu
We nawe!
Hakuna mlokole mwizi, ila kuna wezi wanajifanya walokole.
 
yusuph mhoja

the mbasha crisis episode iii: Bonge la movie, hebu icheki hapa;

barua kutoka kwa mume wa flora mbasha kwenda kwa mchungaji gwajima

"mchungaji ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwako.

Mchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!

Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya mwanamapinduzi foundation ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi maximilian machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??

Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!

Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia nashera hotel maeneo ya forest hill!!

Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!

Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!

Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!

Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... Na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa nitakushinda! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, i will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!

Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako how did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda

yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!

Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu fedha au huyo mchungaji mwanamazingaombwe

hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii ni nini kilichokuoata mkewangu??

Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!

Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili tanzania, na tusipotubu tukajirudi mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!

Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!

Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!

Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!

Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!

Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!

Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!

Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."

duh! Hii kali mazee, lkn endelea kutiririka mzeiya tumechuka na hawa wachungaji feki kumbe mafisi
.....gwajima ashindwe na alegee katika jina la yesuuu
 
Back
Top Bottom