Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Andiko la Mussa Lugete kuhusu uwakilishi wa balozi mtarajiwa wa Rwanda nchini Tanzania laenda kimataifa na kunukuliwa katika mtandao tajwa :BARUA YA WAZI KWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR SAMIA SULUHU HASSAN KUHUSU KASHFA MBALIMBALI ZA BALOZI MTEULE WA RWANDA NCHINI TANZANIA GENERALI PATRICK NYAMVUMBA.
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan nakusalimu na kukupongeza kwa sababu tarehe 19/3/2024 utatimiza miaka mitatu madarakani tangu uchukue nchi baada ya kifo cha aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dr John Pombe Magufuli aliyefariki tarehe 17/3/2021. Ndugu Mheshimiwa Raisi namuomba Mungu akupe uvumilivu, ustahimilivu, busara, maarifa na nguvu za kuendelea kuwahudumia Watanzania zaidi ya milioni sitini na mbili ambao wanakutegemea ili kuwapeleka kwenye mafanikio.
Ndugu Mheshimiwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan naitwa Lugete Mussa Lugete mchambuzi wa siasa za Kimataifa, Mwanahistoria na Mwanamajumui wa Afrika. Ndugu Mheshimiwa Raisi ni utaratibu wangu kukuandikia barua za wazi pale ambapo naona kuna haja ya kufanya hivyo.
Ndugu Mheshimiwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan lengo la barua yangu ni kuweka pingamizi kwa serikali ya Rwanda kumteua Balozi mpya nchini Tanzania ambaye ni Generali Patrick Nyamvumba. Mimi sio Mtumishi wa umma wala mshauri wako naandika kama Mtanzania wa kawaida.
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan Jina la Patrick Nyamvumba sio ngeni katika medali za ujasusi na intelijensia barani Afrika.
Ndugu Mheshimiwa Raisi wote tunafahamu Kwamba wakati wa mauaji ya kimbari Rwanda kuanzia mwezi wa tatu mpaka mwezi wa Saba mwaka 1994 Patrick Nyamvumba aliongoza kikosi cha askari wa Kitutsi yaani Inkotanyi Amaraso kufanya mauaji ya Wahuti ambao tayali walikuwa wameonyesha kusalimu amri.
Ndugu Mheshimiwa Rais, baada ya kadhia ya mauaji ya kimbari Rwanda baadhi ya askari wa kihutu kutoka Rwanda walikimbilia Mashariki ya Kongo mikoa ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini hata hivyo serikali ya Rwanda iliunda kikosi cha Siri kikiongozwa na Patrick Nyamvumba na James Kabarebe kuwafuata na kuwaua huko Kongo.
Ndugu Mheshimiwa Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan. Kiufupi historia ya balozi mteule wa Rwanda nchini Tanzania Generali Patrick Nyamvumba imejaa ukakasi na sintofahamu kama ifuatavyo.
Duru za kijasusi zinaalifu Kwamba Patrick Nyamvumba alizaliwa mwaka 1967 nchini Rwanda kipindi cha uongozi wa Gregory Kayibanda ambaye alikuwa Raisi wa Kwanza wa Rwanda kuanza mwaka 1962 mpaka alipopinduliwa mwaka 1972 na Meja Generali Juvenile Habyalimana. Hata hivyo mwaka 1959 yalitokea mapinduzi ya Kihutu nchini Rwanda ambapo Watusti zaidi ya laki mbili walikimbilia Uganda na kupokelewa huko,huku wengine wakienda Mashariki ya Kongo na kujiita Banyamulenge na wengine walikuja Tanzania hasa mikoa ya Kigoma na Kagera.
