Barua kwa Prof. Nabi: Nabi mwambie Mayele aache kutetema kwenye mashindano ya CAF.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kucheza na jukwaa kunaondoa umakini uwanjani, kunaongeza wasiwasi kama ukipoteza nafasi, ukipigwa chenga, timu ikichelewa kupata bao na ukifanyiwa substitution. Kutetema kunamfanya mayele ahitaji nafasi 6 ili atumie vizuri nafasi moja vizuri, hiyo sio sawa. kwa upande mwingine Phiri wa Simba anahitaji nafasi 3 tu ili atumie moja vizuri kwakuwa Phiri hachezi na jukwaa kama Mayele, Inonga na Morrison.

Makambo ni bora pia kwenye target, mwiingize uwanjani acheze dk 20 sio dk 4 za sasa. Wachezaji kama Nkane, Ambundo, Farid na mauya ni wachezaji hatari sana wasioonekana kwenye mipango na maandalizi ya adui, watumie sana hawa vijana kama ukiona mambo yamekwama uwanjani, utaona matunda yake.
 
Mchezaji mwenye hat tricks mbili mfululizo kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika unawezaje kusema hajui kufunga?

Mchezaji mwenye uwezo wa kuifunga Simba kwenye mechi mbili mfululizo kwenye mechi ya ngao ya jamii utasemaje hajui kufunga?

Hakuna kocha duniani asiyetaka kuwa na mchezaji kama Mayele kwenye kikosi chake. Mchezaji anayeweza kufunga magoli ya kuipa ushindi timu yake mara kwa mara huku akiamsha vibe ya kushangiliwa uwanjani kila anapofunga, huyo ni mchezaji bora siku zote.
 
Kwan huwa anatetema wakati mchezo unaendelea, ushabiki kazi Sana ndugu zangu
 
Kucheza na jukwaa kunaondoa umakini uwanjani, kunaongeza wasiwasi kama ukipoteza nafasi, ukipigwa chenga, timu ikichelewa kupata bao na ukifanyiwa substitution. Kutetema kunamfanya mayele ahitaji nafasi 6 ili atumie vizuri nafasi moja vizuri, hiyo sio sawa. kwa upande mwingine Phiri wa Simba anahitaji nafasi 3 tu ili atumie moja vizuri kwakuwa Phiri hachezi na jukwaa kama Mayele, Inonga na Morrison.

Makambo ni bora pia kwenye target, mwiingize uwanjani acheze dk 20 sio dk 4 za sasa. Wachezaji kama Nkane, Ambundo, Farid na mauya ni wachezaji hatari sana wasioonekana kwenye mipango na maandalizi ya adui, watumie sana hawa vijana kama ukiona mambo yamekwama uwanjani, utaona matunda yake.
Mayelle anatetema hadi chooni, mwacheni apumuwe
 
Mayele hajui kucheza na jukwaa yeye ana cheza na Nyavu tu.
Hapana, sio kweli, wakongo ni watu wanaopenda watu na kusifiwa. Yaani wanataka misifa kinoma. Mayele anacheka na nyavu kweli lakini anakosa clear chance nyingi sana kabla ya kuzigeuza chache kuwa magoli. Hii inasababisha yeye na viungo wote kupanic na kusababisha viungo kujaribu kutaka kufunga wao wenyewe baada ya pasi zao nyingi kushindwa kugeuzwa na mayele kuwa magoli. ndio maana unaona akina Fei, Farid, Aziz, Moloko, Aucho, Sure boy, Djuma kila mtu anafikia wakati anataka kufunga mwenyewe hata kama hayuko kwenye sehemu safi ya kufunga.
 
Yaani mtu unakurupka na infinix lako kumshauri kocha mwenye leseni ya kufundisha timu zote duniani.
Aisee Mkurugenzi, acha unyanyapaa basi. Ufahamu fika wengi tumetoka kumuliki simu aina ya tecno miaka siyo mingi! Na sasa tumeji upgrade kwenye infinix!

Sasa unapoanza kutusimanga na hizi simu zetu za infinix, lengo lako nini hasa!! Tuuze ili tununue Iphone, au samsung!!!
 
Mchezaji mwenye hat tricks mbili mfululizo kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika unawezaje kusema hajui kufunga?

Mchezaji mwenye uwezo wa kuifunga Simba kwenye mechi mbili mfululizo kwenye mechi ya ngao ya jamii utasemaje hajui kufunga?

Hakuna kocha duniani asiyetaka kuwa na mchezaji kama Mayele kwenye kikosi chake. Mchezaji anayeweza kufunga magoli ya kuipa ushindi timu yake mara kwa mara huku akiamsha vibe ya kushangiliwa uwanjani kila anapofunga, huyo ni mchezaji bora siku zote.
kuna wakati unatakiwa uwasifu viungo wake kwa kumtengenezea nafasi nyingi mno kuliko uwezo wake wa kuzitumia. Kama yanga ingekuwa na mchezaji kama Moses Phili pale mbele huenda Zalan wangeoga magoli mengi sana. Hata ni lazima tuisifu zaidi safu ya kiungo kwa kutengeneza nafasi nyingi zinazopotea na zinazogeuka magoli.
 
Wew ni kocha au mchambuzi? maneno yote hayo usikute ni shabk maandazi tu ambaye hajui hata kupiga danadana.
 
Kucheza na jukwaa kunaondoa umakini uwanjani, kunaongeza wasiwasi kama ukipoteza nafasi, ukipigwa chenga, timu ikichelewa kupata bao na ukifanyiwa substitution. Kutetema kunamfanya mayele ahitaji nafasi 6 ili atumie vizuri nafasi moja vizuri, hiyo sio sawa. kwa upande mwingine Phiri wa Simba anahitaji nafasi 3 tu ili atumie moja vizuri kwakuwa Phiri hachezi na jukwaa kama Mayele, Inonga na Morrison.

Makambo ni bora pia kwenye target, mwiingize uwanjani acheze dk 20 sio dk 4 za sasa. Wachezaji kama Nkane, Ambundo, Farid na mauya ni wachezaji hatari sana wasioonekana kwenye mipango na maandalizi ya adui, watumie sana hawa vijana kama ukiona mambo yamekwama uwanjani, utaona matunda yake.
Una leseni gani?
 
Mayele kwa hii na itakayofuata kama watafanikiwa kupita ndio nitamuona mchezaje kweli,raundi hii ya kwanza beki atakazokutana nazo ni zenye akili nyingi sio zile alizozizoea hapa nyumbani
 
Katika hali kama hiyo anatakiwa mfungaji ambae akipatiwa nafasi 2 anaitumia moja kufunga goli. Usiwaze ukifunga goli utafanya nini na utapewa zawadi gani, tulia.
 
Mfano wa huyo striker ambae hakosi magoli ni yupi ?
 
Hakuna striker duniani ambae hakosi magoli lakini wanatoutiana viwango vya kukosa, Kuna kukosa magoli kwa kiwango Cha Halland, Messi Ronaldo, mbape, Mayele, Phiri, makambo, Mpole, Sopu, nk.
 
Back
Top Bottom