A
Anonymous
Guest
Mhe. Waziri;
Tafadhali rejea mada tajwa hapo juu,
Kwa heshima na taadhima kubwa ninaomba kukuandikia nakuleta mbele yako maoni yangu binafsi na taarifa juu ya baadhiya masuala yanayojiri katika Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) hususani vitendo vya uvunjifu wa sheria za nchi, katibaya Kamati ya Olimpiki Tanzania sambamba na hali ya kukosautiifu wa kutekeleza maelekezo yanayotolewa na mamlakambalimbali za Serikali unaofanywa na Viongozi wa TOC waliopo Madarakani.
Mhe. Waziri, tunafahamu kuwa kwa uchache wao au kwakukosa uzoefu siyo rahisi watumishi na wataalam ulionaoWizarani au katika taasisi zako kufahamuau kung’amua kilalinalofanyika katika tasnia hii na kukufahamisha kwa usahihi.
Mhe Waziri, Mimi ni mwanariadha mstaafu, niliekua nakimbiambio za kilometer 42 na kuwahi kuiwakilisha nchi katikamashindano mbalimbali ikiwamo michezo ya Olimpiki yamajira ya joto ya mwaka 2016 yaliofanyika Jijini Rio Nchini Brazil.
Mhe Waziri, ninakuandikia Barua hii moja kwa moja baada yasiku za nyuma kuwahi kuandika Barua zingine nilizozielekezaBaraza la Michezo la Taifa (BMT) lakini sijasikia au kuarifiwajuu ya hatua zilizochukuliwa katika kurekebisha niliyoyaelezana kuondoa hali iliyopo.
Mhe Waziri, naomba nikutaarifu kuwa pamoja na uongozi huuuliopo madarakani sasa kutoleta mafanikio yoyote katikamichezo ya Olimpiki kwa zaidi ya miaka ishirini (20) ninapendakukujulisha kuwa uongozi huu umekua ukichezea katiba yaTOC karibu kila mwaka mmoja kuelekea mwaka wa uchaguzi. Kwa mfano tu, uchaguzi wa mwisho wa TOC uliofanyikaDesemba 2020 ulitanguliwa na marekebisho ya katibayaliofanyika Desemba 2019.
Baada ya kipindi cha uongozi cha miaka minne (4) kupita,uchaguzi mwingine ulitarajiwa kufanyika kwenye mkutanomkuu wa uchaguzi mnamo tarehe 14/12/2024 kabla ya zoezihilo kusitishwa na serikali kupitia msajili wa vyama na vilabuvya michezo nchini (msajili),
Kama kawaida yao, uchaguzi huu ulitanguliwa na marekebishoya Katiba yaliofanyika kupitia mkutano mkuu wa tarehe 09 Desemba 2023 na kuwasilishwa kwa Msajili mwezi Oktoba, 2024 ili kuidhinishwa na kuweza kutumika kabla ya tarehe14/12/2024.
Tunashukuru kuwa mchakato huu nao uliwezakusitishwa kutokana na tulichojulishwa kwamba serikaliilifatilia na kuona kuwa malalamiko ya wadau na wanachamawa TOC dhidi ya utaratibu wa marekebisho ya Katiba yaliofanywa katika mkutano na baada ya mkutano huo mkuu waTOC wa tarehe 09/12/2023 haukuzingatia taratibu za kikatiba nasheria za nchi.
Mhe. Waziri, Utaratibu huu wa kurekebisha katiba kabla yauchaguzi umekua ni utamaduni wa viongozi wa TOC tangumiaka ya 2000 baada ya viongozi wa sasa kuingia madarakanihali inayoleta hisia kwamba marekebisho ya katiba huwahayabebi maslahi mapana ya tasnia bali yanalengakuwatengenezea mazingira viongozi waliopo kuendelea kuwamadarakani kwa kuweka masharti yanayolenga kuwabana nakuzuia wengine wapya kugombea, hisia zangu hizi zinatokanana changamoto kadhaa za kikatiba ambazo nimezifuatilia zikijitokeza tangu katika mkutano mkuu wa Desemba 09/2023, ambazo ninaamini kama hazitaangaliwa vizuri changamotokama hizi zinaweza kuwa zinajitokeza katika kila mikutanomingine itakayofanyika kila mwaka mmoja kabla ya mwaka wauchaguzi mkuu wa TOC huko mbeleni na kusababishausumbufu mkubwa kwa wataalam na viongozi wa Serikali.
