SoC02 Barua kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Stories of Change - 2022 Competition

Mdaka Mdaka

Member
Joined
Jul 23, 2022
Posts
5
Reaction score
4
Ilikuwa kwamiaka 23 au nazaidi sikumbuki, ninachokumbuka nikwamba ulifanya kila uwezalo kuipatia nchi uhuru, ukaweka jitihada kubwa za kuliunganisha Taifa na mwisho mikakati madhubuti yakuleta maendeleo. Mwalimu; uliwachukia maadui watatu waletao udhalili; umaskini, ujinga na maradhi. Ukaimarisha vijiji vya ujamaa navyama vya ushirika kukabili umaskini; Elimu ya kujitegemea uliipa kipaumbele ili Watanzania waweze kujitambua na kutokomeza ujinga. Huduma muhimu zajamii zilipewa nafasi ya kipekee kukabili maradhi na kurudisha utu wa Mtanzania ulioharibiwa na Wakoloni. Imani yako ilijengwa na tumaini la kesho itakuwa bora kuliko leo, ukiamini kama njia nisahihi umbali sitatizo.

Mwalimu; naumia sana kukwambia kuwa Watanzania sikuhizi tumekuwa kama Konokono, kutwa tunatembea namzigo washida. Leo kilakona nivilio kama chumba chauzazi, kusemakweli kwetu ni matusi, msimamo nikiburi, kutenda wema maranyingi nikejeri na dharau, wizi, ufisadi, rushwa na dhulma, nisehemu ya maishayetu. Mwalimu; nikweli kuwa kesho haifi na subira lengo lake kuu ni kuvutaheri, mbona kwetu ni kinyume? Kilasiku tumeishia kula wali mkavu pasi na kujali tumegaa-gaa kiwango gani kwenye mitaa ya Karume, Mbalizi, Nyegezi, Msalato, Ngaramtoni au Nangwanda Sijaona. Mbaya zaidi kunamuda hata huo wali mkavu hatupati.

Mwalimu; tunahitaji mapinduzi na maboresho katika nyanja za siasa na utawala, jamii, uchumi na teknolojia ndani ya Taifa letu, kwasababu huku ndikoziliko chemchem za uzima wetu.

1:> Maboresho ya kiutawala na kisiasa; Mwalimu, hakuna Nchi inayoweza kuendelea pasi na siasa safi na utawala bora utaowezesha usimamizi madhubuti wa rasilimali zake, nakwenyehilo taasisi imara ninyenzo muhimu sana. Mwalimu; taasisi zetu nidhaifu mno, kiasikwamba hazifanyikazi vile inapaswa bali zinafanyakazi vile mtu fulani anataka. Tunahitaji mapinduzi yakitaasisi na kimfumo;

a》Taasisi ya usimamizi wa uchaguzi(NEC) na usimamizi wa siasa (Ofisi ya Msajiri wa vyama). Mwalimu; uchaguzi unafanya demokrasia iwepo, viongozi wa kisiasa wanafanya demokrasia ifanye kazi, hata Robert Dahl(1971) na David Held(2006) wanaafiki hilo. niukweli uliokuwa wazi kuwa uchaguzi na siasa, ndio roho ya nchi yeyote ile ya kidemokrasia, bahatimbaya sikuhizi Tanzania hakunatena siasa safi wala uchaguzi bali ni siasa chafu na uchafuzi. NEC imekuwa tume ya chama na Serikali. Ofisi ya msajiri wa vyama, kaziyake nikuvibana vyama vyaupinzani ili zidumu fikra za mwenyekiti. Mwalimu; njia kuu ya kuboresha taasisi hizi ni kuzitenganisha na mhimili wa Serikali kwa njiazote ili ziwehuru kiutendaji. Zilindwe na ibara maalum ndani ya katiba na vifungu mbalimbali vya kisheria badala ya kutegemea huruma ya Rais.

b》Taasisi za uchunguzi na usalama. Mwalimu; taasisi zetu za uchunguzi kama TAKUKURU na nyingine zimekuwa kama gari la udongo, lisilofanya kazi nyakati za mvua. Zimekuwa kama kichwa cha Tembo, kikubwa lakini hakibebimzigo. Zimekuwa kama roboti, zinafanyakazi vile watu fulani wanataka. Nambaya zaidi zinaishi kwamisingi ya kwenyeuzia, penyezarupia. Jeshiletu la Polisi nnamashaka kuwa sasahivi wamekunywa maji ya bendera, nahuenda ukiwachanja damu zao nikijani. Mwalimu; lile ghala la AK-47 ulilowaachia halilindi tu mpaka kule Sirari, Mara bali pia kuwadhuru Wamasai wa Loliondo ili kupisha wageni kuwekeza. Kuwafukuza wamachinga wanaosakatonge mijini. Kuhakikisha katiba mpya haipatikani. Kuhakikisha wapinzani hawapumui, Mbowe anakaa sero kwakesi ya kubambikiziwa, Godbless Lema anatorokea ughaibuni kama mkimbizi wakisiasa na Zitto Kabwe anaishi kwa wasiwasi kule Ujiji, Kigoma. Mwalimu; katiba mpya yenye mfumo utaoviweka huru vyombo hivi kutoka kwenye minyororo na utumwa wa serikali, ndio mwarubaini.