Miaka ya 1980 Patrick Nyamvumba alitoroka kutoka Rwanda na kwenda Uganda wakati huo Generali Emmanuel Fred Gisa Rwigema alikuwa akikusanya wanyarwanda ili kuunda kikosi cha ukombozi wa Rwanda kutoka mikononi mwa Wahuti au Interahamwe . Mpango wa siri kati ya Kiongozi wa waasi nchini Uganda kipindi hicho Yoweri Kaguta Museveni na kiongozi wa Kitutsi nchini Uganda Emmanuel Fred Gisa Rwigema ilikuwa ni kuwatumia waasi wa Kitutsi nchini Uganda Ili kuingia Ikulu na kuuangusha utawala wa Milton Obote aliyeshinda uchaguzi wa mwaka 1980 baada ya kuanguka kwa utawala wa Generali Idi Amin Dada kufuatia Operesheni Chakaza iliyotekelezwa na serikali ya Tanzania.
Ndugu Mheshimiwa Raisi Dr Samia Suluhu Hassan, Raisi wa sasa wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni aliwatumia wakimbizi wa Kitutsi kwenda ikulu kufuatia vita vya msituni na mwaka 1987 Museveni aliapishwa Kuwa Raisi wa Uganda, mchakato wa Museveni kutimiza ahadi ya kuwarudisha wakimbizi wa Kitutsi Rwanda ukaanza ambapo tarehe 1/10/1990 Generali Emmanuel Fred Gisa Rwigema alivuka mpaka wa Uganda na askari 4000 kwenda Rwanda kupindua serikali ya Juvenile Habyalimana bahati mbaya Serikali ya Zaire chini ya Generali Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu Wa Zabanga iliunasa mpango huo na hali ikawa mbaya ambapo Generali Emmanuel Fred Gisa Rwigema ambapo alipigwa risasi katika mazingira ya ajabuajabu. Miongoni mwa askari waliokuwepo katika kikosi cha Rwigema ni Patrick Nyamvumba.
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Rwanda na Uganda wamekuwa vikwazo kwa muda mrefu katika kufikia amani nchini Kongo kwa sababu wanamaslahi mapana ikiwemo kupora madini na kusambaza silaha kwa makundi mbalimbali ya waasi kupitia Ziwa Kivu
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ikumbukwe Kwamba Laurent Desire Kabila alikuwa Tanzania kwa miaka mingi akipanga namna ya kumuondoa Madarakani Generali Joseph Desire Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu Wa Zabanga, Laurent Desire Kabila hakuwa na msaada mkubwa mpaka pale mwaka 1995 ambapo Rwanda na Uganda yaani Kagame na Museveni walivyokutana na Laurent Desire Kabila na kuunganisha nguvu za kumuondoa Madarakani Mobutu, katika hali isiyo ya Kawaida Laurent Desire Kabila akakubali kusaini mkataba wa Lemera mwaka 1996 mkataba huo ulikuwa na masharti kumi ,mosi Ikiwa Laurent Desire Kabila atakuwa Raisi wa Kongo lazima Kongo igawanywe Kuwa nchi mbili yaani kuzaliwa kwa taifa la Mashariki mwa Kongo lenye mikoa ya Kivu Kusini Bukavu na Kivu Kusini Goma.
Pili, Jeshi la Kongo linapaswa kujumuisha Watalaam kutoka Rwanda na Uganda,tatu Laurent Desire Kabila hapaswi kuamua jambo lolote kuhusu Banyamulenge bila kuomba ushauri kutoka serikali ya Rwanda na Uganda, nne Wakongomani wanaoishi mikoa ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini wanapaswa kuhamishwa Ili kupisha makazi ya Watusti kutoka Rwanda na Uganda yaani taifa la Banyamulenge. Tano Waasi wa kikundi cha Ukombozi wa Kongo wanapaswa kupewa Uraia Kongo ikiwemo haki ya kupiga kura. Sita Mpaka wa Rwanda na Kongo kupitia ziwa Kivu haupaswi kufungwa. Saba Ujenzi wa Reli kutoka Kongo kupitia Rwanda ,Uganda na Zambia Ili kukuza uchumi. Nane;Jeshi la Kongo litapata mafunzo kutoka Jeshi la Rwanda na Uganda. Tisa; Laurent Desire Kabila hapaswi kuomba ushauri kutoka serikali ya Tanzania bila kuwaambia Rwanda na Uganda. Kumi; Kongo inapaswa kupunguza uhusiano na serikali ya Ufaransa. Mwisho makubaliano ya mkataba wa Lemera ni Siri na hayapaswi kuvunjika .