Mhe Waziri, Katika barua yangu hii nitajaribu kufafanua baadhiya changamoto za kikatiba kwa kipindi cha 2023-2024 na hasanitajikita katika katiba halali ya TOC iliopo sasa ambayo ni ileyenye marekebisho ya mwisho ya mwaka 2019.
1. Utaratibu wa kuitisha mkutano mkuu wa kawaida naUtaratibu wa marekebisho ya Katiba
2. Sifa za wanachama hai wa TOC
3. Utaratibu wa uteuzi na Sifa za wajumbe wa kamisheniya uchaguzi
4. Uaminifu wa viongozi wa TOC
1. Utaratibu wa Kuitisha mkutano Mkuu wa Kawaida na Utaratibu wa marekebisho ya Katiba
Mhe Waziri, Mnamo tarehe 09 Desemba 2023, TOC ilifanyamkutano mkuu wa mwaka pale Dodoma Hotel na mkutano huuulipaswa kuitishwa kwa notisi ya siku zisizopungua 30 ambayoilipaswa kuambatana na agenda na nyaraka zote zinazokusudiwakujadiliwa kwenye mkutano huo ikiwamo mapendekezo yamarekebisho ya katiba.
Kinyume na malekezo haya ya katiba, mapendekezo yamarekebisho ya katiba ya 09 Desemba 2023 yaliwasilishwa kwawanachama siku ya tarehe 04 Desemba 2023 (siku tano tukabla ya mkutano) na hivyo kukiuka matakwa ya katiba, nazaidi kuwanyima wajumbe wa Mkutano huo, ambao ni viongoziwa vyama shiriki vya TOC, muda wa kutosha kupitia nakutafakari na kuyawasilisha kwa wanachama na wadau waokwajili ya kuyajadili na kupata maoni ya Pamoja.
Mhe waziri, kutokana na kasoro hii rasimu ya katiba yenyemarekebisho ya 2023 ilijikita katika Mawazo na matakwa yaviongozi wachache walio madarakani.
Mhe. Waziri; mkutano mkuu wa uchaguzi wa 2024 uliitishwatarehe 04/11/2024 kwa kutumia katiba yenye marekebisho ya2023 yaliokua si ya halali kwa sababu wakati mkutano mkuuhuo wa kawaida na wa uchaguzi unatangazwa rasimu ya katibampya ya 2023 ilikua bado haijasajiliwa kwa msajili, Tunashukuru kwamba katiba mpya ilipogongwa muhuri waMsajili ikaonesha kuwa imepitishwa tarehe 26/11/2024 na ndipobaadhi ya wadau na wanachama wa TOC wakaona kumbeyaliyotangazwa tarehe 04/11/2024 yalikuwa ni kinyume nakatiba hiyo mpya, hivyo wakaona mchakato huo ulikuwa sihalali wakati unaanza.
Baadhi ya wanachama na wadau waliwasilisha mbele ya serikalikupitia msajili BMT, maoni ya kutoridhishwa kwao na jambohilo, na tunamshukuru msajili ambae baada ya kuona maoniyana mashiko tarehe 02/12/2024 alitoa maelekezo kwa niaba yaserikali ya kusitisha mchakato wa uchaguzi uliokusudiwakufanyika 14/12/2024.
Baada ya maelekezo ya serikali ya kuzuia uchaguzi wa 2024, TOC ilitangazia uma kufutwa kwa zoezi la uchaguzi na ilisogezambele mkutano wa kawaida kutoka tarehe 14/12/2024 iliokuaimepangwa awali, na kwenda tarehe 28/12/2024 ambayo ndiotarehe ya barua hii. Tulipowauliza wawakilishi wetu kwa ninimkutano huu umeitishwa wakati michakato ya uchaguzi nakatiba imesitishwa tukaambiwa kuwa utakuwa ni mkutano wakawaida tuu wa kusomeana taarifa za utekelezaji na mapato namatuimizi pasipo kuwepo kwa agenda za uchaguzi namarekebisho ya katiba.
Jana tarehe 27/12/2024 wajumbe wa Kamati ya Utendaji(exComm) ya TOC walikutana na Pamoja na menginewalitaarifiwa kuwa Msajili amesitisha kwa barua , mchakato wamarekebisho ya Katiba hadi baada ya uchaguzi ambaounatakiwa ufanyike kwa kuzingatia katiba ya yenye masharti yazamani. Sisi wadau tumeufurahia sana uamuzi wa Msajili natunaimani kuwa hatua hiyo italinda maslahi mapana yawanamichezo na kuwapa wadau wa TOC fursa ya kutoshakujadili marekebisho hayo kwa upana wake bila ya kuwa nambinyo (pressure) ya uchaguzi au visingizio vya maelekezokutoka IOC.