c》Katiba mpya. Mwalimu; Malcom X aliwahi kusema, "kesho iliyokuwa bora, ipo kwawale waliojiandaanayo leo vyema". Mwalimu; kwadhati kabisa nikwambie siioni keshobora kwakatiba hii tuliyonayo sasa. Kwanza ilirithiwa kutoka ukoloni, pili ikabuniwa na kukarabatiwa nawatu wachache wachama kimoja cha TANU, tatu ikarekebishwa sehemu chache huku wakihakikisha maslahi ya chama chao chakijani yanalindwa ipasavyo kutokana na marekebisho hayo. Mwalimu; tunataka katiba mpya leo sio kesho. ¹Katiba tuliyonayo imetuondolea haki, tumebaki na uvumilivu. ²Imemfanya Rais kuwa Mungu na wafuasi wake kuwa Malaika watiifu. ³lmetufanya tuwe na mhimili mmoja kiutendaji namitatu kimaandishi. ⁴Imefanya tuishi ndani ya mfumowakiimra, huku demokrasia ikiimbwa kinadharia. Mwalimu; suluhisho la matatizo hayayote nikatiba mpya, itayoridhiwa na kuakisi maisha ya Watanzania wasasa na mfumo wa kidemokrasia tunaoutaka.

2:> Mapinduzi ya kijamii; Mwalimu, jamii yetu imeharibika kwakiwango kikubwa, yanayotokea kwenye jamiiyetu leo hayapendezi kwamungu wala machoni mwawatu. Maadili yameondoka, utu unaenda kuwa historia na ustaarabu unakaribia kukataroho. Mwalimu; sijajua kama ulisikia ya risasi saba za kichwa, guniambili za mkaa, Baba kambaka mtotowake au yule kakamatwa naviungo vya binadamu. ¹Mwalimu; leo kwetu wizi, rushwa, ufisadi na dhulma nisehemu muhimu ya maisha yetu. ²Mwalimu; leo hii Tanzania kunavijana wanaodai hakizao, haki za ndoa ya jinsiamoja. ³Mwalimu; leo hii kumbi za starehe na anasa ninyingi kuliko nyumba za ibada. ⁴Mwalimu; leo hii vijana wanasema bora uishiwe damu kuliko bando litalokuwezesha kuingia kwenye mitandao yakijamii kupata umbea, huko wanasema kuna-connection, wengine wanadai kuna-ubuyu. Mwalimu; hali ya jamii yetu nimbaya mno, tunahitaji mapinduzi makubwa yakijamii kwakufanya mengi, yakiwemo yafuatayo.

a》Matumizi mazuri ya nyumba za ibada. Misikiti na Makanisa yatumike kama nyenzo muhimu za kuchochea maadili na uadilifu katika jamiiyetu. Tusiishie ku-durusi hadithi za Sahihi Bukhari na Muslim kuelezea uzuri wapepo, pia tutumie aya nyingi za Qur-an kupinga wizi, rushwa, ufisadi, dhulma na maadili-ovu. Madhabahu yaendelee kutukumbusha Mithali(14:29-34), yaweke nguvukubwa kwenye Isaya(1:16-17), napia Polisi nao waelezwe Luka(3:14).

b》Malezi bora katika familia. Familia ziweke nguvukubwa kwenye kuwalea na kuwakuza watoto kwakuzingatia maadili yanayofaa namiiko ya jamii yetu. Pia tuwaandae watoto kuwa wazazi bora nasio bora-wazazi.

c》Adhabu za kijamii. Jamii iache kuwatukuza na kuwalea wezi, mafisadi, wahujumu na waovu, badala yake iwapeadhabu zakijamii kama kuwatenga na kufichua uovu wanaoufanya kwenye vyombo vya dola. Waovu wawe nimaadui wa umma, nasio marafiki wa jamii. Tunawezaiga kwa China na Japan.

3:>Mwalimu; nnamengi yakuongea kuhusu Uchumi na teknolojia sema muda hauruhusu, nikipata nafasi ntakuandikia barua nyingine nikujuzemengi juuyahayo.

Mwisho; naomba uwasalimie nduguzetu huko. Msalimie Sokoine, Lucy Lameck na Abdulwahid Sykes. Ukimwona Sitta, mwambie tunatamani arudi kuliongoza Bunge. Napia ukimwona Kwame Nkrumah mpesalamuzangu zadhati, mwambie Afrika bado hatujaungana. Kishamwambie leo Waafrika kitamaduni tumevurugwa, kijamii tumesambaratika, kisiasa tumedhoofika na kiuchumi halizetu mbaya kupindukia.

Wakikuuliza nani kaandika baruahii? Waambie nimimi kijana mzalendo, raiamwema, mwenye mapenzi yadhati kwa jamiiyangu. Wakikuulizatena nini lengo la baruahii? Waambie, ujenzi wa jamiimpya iliyobora.
 
Upvote 5
Ndugu msomaji unaombwa kupigia kura chapisho hili k

wa kubofya hiko kialama chakijani cha ^ chini ya post, pamoja na kutoa mchango wako juu ya Barua hii. Asante.
 
Back
Top Bottom