Barua kwa mwanangu - you are the reason, Benedikt

MAKULILO

Member
Joined
May 30, 2010
Posts
84
Reaction score
95
Wiki iliyopita, Ijumaa February 10 mwanangu wa kwanza, Benedikt Fulbright Makulilo alitimiza mwaka mmoja. Binafsi niliona kuachilia vitu kama keki na zawadi nyinginezo ndogondogo ambazo ni ngumu kukumbuka, nikaona ni vyema nimwandikie ujumbe/barua moja ndefu ambayo akikuwa akiisoma ataiweka katika kumbukumbu zake.

Barua yenyewe ni hii hapa: MICHUZI: hepi besdei ya kuzaliwa benedikt fulbright makulilo

Na hii itaendelea kuwa ni tamaduni yangu ktk kila birthday ya mwanangu/wanangu nitakuwa nawaandikia barua, hata kama nikiwa mzee. Binafsi sipendi kununua kadi na kuweka jina la mtu tu, napenda kutafuta ujumbe mwenyewe na kuuandika toka awali.

Nawatakiwa siku njema

MAKULILO
 
Brother Makulilo, kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kazi nzuri ya kujitole ambayo umekuwa ukiifanya, nikuambie tu inawezekana wakati mwingine hupati feedback ila scholarship tips zako zimesaidia wengi na wengi wamefanikiwa,Mungu akubariki sana mimi binafsi ni member ya blog yako hivyo nimekuwa nikipokea updates mbalimbali mara kwa mara na zinanisaidia sana.
Hongera pia kwa mwanao aliyefikisha mwaka mmoja, umenifundisha jambo kwa mwanangu ambaye sasa ana miezi 5, Mungu akimjalia kufikisha mwaka naye nitakuja na jambo ambalo ni innovative kama hilo lako.
Kila la kheri mkuu
 
Mzee wa real madrid salam zao huko Carlfornia na hbd kwa mwanao
 
nimekuwa impressed as a yummy mummy' kwa kweli nimeipenda na mimi nitatafuta urithi mzuri kwa my beautiful daughter ambayo itakuwa elimu bora na self awareness kama wazazi wote wangekuwa kama wewe tungefika mbali hata haya madivision zero yangepungua. wito wangu kwa wazazi na wazazi to be tuwape watoto wetu msingi bora.
 
........Hongera kwa kukuza, maneno ya barua yako ni mazuri sana. Ikiwezekana tunga kitabu kabisa.
 
What a lovely letter!!!!
Happy birthday Benedikt!
 
........Hongera kwa kukuza, maneno ya barua yako ni mazuri sana. Ikiwezekana tunga kitabu kabisa.

Asante sana Mdau pretty......nipo naandika kitabu. Kitabu cha kwanza ni cha scholarships kiitwacho SCHOLARSHIP OPPORTUNITIES IN AMERICA AND EUROPE: The Secret From Makulilo hiki kitakuwepo sokoni mwaka huu. Sikiliza book trailer yake hapa in Audio Format Scholarship Book - The Secret from Makulilo - YouTube

Mwakani nitaandika kitabu kingine kiitwachi HOW I CAME TO AMERICA Hiki kitakuwa ni MEMOIR moja matata, ambayo itazungumzia maisha yangu, nilianzaje mpaka kufika hapa, na jinsi ya ku-settle ughaibuni na kuwa wa msaada ktk jamii yako uliyotoka hata kama huishi huko.

Tupo pamoja

MAKULILO
 
kaka scholarship zipo bado?
happy birthday mwanao


Ndugu scholarships zipo za kumwaga. Just tembelea links zangu....weekend hii iliyopita nimeweka posts mpya kibao. Na nitaweka nyingi kabla ya Ijumaa hii.

Pia, ukitembelea jukwaa la elimu la hapa kwenye Jamii Forums huwa naweka baadhi ya makala ambazo nimechambua vitu muhimu vya scholarships...makala hizo pia unaweza kuzipata kwenye gazeti la Jamhuri huko...huwa kila Jumanne natoa makala za scholarships

MAKULILO
 

Hongera kaka, natumai utavitafsiri maana inglishi is not richabo ni moja ya changamoto zinazofanya tuogope kuomba maskolashipu hivyo labda nakala za kiswahili zitatufanya tuelewe vizuri na kugangamala kujifunza kimombo - natumai ulifuatilia huu mjadala kwenye hizi linki hapa chini kuhusu kwa nini wabongo tuko nyuma kuliko nchi zingine za kiafrika katika kutafuta hizo fursa:

UDADISI: Rethinking in Action: Scholarships - Where are Tanzanians (again)?

UDADISI: Rethinking in Action: From Frank: For TZ Students Seeking Scholarships
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…