Mhe Waziri, Pamoja na kuwepo kwa maelekezo ya Msajiliyaliyotolewa kwa mujibu wa Sheria kwa barua ambayo TOC wamekiri kupokea na wamewaonesha wajumbe wao japohawakuisoma kwa sauti. Utaratibu wa kuitisha mkutano mkuuhususani marekebisho ya katiba au uchaguzi, kuna hitaji lakikatiba la kuwasilisha nyaraka na taarifa zote kwa wanachamasiku 30 kabla ya siku ya mkutano mkuu.
Tumesikitishwa kwamara nyingine tena kuona viongozi wa TOC wanakiuka katibakwani agenda za mkutano huu ziliwasilishwa kwawanachama siku ya tarehe 27 Desemba 2024 (siku moja kablaya mkutano) wengine kwa kupitia barua pepe na wengine kwakupewa walipowasili Dodoma Hotel wakati wa kujisajilikuhudhuria mkutano.
Aidha, kwa makusudi maelekezo ya Serikali yalikiukwa kwaninyaraka za mkutano zilipotoka zilionesha kuwa agenda namba 8ya agenda za mkutano mkuu huu ilikua ni kuhusu mapendekezoya marekebisho ya katiba ya TOC, kitendo ambacho kwa mara nyingine wameonesha kuto kuwa watiifu kwa serikali kwaniwanaendelea kuitisha mjadala ambao wameshaelekezwaufanyike baada ya uchaguzi, yaani usimamiwe na uongozi mpya utakaochaguliwa.
Hali hii inaonesha kama ilivyokuwa tarehe 9 Desemba 2023, agenda ya marekebisho haikuwa na muda wa kutosha na sasaleo wamerejea tena kulazimisha marekebisho yajadiliwe bilawajumbe kupewa muda wa kutosha, kinyume na alivyoelekezaMsajili.
Agenda hiyo ilikiuka utaratibu wa marekebisho yakatiba ulioelekezwa katika katiba. Kwa kifupi Kamati Tendaji imerudia makosa yale yale yaliyopelekea kusitishwa kwa zoezila uchaguzi wa 2024 na marekebisho ya katiba ya 2023.
Mhe. Waziri; Ni hisia zangu kua sekretarieti ilifanya kusudikusambaza ajenda za mkutano mkuu siku moja kabla ilikuwanyima wanachama wake na watanzania kwa ujumla hakiya kujua kile kinachoenda kubadilishwa kwenye katiba ya TOC na hivyo wajumbe kujikuta wanafikia maamuzi bila kua namaoni ya wadau wao wala uelewa wa kutosha kuhusumarekebisho yanayopendekezwa. Kwa ukiukwaji huu ni wazikua marekebisho yaliofanyika ni batili na hayapaswikutambuliwa.
Tunaomba ubatilishe au utoe maelekezo yako ilimsajili abatilishe hiki kilichojadiliwa leo na kuwapa adhabu kali viongozi waliokaidi maelekezo ya Msajili (serikali).
Tulichotegemea wao wafanye katika mkutano huu ni kutangazaupya kuanza kwa mchakato uchaguzi kwa kutumia katiba yazamani kama walivyoandikiwa, badala yake wameanzakuwatambia wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuwa waowanaheshima maelekezo ya IOC na siyo serikali au msajili nakwamba watahakikisha msajili anapoteza kazi kwa sababuanawazuiazuia na kusababisha IOC iifungie Tanzania.
Mhe. Waziri, tunaomba msajili asilegeze msimamo, wamemtegeamitego yao kwa kusingizia IOC lakini wanataka kupitishamatakwa yao binafsi badala ya kujali maslahi mapana ya sektaya michezo.
2. Uamuzi uliofanywa na mkutano siyo halali ,
Mhe Waziri, TOC ina aina tatu za wanachama ambao ni watubinafsi (Individual Members) wanachama wa heshima(honorary members) na wanachama wa uwakilishi(Representative members) sifa mojawapo ya mwanachama wauwakilishi ni lazima kwa mwanachama kuandaa michezo yakitaifa inayojulikana. Vilevile Ibara ya 6.1.3 ikisomwa na Ibara ya 13.0.4 inaeleza kuwa wanachama wa TOC watakaohesabikakwenye koram na kua na haki ya kupiga kura ni wale tuwanaotimiza wajibu wa mwanachama ikiwamo kuendeshashughuli za michezo inayotambulika.
