Father of All
JF-Expert Member
- May 30, 2026
- 458
- 843
Makamu wa rais aliyelazimika kujiuzulu akadai kajiuliza mwenyewe Emaruel Nchimbi,
Japo umeondoka kimya kimya, umeacha kelele kila mahari.
Japo, umesema kuwa umeachia ngazi na si kuachiswa madaraka au tuseme kutemeshwa bungo, umeacha kitendawili ambacho anayeweza kukitegua ni wewe ama rais mama.
Umesema eti umejiuzulu kumpa nafasi rais ya kufanya mabadililko. Mabadiliko yapi? Je wewe ulikuwa kikwazo cha mabadiliko au ulitaka mabadiliko ya. mabadiliko asiyoyataka rais au utitaka kumbadilisha kabla ya kukubadilisha?
Hadi sasa, sijui hayo mabadiliko, kama kweli ndiyo sababu ya kujiuzulu si mabadiliko ya kawaida tuyajuayo bali mengine mengi.
Najikuta nikimkumbuka Humphrey Polepole aliyepolepolewa hadi sasa asijulikane kama yu hai au marehemu.
Sasa rasmi umetema bunge hata kama umetemeshwa, nakusihi kijana wangu usiende kupayukapayuka kama alivyofanya Polepole hadi akakolimbiwa kwa wanaojua kilichomtokea Horace Kolimba Katibu wa zamani wa CCM aliyeuawa kule Dodoma.
Zama hizi siyo zile za. zama japo hata zama mambo ya kutoana roho kulikuwapo ndiyo maana kuna misamiati ya kukolimbiwa kwa wale tulizaliwa zamani. Hakuna kilichonifurahisha kama CCM kuanza kukatuana nyinyi kwa nyinyi.
Kwa ufupi, nenda kimyakimya uishi kuliko kuamua ngangari kama Polepole wakakupolepole aka kukolimbiwa.