Mpingamkoloni
Member
- Feb 14, 2021
- 13
- 33
Mheshimiwa Rais!
Mimi ni mwananchi wa kawaida sana hapa Tanzania. Mimi ni mwanachama mwaminifu wa CCM tokea enzi za siku za mwisho za TANU.
Mheshimiwa Rais, sitopoteza muda wangu kutaja mambo mema mengi uliyowafanyia watanzania, maana nitatumia siku nzima na hivyo barua yangu itakosa maana. Wote tunajua hatukukosea kukuweka kwenye kiti cha Urais.
Mheshimiwa Rais, nimeamua kuandika barua kupitia mtandao huu, mara baada ya kukosa namna ya kuwasiliana nawe. Naamini hata kama hutosoma ujumbe huu, basi vyombo vyako makini kwa namna yeyote ile vitakufikishia ombi langu.
Mheshimiwa Rais, ninashukuru sana kwa kuwataka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenda kuanzisha shule ya afya mkoa jirani Mbeya. Kwetu sisi tuliopo nyanda za juu kusini ulitupa hamasa tosha hasa ukizingatia tulikuwa tumesahaulika sana kupata taasisi na miundo mbinu toka serikalini. Vyuo vyote vya afya vilikuwa vinakimbilia kanda za kuanzishwa Dar es Salaam.
Mheshimiwa Rais, mwaka jana nilibahatika kushiriki mahafali ya madaktari wa kwanza hapo Mbeya. Mjukuu wangu alikuwa miongoni mwa wahitimu wa kwanza wa kozi ya udaktari wa binadamu. Mahafali haya yaliongozwa na Mhe. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Mhemishiwa Rais, katika mahafali haya sehemu kubwa ya Hotuba ya Rais Mstaafu ilikuwa ni kuomba kupewa ardhi ili chuo kikuu cha Dar es salaam kijenge miundo mbinu yake ikiwa ni pamoja na hospitali kubwa. Mimi niliona ni jambo rahisi sana, kwa sababu limezungumzwa na Rais mstaafu lakini nasikia hadi niandikapo sasa bado halijafanyiwa kazi. Baada ya mahafali haya, mjukuu wangu alininong'oneza kwa kulalamika kwamba ameshangazwa kutosikia sifa za wao kuhitimu kutoelekezwa kwa hospitali ya Mbeya na madaktari bingwa wake waliowafundisha katika mazingira magumu, lakini sifa za kuwaivisha wao zilienda chuo kikuu.
Mjukuu wangu aliniambia, kwake yeye haoni mchango wa chuo kikuu cha dar es salaam zaidi ya kuwapa cheti kwani walikula na kushiba kwa kulishwa na hospitali ya Mbeya pamoja na madaktari wake bingwa ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa changamoto kubwa sambamba na kudharauliwa kama hawatoshi. Mheshimiwa Rais, binafsi sijui hata tone kuhusu elimu ya madaktari wa binadamu zaidi ya mifugo.
Mheshimiwa Rais, mimi nilikuwa miongoni mwa watumishi wa mwisho mwisho wa Tanganyika Packers Ltd (TPL). Ninajua Mbeya tulikuwa na ardhi kubwa kama sikosei basi ni takribani ekari elfu kumi. Nilisikia kwamba Chuo Kikuu waliomba sehemu ya hiyo ardhi na ati walikataliwa. Nimesikia karibuni kwamba Wizara ya Kilimo inataka ifuge ng'ombe na kwamba hiyo ndiyo sababu ya wao kukataa kuwapa chuo kikuu cha Dar es Salaam ardhi ili wajenge miundo mbinu yao. Nasikia chuo kilihitaji sehemu tu ya hilo shamba.
Mheshimiwa, Rais ninashangaa sana kusikia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimepewa maeneo madogo madogo ambayo yaliyo nje ya mji wa Mbeya huku ardhi kubwa ikihodhiwa na Wizara ya Kilimo kwa wa wazo la mradi mzuri ambao sidhani kama utaanza leo wala kesho. Sote tunajua huduma zinatakiwa na walaji walipo, na kama chuo kingepata ardhi kubwa ya Tanganyika packers ingekuwa rahisi huduma kubwa kama hospitali inayotarajiwa kujengwa kuwafikia wananchi, hasa tukizingatia kuwa Tanganyika Packers iko katikati ya Mbeya ambapo ni mjini sana. Kama sote tunafanya kazi kwa manufaa ya watanzania ilikuwa vyema kwa Wizara ya Kilimo kutoa sehemu ya eneo hilo kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wao wakatafuta ardhi ya kufuga nje ya mji.
Mhe. Rais, hilo ni ombi langu kuu.
Sambamba na hilo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapaswa kijikite kuboresha uwezo wa hospitali zilizopo nyanda za juu, ikiwepo ya Mbeya. Uwepo wa Chuo Kikuu chochote ulete tija na mabadiriko yanayoenda sambamba na huduma wanazotoa.
Mheshimiwa Rais, Chuo Kikuu kitambue umuhimu wa hospitali ya rufaa na madaktari bingwa walionao sasa ambao wamesomeshwa kwa gharama kubwa na serikali. Iwathamini. Isiwadharau. Iwasikilize. Iwape stahili zao kama malupulupu, vyeo na nafasi za kuwasomesha masomo ya juu zaidi.
Mheshimiwa Rais, Tunakuamini. Umejaa hekima.
Unajua ni maamuzi gani wapasa kuyafanya, ila huu ni ushauri tu.
Asante.
Mkoloma, Iringa