Mhe waziri, Mkutano mkuu wa TOC wa 28 Desemba 2024 kama ilivyo kuwa ule wa 9 Desemba 2023 ulihudhuriwa nawawakilishi wa wanachama ambao hawatimizi wajibu wao kwakutofanya shughuli yoyote ya michezo kwa zaidi ya miaka 8 iliopita (kwa mfano………)na wenginetangu kujiunga kwao na TOC, kwa lugha rahisi wamekuawanachama kwaajili tu ya kuhudhuria mikutano ya TOC nakupiga kura kwa maslahi ya TOC badala ya kushiriki katikakuendeleza michezo.
Kwa mantiki hiyo, Mhe Waziri, shughulina maamuzmzi ya mkutano mkuu wa Desemba 28, 2024 nibatili na hayapaswi kutekelezwa ikiwamo marekebisho ya katibayaliopitishwa kwakua ilizuiliwa na Msajili na zimefanywa nawanachama wasio halali kikatiba.
3. Uteuzi na Sifa za wajumbe wa kamisheni ya uchaguziya TOC havijazingatia katiba,
Mhe Waziri, katiba ya 2020 inaelekeza kuwa kamisheni yauchaguzi itateuliwa/kuchaguliwa na mkutano mkuu wa kawaidakila mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi.
Wajumbe wa kamisheni ya Uchaguzi waliopo madarakani sasani wafuatao;
i. Ndugu Ibwahim Mkwawa
ii. Ndugu Khalfan Salim Omar
iii. Ndugu Malangwe Ally @ Mchungahela
Mhe Waziri, Kamati hii inahusisha wajumbe ambao baadhi bad oni watumishi wa Serikali lakini wanashiriki vitendo ambavyosisi wadau tunaviona viko kinyume hat ana matakwa ya Serikali, kwa kusaidiana na viongozi wa TOC wamekuwa sehemu yakutengeneza huu mgogoro na kukiuka sheria na Katiba zilizosajiliwa kisheria na kusababisha usumbufu kwa serikali -mwajiri wao.
Ukiachilia mbali mashaka yetu katika uadilifu wao, hoja yanguni kwamba utaratibu wa kuwapata wajumbe hawa waliotajwahaukufuata katiba kwani kama jinsi inavyoonekana katikaMuhtasari ambatishwa hakukua na uchaguzi wala uteuzi wawajumbe hawa uliofanywa na mkutano mkuu wa mwisho9/12/2023) kabla ya Mwaka wa uchaguzi (2024 ), bali kilichoponi Makamu wa Rais wa TOC kusoma tu majina ya wajumbe waKamati hiyo mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu na mara baada ya kuyasoma moja kwa moja ilifuata tukio la kuahirishwakwa Mkutano Mkuu saa 12:17 jioni bila kuwapigia kura.
Utaratibu huu umekiuka Ibara ya 17.0.1 na Ibara ya 13 za Katiba ya TOC zinazohusu utaratibu wa mkutano mkuukuteua/kuchagua wajumbe hao na siyo viongozi kuwateua. Kwa mantiki hiyo, wajumbe hawa wa Kamisheni ya Uchaguzi nibatili na hawapaswi kujihusisha na shughuli yoyote inayohusuuchaguzi wa TOC kwakua hawakuchaguliwa au kuteuliwa namkutano mkuu kwa mujibu wa Katiba, na wala majina yaohayakuwasilishwa kwa wanachama siku 30 kabla ya siku yamkutano ili wanachama na wadau wao wapate fursa yakuyachunguza kama wanafaa au la. Walipewa nafasi hizokirafiki kwa kuzingatia maslahi binafsi. na ndiyo maanawanashindwa kuwashuri kikamilifu juu ya kufuata katiba nasheria.
Mhe Waziri, kuhusu sifa za wajumbe watatu (3) wa Kamisheniya Uchaguzi kuna dosari kadhaa. Mjumbe mmojawapo wakamati hiyo ya uchaguzi ni Ndugu Ibrahim Mkwawa ,ambae nimtumishi wa Umma, ndiye mwenyekiti. Licha ya kuwahi kuwaMsajili wa Michezo chini ya BMT yeye bado ni sehemu yaSerikali inayoisimamia TOC hadi sasa.