Ndugu Mheshimiwa Raisi huo ndio mkataba wa Lemera unaitesa Kongo mpaka leo. Kwakuwa ndoto ya Laurent Desire Kabila ilikuwa ni kwenda ikulu kwa njia yeyote ikabidi akubali kusaini mkataba wa Lemera ndipo Rwanda na Uganda wakatengeneza Operesheni Banyamulenge kwenda kumuondoa Madarakani Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu Wa Zabanga na serikali ya Tanzania ilibariki mchakato mzima.
Mwaka 1997 Laurent Desire Kabila akaanza kutekeleza baadhi ya masharti ya mkataba wa Lemera kwa kukubali washauri wa mambo ya kijeshi kutoka Rwanda na Uganda mfano James Kabarebe kutoka Rwanda akateuliwa Kuwa mkuu wa majeshi ya Kongo,Bizimana Karaha kutoka Rwanda akawa waziri wa Mambo ya nje wa Kongo na Patrick Nyamvumba akawa idara ya ujasusi wa Kongo ikulu. Baadae Laurent Desire Kabila akawageuka Kagame na Museveni ndipo viongozi wa Rwanda na Uganda wakaondoka Kongo na kupanga mbinu za kumuua Raisi wa Kongo Laurent Desire Kabila kupitia Operesheni Kitona ambayo ilishindwa na serikali ya Rwanda na Uganda kupata aibu kubwa hata hivyo Laurent Desire Kabila aliuawa mwaka 2001 ikulu kwa kupigwa risasi .
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan Tanzania ni taifa huru ambalo tangu uhuru December mwaka 1961 limekuwa likijipambua kama kimbilio la wanyonge na kiboko ya madhalimu. Sio dhambi nikisema Kwamba Balozi mteule wa Rwanda nchini Tanzania Generali Patrick Nyamvumba ni dhalimu na hapaswi kuishi hapa Tanzania kwa sababu ameua watu wengi na kuhujumu amani na ustawi wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kuanzia mwaka 2013 hadi 2019 Generali Patrick Nyamvumba aliteuliwa Kuwa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda. Kabla ya hapo kuanzia mwaka 2009 hadi 2013, alitumikia Sudan kama Kamanda wa Kikosi cha Umoja wa Afrika-Umoja wa Mataifa huko Darfur (UNAMID). Ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Nigeria, Nyamvumba hapo awali alitumikia RDF kama kamanda wa vikosi vya ardhini, Kamanda wa Chuo cha Kijeshi cha Rwanda huko Nyakinama, Wilaya ya Musanze, Rais wa Mahakama ya Kijeshi ya Juu (2007-2009), Mkuu wa Logistiki, na Mkuu wa Operesheni, Mpango, na Mafunzo (1998-1999).
Mashtaka ya jinai ya vita
Kama kiongozi wa Tawi la Mafunzo la Front Patriotiki ya Rwanda (RPF) wakati wa Vita vya Kisasi vya Rwanda, Nyamvumba inadaiwa aliongoza operesheni za kikundi cha mauaji ambapo raia wa Kihutu katika maeneo yaliyodhibitiwa na RPF walichinjwa. Wanajeshi wa Nyamvumba walivutia na kuua Wahutu katika mikutano. Baadhi yao walipigwa na kuuawa kwa bunduki au majembe na kutupwa katika Mto Akagera. Waathiriwa pia walipakizwa kwenye malori, kuchukuliwa Hifadhi ya Taifa ya Akagera na kuuawa huko, kabla ya kuchomwa moto.
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2019 wakati Patrick Nyamvumba akiwa mkuu wa majeshi ya Rwanda serikali ya Tanzania ilipoteza zaidi ya askari 30 waliokuwa Kongo wakilinda amani kupitia vikosi vya Umoja wa Mataifa yaani MONUSCO.
