Barua kwa Rais Kikwete toka Musoma Vijijini

Barua kwa Rais Kikwete toka Musoma Vijijini

Nikupateje,
Nimekupata kweli kweli. Sasa tufanyeje ili tuweze kuadress matatizo ya Nyanja na Majita nzima? Nasema hivi kwa sababu kulalamika peke yake hakutoshi. Lazima tuangalie solutions na tutafute njia za kuzifikia hizo solutions. Mimi tangu familia yangu itoke Majita ni kitambo lakini bado naji- identify kama mtu wa huko. Kama kuna lolote tunaloweza kufanya individually and as a group naomba unihesabu kwenye kundi. Lakini pia ni upotofu kufikiria kuwa Kikwete anaweza kusaidia. Nendeni kwenye jimbo lake muone alifanya nini miaka yote aliyokuwa mbunge kule.
 
Wajita jipangeni basi kutafuta mtu, MJITA wenu ambaye anaubavu wa kushindana na Mhe. Nimrod Mukono. Tatizo ni kuongea sana YEGO MWAMBA lakini hakuna tija. Ila niwaonye jambo moja, TABIA YA UKABILA MLIYOIONYESHA wakati wa kampeni za mwaka 2005 ndiyo iliyowaponza. Wekeni ukabila pembeni na mshikamane kwa pamoja na Bw. Mukono. Si afadhali amewaletea mabati ya kuezekea shule, je ninyi mumeweka juhudi gani au mnadhani Mbunge ndiyo kila kitu yaani awaletee kila kitu nyie mmebweteka tu.

PUNGUZENI au ACHENI KABISA UKABILA WATU WA MUSOMA VIJIJINI.
 
kweli mkuu ukabila hafai na siku ukiingia kwenye hilo imbo mto utawaka. mimi nalijua vizuri jimbo lile.

lina tarafa ya kiagata yenye wakurya watupu na haijawahi kuwa na mbunge mkurya tangu uhuru! na wanalalamika ila wanasemea chinichini. kila uchauzi wajita kwa wingi wao huungana kumchagua mjita na au mzanaki kama ana ngawira kama mkono.

siku ukabila kianza, ile tarafa ya kiagata haitatawalka, watu wana hasira keli pale. tuombe Mungu
 
Nikupateje,
Nimekupata kweli kweli. Sasa tufanyeje ili tuweze kuadress matatizo ya Nyanja na Majita nzima? Nasema hivi kwa sababu kulalamika peke yake hakutoshi. Lazima tuangalie solutions na tutafute njia za kuzifikia hizo solutions. Mimi tangu familia yangu itoke Majita ni kitambo lakini bado naji- identify kama mtu wa huko. Kama kuna lolote tunaloweza kufanya individually and as a group naomba unihesabu kwenye kundi. Lakini pia ni upotofu kufikiria kuwa Kikwete anaweza kusaidia. Nendeni kwenye jimbo lake muone alifanya nini miaka yote aliyokuwa mbunge kule.

Mkuu Jasusi,
Nimedokeza kidogo kwamba kwanza tuachane na dhana kwamba kuna mtu ana mvua ya hela na kwamba ndiye Mkombozi. Ingekuwa ni mvua ya hela basi hiyo mvua angeinyesha Nyerere. Wala si Musoma tu, Mara yote ingekuwa kama London na hakuna mtu katika nchi hii angethubutu kutugusa. Fikiria kiwanja cha ndege kwake na Rais ni cha vumbi. Tena si kama miji mingine kiwanja cha Musoma kiko katikati ya mji. Ndege ya Nyerere ilikuwa ikitua kila mmoja aliijua hata muungurumo bila hata kuitizama. Hivyo kila mmoja alijifungia ndani kwa dakika kumi nzima ili vumbi liishe.

Unadhani matatizo kama hayo ama Nyerere hakuyaona au hawakumfikishia? Ni kwamba aliyajua hata kabla hajawa Rais na wana-musoma walijua hawawezi kunyenyekea mafisadi. Mimi kwanza lile jina Maregesi kwenye waliochota pesa za EPA linanitia kichefuchefu sijui angeingiaje Musoma enzi za Nyerere.

Kuhusu tufanyeje wala hatuna haja ya kuuliza sana. Nimesema jibu lipo. Mfano ni Tarime. Serikali nzima ilihamia Tarime wakaishia kuondoka siku moja kabla ya kutangaza matokeo. Unadhani huko Tarime Nimrod Mkono hakutia mkono wake kama lilivyo jina lake? Tena huko ndiko wamejaa wakurya wenzake. Musoma mjini au vijijini hauna wakurya. Kuna wajita, wasweta, wakyaya, waruri nk. Tarime imegeuka kuwa Halmashauri yenye mfano kwa Tanzania nzima. Inaongozwa na upinzani (CHADEMA) lakini mbinu za kuidumaza zimegonga ukuta na zitagonga ukuta siku zote.

Wana-musoma wakae na mkuu wao wa Mkoa waangalie nini cha kufanya. Walifanya kazi nzuri isiyosahaulika chini ya mkuu wa Mkoa aitwaye Isa Kaisi. Huyu alikuwa na utundu wake kuingia bungeni na jeans lakini ndiye mkuu wa mkoa pekee aliyeuweza mkoa wa Mara. Kaisi alikomesha biashara ya gongo kwa kuvaa bukta zake anaingia usiku mtaani kwenye vilabu vya gongo bila kufahamika na baada ya dakika tano wanakuja FFU kuwakamateni wote. Kumbuka kwamba Isa Kaisi hakuwa mjita au nini. Lakini alipendwa kupita kiasi.