Mjumbe huyu ni Mshauri wa Sheria wa TOC ambae ameteuliwana Kamati ya utendaji ya TOC kwa mujibu wa Ibara ya 28.3 yaKatiba. Aidha, aliteuliwa na Viongozi wa TOC kuwa mwandishimkuu wa rasimu ya katiba ambayo viongozi wa TOC wanalazimisha kuipitisha kwa ajili ya kulinda maslahi yao, hii I bila kuangalia kuwa viongozi hawa ndiyo waliotumia fedha nanafasi ya TOC kumsomesha nje ya nchi.
Hali hii inaleta mgongano wa kimaslahi (interest) na kimamlaka(authority) kwa yeye kua mjumbe na mwenyekiti wa kamisheniya uchaguzi ya TOC yenye wajibu wa kusimamia chaguzi za wajumbe wa kamati Tendaji wakati huo huo ni MwanasheriaMshauri wa TOC nafasi ambayo ni chini ya Sekretarieti ambayoni sehemu ya Kamati ya Utendaji Kwa nyadhifa hizo alizo nazo, ni rahisi sana kwa yeye kutokua huru na maamuzi yake pale yanapokinzana na maslahi ya viongozi hawa walio madarakanihadi sasa na ambao wanawania nafasi zinazopendekezwa katikakatiba mpya kuwa na mkate mnono zaidi ya awali. Kwa kuzingatia kuwa Wanagombea ndio waliomteua kushika nafasiya mwenyekiti wa uchaguzi na kuwa na kura ya turufu ikitokeakura za wajumbe wa Kamisheni hiyo kuwiana.
Mhe Waziri, kwakuwa taarifa za uhakika kwamba NduguIbrahim Mkwawa amefadhiliwa masomo yake ya Post Graduate Diploma na TOC, hili nalo ni wazi katika hali ya kiubinadamumaamuzi yake yanaweza kuathiriwa na hitaji lake la kulipafadhila kwa wajumbe wa kamati ya utendaji walioamuakumsomesha iwapo watakua wagombea wa uchaguziutakaosimamiwa na kamati yake.
Mhe Waziri, vile vile mjumbe mwingine wa Kamati yaUchaguzi ya TOC Ndugu Malangwe Ally Mchungahela (wakiliwa Serikali) ambaye naye aliwahi kuwa msajili wa Vyama vyaMichezo chini ya BMT na akaondolewa katika nafasi hiyo naWizara hii hii kwa kile kinachosemekana ni ukosefu wa maadili,hivyo kuwa mjumbe kwenye kamati ya uchaguzi katika TOC ni hatari kwa maslahi ya uchaguzi huru na wa haki.
Mhe waziri, pamoja na hayo hapo juu kuhusu mgongano wakimaslahi, naomba kukutaarifu kuwa kwa mujibu wa Ibara ya25.0 ya Katiba ya TOC (2019) TOC inawajibika kuunda bodimaalum ya rufaa, utatuzi na usuluhishi itakayowajibikakushughulikia na kutatua wa migogoro ya kimichezo au yakitaasisi itakayowasilishwa kwake na Mkutano Mkuu, Kamatiya Utendaji au Mwanachama wa TOC.
Licha ya Msajili kuelekeza kamati ya uchaguzi na rufaazitenganishwa , viongozi Viongozi walio madarakaniwamekuwa hawataki kufanya hivyo kwa kisingizio kwambaIOC na badala yake wanaitumia Kamisheni ileile ya uchaguzikusikiliza rufaa dhidi ya uamuzi wao wenyewe, katika hali hiiutatuzi na usuluhishi wa migogoro ikiwamo rufaa za uchaguzihauwezi kuwa huru na ni kinyume na sheria za nchi.