Kuanzia mwaka 2017 Hadi mwaka 2019 askari 30 wa Tanzania walipoteza maisha Kongo,ni kipindi hicho ambapo Tanzania ilikuwa na uhusiano mzuri na Rwanda ambapo Raisi wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alikuwa swahiba na Raisi wa Rwanda dikteta Generali Paul Kagame Inkotanyi.
Ndugu Mheshimiwa Raisi Dr Samia Suluhu Hassan shambulio la mwaka 2017 ambapo Tanzania ilipoteza askari 12 halafu waasi wa ADF wenye asili ya Uganda kujitokeza hadharani na kusema wanahusika ulikuwa ni mpango wa kumzubaishi Raisi Magufuli na vyombo vya ulinzi na usalama,hata hivyo kumekuwa na biashara kati ya viongozi wa ADF na M23 Kwamba iwapo ADF wakishambulia askari wa Umoja wa Mataifa basi M23 watatoka mbele ya kadamnasi na kujipa uhusika vivyo hivyo M23 nao wakishambulia huwatuma ADF kujipa uhusika. Ikumbukwe Kwamba tarehe 22/2/2021 Balozi wa Italia nchini Kongo Luca Attanasio aliuawa katika mkoa wa Kivu Kaskazini mji wa Goma eneo la Rutshuru akiwa na maafisa wawili kutoka shirika la chakula Duniani, upelelezi uliofanywa na serikali ya Italia kwa ushirikiano na Shirika la Ujasusi la Hispania ulibaini Kwamba Waasi wa M23 kutoka Rwanda na wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda ndio waliohusika hata hivyo waasi wa FDLR walijitangaza kuhusika.
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2013_2019 Tanzania ilipoteza askari wengi Kongo kipindi ambacho Patrick Nyamvumba akiwa mkuu wa majeshi ya Rwanda na ndicho kipindi ambacho M23 ilikuwa ikipokea misaada ya silaha na mahitaji ya kijeshi kutoka Rwanda na mpaka Umoja wa Mataifa kupitia balaza la ulinzi na usalama kuitishia Rwanda kuiwekea vikwazo vya kiuchumi kama haitaacha kuwasaidia waasi wa M23.
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naomba uzuie ujio wa Balozi mteule wa Rwanda nchini Tanzania Generali Patrick Nyamvumba kwa maslahi mapana ya Tanzania na ustawi wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Ndugu Mheshimiwa Raisi Dr Samia Suluhu Hassan Nina mengi ya kuandika kuhusu balozi mteule wa Rwanda nchini Tanzania Generali Patrick Nyamvumba ila muda hautoshi Inshallah ukinipa mwaliko ntakuja ikulu kukueleza kwa kina. Ramadhan Karim.
Wako Mzalendo,Mtiifu na Mwanazuoni Lugete Mussa Lugete.
.
Asante.Nondo niliyonayo ni hiyo hiyo kuwa Nonsensical and absolutely Rubbish tu Mkuu.
Nakazia hoja. Kwani hakuna wengine wanaoweza hiyo kazi ni lazima awe yeye?Hapana, ila huyo akataliwe kwa sababu dhahiri kabisa, kwani lazima kumpokea?
Mkuu desa lote hilo lilivyoshiba ni Rubbish??😀 😀 😱Nonsensical and absolutely Rubbish!!
We utakuwa mtusiNonsensical and absolutely Rubbish!!
Kaa kwa umakini uzi huu utawagundua watusi ni kina nani, watapinga tuMkuu desa lote hilo lilivyoshiba ni Rubbish??😀 😀 😱
HakikaWe utakuwa mtusi
Ndio aje yeyote sio huyu mwenye damu za ndugu zetu wa JWTZ.Nakazia hoja. Kwani hakuna wengine wanaoweza hiyo kazi ni lazima awe yeye?
Serikali imstukie mapema.
Muhimu contents Mkuu, hata akicopy sawa tu. Wachambuzi pia wanasomaAndiko la Lutege laenda kimataifa na kunukuliwa katika mtandao tajwa :
Controversy Swirls as General Nyamvumba Nominated as Rwanda’s Ambassador to Tanzania.