Kumbuka Isa Kaisi alivyoshirikiana na wabunge wake Charles Chinuno Magoti na Abel Mwanga ule mwaka 1987 na kufumua mabomba ya maji mji mzima. Tulilalamika tukawa tunaoga maji ziwani kwani miezi sita maji hayakutoka lakini mtandao mpya wa maji ulipoanza kazi Musoma ikasahau tatizo la maji. Isa Kaisi na wabunge wake ndio waliishinikiza HESAWA ijikite kuchimba visima vya maji mpaka kule ziwani Igenge unakovuka kilometa tatu kutoka Nyegina.

Mafisadi walioitafuna nchi ndiyo hao walioiathiri Musoma. Samaki sangara ambaye Musoma hatumuiti "Sangara" tulimuita "Ichengu" au "Imbuta" ilikuwa ni Mkombozi kiuchumi na lishe. Vilipoanzishwa viwanda vya minofu ya samaki Musoma haikuepuka ufisadi huo. Jamaa alikuwa na kiwanda chake kinaitwa Madhara alijaribu kumiliki biashara hiyo sijui akaishia wapi lakini wanamusoma wakaishia kula mapanki mliyoyakana kwamba hamuyali kwenye hotuba zenu.

Cha msingi ni kwamba tunalijua tatizo letu. Tatizo la shule lilijulikana kabla hata ya mwaka 1980. Tuchague bila kuangalia itikadi ya chama tujali matatizo yetu. Hawa wenye mvua ya hela hawaijui Musoma vijijini. Unakumbuka ilitokea njaa Musoma vijijini wajita wakashindia maembe. Wakati huo ilikuwa enzi za Chama kimoja. Mbona hawakunyesha mvua zao za hela kipindi hicho au wanataka kutudanganya na wao mvua ziliwanyeshea siku hizi kutoka BOT.

Nina mwaka sijaenda Musoma. Lakini nasikia ile barabara ya kwenda Majita inayopita Chuo cha Maendeleo-Buhare inajengwa kwani nina taarifa kwamba nyumba za jamaa zangu zinabomolewa na watalipwa. Sijajua ni project ya nani na kwa nini au ndiyo mbinu zimeshaanza kwa ajili ya uchaguzi huu.

Wajita jipangeni basi kutafuta mtu, MJITA wenu ambaye anaubavu wa kushindana na Mhe. Nimrod Mukono. Tatizo ni kuongea sana YEGO MWAMBA lakini hakuna tija. Ila niwaonye jambo moja, TABIA YA UKABILA MLIYOIONYESHA wakati wa kampeni za mwaka 2005 ndiyo iliyowaponza. Wekeni ukabila pembeni na mshikamane kwa pamoja na Bw. Mukono. Si afadhali amewaletea mabati ya kuezekea shule, je ninyi mumeweka juhudi gani au mnadhani Mbunge ndiyo kila kitu yaani awaletee kila kitu nyie mmebweteka tu.
PUNGUZENI au ACHENI KABISA UKABILA WATU WA MUSOMA VIJIJINI.

Huyu Mzee Kibiongo ni kumuacha na kibiongo chake hajui anachokiongea na haijui Musoma. Wajita hawana ukabila. Wameongozwa na watu kama Herman Kirigini toka 1975 hadi 1985.

Unaposema waache ukabila basi unanipa picha kwamba Mkono anataka ifutike historia ya Majita ilivyojitutumua kivyake na aonekane bila yeye hakuna wanaloliweza. Mkono ni mtu wa juzijuzi tu hata mwenyewe alieleza kuwa siasa alikuwa chaguo lake alishinikizwa. Hivyo wakati hajafikiria siasa wenzake walifanya niliyoyaeleza. Ila juhudi zake kufuta historia zitaishia ukingoni kama zilivyoshindwa aliposirikiana na mabosi wake kuivuruga Tarime.

Unasema kaweka mabati ya shule. Hebu soma thread yangu nzima ujue shule zilianza kuwekwa lini. Mbona huyo Nimrod Mkono wako ameshindwa kuikumbuka hata Mwisenge Primary School shule aliyosoma Baba wa Taifa hili. Mwisenge imebaki gofu kama jirani yake Musoma Hotel. Hotel pekee nchini iliyoonja dhahma ya ubinafsishaji. Zingine zilipata mbia yenyewe inaishia kuota buibui na popo kuzaliana kana kwamba haikuwahi kuwa ya kitalii.

Kuna mtu kaleta wazo nalikubali kwamba lianzishwe jimbo jipya la uchaguzi liitwe MAJITA libebe kuanzia Nyegina, Mukirira, Mugango, Buruma, Kiriba, Busumi, Murangi, Bukima, Chumwi, Mabhui Merafuru, , Majita na iishie Muhoji. maanahapo ndipo unapoanza kuwapata wakurya.
 
Oneni nilichokuwa nasema kwenye hii attachment. Wana-Mara wa kata ya Manga wamejiunga na kujenga shule yao kivyao.

Picha hiyo ilitoka kwenye gazeti la Mwananchi, Januari 10, 2010, Ukurasa wa 7
 
Attachments

Kuna mtu kaleta wazo nalikubali kwamba lianzishwe jimbo jipya la uchaguzi liitwe MAJITA libebe kuanzia Nyegina, Mukirira, Mugango, Buruma, Kiriba, Busumi, Murangi, Bukima, Chumwi, Mabhui Merafuru, , Majita na iishie Muhoji. maanahapo ndipo unapoanza kuwapata wakurya.

Akina Wachasugu Wachamae kwa nini liitwe majita? ...Na Jimbo la Mwibara liitwe South Majita?
 
Back
Top Bottom