March 16, 2024
By Adonis Byemelwa
View attachment 2937318
General Patrick Nyamvumba, the controversial nominee, assumes his role as Rwanda's Ambassador to Tanzania amidst mounting scrutiny. Photo/File.
The Tanzanian government's recent diplomatic maneuvers have ignited a storm of controversy and apprehension across the nation.
At the center of this maelstrom is the contentious nomination of General Patrick Nyamvumba as Rwanda's latest Ambassador to Tanzania.
Amid swirling allegations of grave misconduct in his homeland, this appointment has become a lightning rod for scrutiny and concern among citizens and analysts alike.
General Nyamvumba's background is shrouded in controversy, with allegations stemming from his involvement in the Rwandan genocide and subsequent military operations in neighboring Congo.
Reports suggest that during the Rwandan genocide from March to July 1994, Nyamvumba led troops accused of committing atrocities against civilians.
Furthermore, he has been linked to covert operations in Congo targeting Hutu soldiers who had fled Rwanda, raising questions about his suitability for a diplomatic role.
Intelligence sources indicate that Nyamvumba was born in 1967 in Rwanda and has a history of military involvement dating back to the 1980s. His trajectory includes collaboration with Ugandan forces led by President Yoweri Museveni and participation in military actions aimed at overthrowing regimes in Rwanda and Congo.
Concerns about General Nyamvumba's appointment extend beyond his alleged involvement in past atrocities. During his tenure as Chief of Staff of the Rwandan Army from 2013 to 2019, Tanzania reportedly suffered significant losses in soldiers serving under the United Nations peacekeeping forces (MONUSCO) in Congo.
Additionally, Nyamvumba's ties to armed rebel groups operating in the region, such as the ADF and M23, have raised fears of destabilization and violence.
The potential implications of hosting a diplomat with such a controversial background are significant. While diplomatic immunity shields individuals from prosecution in their host country, serious allegations of crimes can strain bilateral relations and undermine trust between nations.
The Vienna Convention on Diplomatic Relations, specifically in Article 9, outlines the procedure for declaring a diplomat "persona non grata" and requesting their departure from the host country.
According to this article, the receiving state has the right to declare any member of a diplomatic mission persona non grata at any time and without the need to justify.
Once declared persona non grata, the diplomat must leave the country within a reasonable period as determined by the receiving state. This provision serves as a mechanism for the host country to address situations where a diplomat's presence is deemed undesirable or contrary to the interests of the host nation.
Given the gravity of the allegations against General Nyamvumba and the potential consequences for Tanzania's reputation and security, experts are urging the government to exercise caution in its diplomatic appointments.
While maintaining diplomatic relations with Rwanda is important for regional stability and cooperation, prioritizing the integrity and values of the Tanzanian nation is paramount.
In light of these concerns, citizens and analysts are calling on the Tanzanian government to reconsider General Nyamvumba's appointment and conduct a thorough assessment of his suitability for the role of ambassador.
By upholding principles of accountability and transparency, Tanzania can demonstrate its commitment to justice and good governance on the international stage.
The delicate balance between diplomatic relations and moral responsibility is brought sharply into focus by the controversy surrounding General Patrick Nyamvumba's nomination as Rwanda's new Ambassador to Tanzania.
As the host country navigates its role in the global community, the appointment of an individual with a controversial past like General Nyamvumba raises significant concerns regarding the country's commitment to upholding principles of justice and accountability.
Renowned historian and Pan-African commentator, Mussa Lugete, known for his insightful analysis of African history and politics, has underscored the troubling implications of such appointments, emphasizing the need for Tanzania to prioritize the well-being and interests of its citizens in its diplomatic engagements.
Lugete captivated attention with a profound 1700-word opus, a fusion of article and advisory, shared on his Facebook platform, directed towards President Samia.
Within this composition, he eloquently illuminated the enduring impact of the Lemera agreement, a historical pact inked by former Congolese President Laurent Kabila, Rwanda, and Uganda. Lugete masterfully underscored how this pact continues to cast a shadow over the Congo, serving as a potent instrument wielded by Rwanda and Uganda to orchestrate strategic military interventions aimed at toppling the entrenched regime of President Mobutu Sese Seko.
Importantly, Lugete pointed out that Tanzania, historically committed to upholding justice and opposing oppression, played a role in blessing these interventions.
The appointment of General Patrick Nyamvumba as Rwanda's Ambassador to Tanzania has ignited a firestorm of controversy, with concerns raised about his alleged involvement in human rights abuses and regional instability.
Renowned historian and Pan-African commentator, Mussa Lugete, has highlighted the potential risks associated with such appointments, particularly in light of General Nyamvumba's tenure as Chief of Staff of the Rwandan Army from 2013 to 2019.
During this period, Tanzania reportedly lost over 30 soldiers serving in Congo under the United Nations peacekeeping forces, a situation exacerbated by rebel activities allegedly supported by the Rwandan government. Lugete's remarks underscore the strategic importance of Tanzania's relations with Rwanda, especially during the presidency of Dr. John Pombe Magufuli, and raise questions about the implications for Tanzania's security and regional stability.
President Paul Kagame's recent dismissal of calls to negotiate with the Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) adds another layer of complexity to the situation. Kagame's strong stance against engaging with the FDLR contrasts with Tanzania's President Jakaya Kikwete's suggestion for direct talks, further straining relations between the two neighboring countries.
Tanzania's refusal to apologize for Kikwete's remarks has sparked a diplomatic row, highlighting underlying tensions between Kagame and Kikwete. The FDLR remains a sensitive issue for Rwanda due to its role in the 1994 genocide and ongoing security threats, making any suggestion of negotiation contentious.
In light of these developments, President Samia Suluhu Hassan's relationship with former President Kikwete could prove instrumental in navigating the diplomatic challenges posed by General Nyamvumba's appointment. Seeking advice from Kikwete, who maintains influence and rapport with Kagame, may provide valuable insights as Tanzania evaluates its response to the situation.
As the Tanzanian government deliberates on the implications of General Nyamvumba's appointment, Lugete's warnings serve as a timely reminder of the need to prioritize national security and regional peace in diplomatic engagements. With tensions simmering between Rwanda and Tanzania, a delicate balancing act is required to safeguard Tanzania's interests while maintaining cordial relations with its neighbors.
Source : tovuti: panafricanvisions.com/2024/03/controversy-swirls-as-general-nyamvumba-nominated-as-rwandas-ambassador-to-tanzania/
Muhimu contents Mkuu, hata akicopy sawa tu. Wachambuzi pia wanasoma
Ahsante Mkuu, unaweza kutusaidia kutuwekea katika lugha yetu, tupate elimu zaidi wengine shule msingi. Kaka uta edit uweke kwa kiswahili itakuwa bora zaidi.Andiko kwa Lugha ya kiingereza limeweka mambo ya ziada mazito na kusomwa na jumuiya pana ya kimataifa.
Safi sana. Huyu ana mikono michafu -Damu za JWTZ na Ndugu zake wananchi wa Rwanda.Ndio aje yeyote sio huyu mwenye damu za ndugu zetu wa JWTZ.
Kama walikataa na sisi tumkatae, kwa heshma ya ndugu zetu wa JWTZ waliopoteza maisha huko DRC.Umesahau kuwa hao Rwanda wameshawahi kumkataa mzee Jack Zoka aliyepelekwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Rwanda?
Kwa sasa tumkatae kwa ndugu zetu wa JWTZ hao wa huko kwao Rwanda watajawabishana wenyewe kwa wenyewe.Safi sana. Huyu ana mikono michafu -Damu za JWTZ na Ndugu zake wananchi wa Rwanda.
Unapenda sana kujinasibisha na rwanda wakati tunakujua ni maamuma mmoja kutoka viunga vya kawe ukwamani..Nonsensical and absolutely Rubbish!!