4. Uadilifu wa viongozi waliopo TOC.
Mhe Waziri, moja ya wajibu wa Wajumbe wa kamati ya utendajiya TOC ni kusimamia Katiba ya TOC wajibu ambao umevunjwana kamati hii kama nilivyoeleza kwa mifano hapo juu. Ukiachamifano hiyo Mhe Waziri, wajumbe hawa wamefikia hatua yakuwaghilibu wanachama wake, na kuihadaa serikali katikamchakato wa marekebisho ya katiba uliofanyika kuanziaDesemba 9 2023. Sababu za kusema hivi ni:-
Mnamo tarehe 4 Desemba 2023 kamati ya utendaji iliwasilishakwa wanachama wake Rasimu ya mapendekezo ya Marekebishoya Katiba ya 2023 kupitia barua pepe ikielekezwa kwawanachama wake kama sehemu ya maandalizi ya mkutanomkuu huo. Mapendekezo ya maeneno ya marekebisho ya katibayaliowasilishwa kupitia barua pepe hiyo, pamoja na yale yaliowasilishwa katika mkutano mkuu yalihusu maeneo matatu tu ya katiba ambayo ni,
(i) kutenganisha utawala na shughuli za utendaji,
(ii) kubadili nafasi ya katibu mkuu wa kuchaguliwa nakua afsa mtendaji mkuu wa kuajiriwa na
(iii)kuongeza idadi ya wajumbe wa kamati tendajikutoka watatu(3) kwenda watano(5) kila upande wamuungano.
Mhe Waziri, katika hali ya kughiribu wanachama wake nakuihadaa serikali kwa maslahi binafsi, baadhi ya viongozi waTOC iliwasilisha kwa msajili rasimu ya katiba kwaajili yakuidhinishwa kwa mujibu wa sheria wakimweleza kuwaimepitishwa na mkutano mkuu ikiwa na marekebisho kwenyemaeneo zaidi ya hayo niliotaja hapo juu. Moja na maeneoyaliyoongezwa na kuwasilishwa kwa msajili bila idhini yamkutano mkuu ni;
(i) sifa za wajumbe wanaogombea uongozi katika kamatitendaji kua mtu ambae hajawahi kuenguliwa katikauchaguzi wowote
(ii) Uongozi kukaa madarakani kwa miaka minne mara vipindi vitatu (4x3) yaani miaka 12,
(iii) Mtu wa miaka 75 kugombea urais,n.k
Mhe Waziri, kitendo hiki kililenga kumpotosha Msajili naserikali na kinaonyesha moja kwa moja viongozi wa TOC waliomadarakani wasivyoheshimu katiba na kukosa uaminifu hadikuchomeka vitu ambavyo wanachama waliowapa dhamana yakuongoza taasisi hii nyeti inayohusu michezo yote nchinihawakuwatuma.
Kwa matendo haya, ni wazi viongozi hawa waliangalia maslahiyao binafsi na kujiwekea mazingira ambayo wakiingiamadarakani yatawawezesha kufanya matakwa yao na simatakwa ya Tanzania. Kwa mantiki hiyo, wajumbe wa kamatitendaji wanakosa sifa za kushika nyadhifa walizonazo kwamujibu wa ibara ya 24.0.2 ya kua watu wenye nidham njema namwenendo mzuri katika jamii.
Aidha, wamekosa uadilifu na utiifu kwa serikali chini ya sheria na kanuni za michezo ambazo TOC ilisajiliwa kuzitii nakuzitekeleza. Kwakufanya hivyo wanastahili kuadhibiwa kwamujibu wa sheria.
Mhe Waziri, naomba kushauri kuwa wakati naiomba serikaliibatilisha yote yaliyofanyika katika mkutano mkuu wa leo tarehe 28/12/2024, naishauri pia ibatilishe uchaguzi mdogoulioendeshwa na Viongozi wa TOC kuchagua viongozi waKamisheni ya Wachezaji ndani ya TOC tarehe 8/12/2024 ambaomwanariadha nguli Alphonce Sin=mbu alienguliwa kwa hila kugombea nafasi hiyo kutokana na sababu za kuwa eti aliiasiTOC jambo ambalo tunajua ni uongo na ukweli wake nikwamba Makamu war ais wa TOC , ambaye tunashangaaalisimamiaje uchaguzi huo wakati yeye siyo kamati ya uchaguzi, alimuengua Simbu kwa sbabu za kuwa hayuko upande wake katika kampeni za uchaguzi mkuu wa TOC.
Vile vile, kwa kuzingatia amri ya Msajili ya tarehe 02/12.2024 uchaguzi huo pia ulipaswa kutofanyika kwakuwa katibainayotumika ni hiyohiyo moja iliyothibitika kuwa ilitumikakabla ya idhini. Hivyo basi uchaguzi wa Kamisheni yaWachezaji nao utangazwe upya sambamba na uchaguzi mkuuwa TOC.
5. Ombi binafsi,
Mhe Waziri, mwisho lakini si kwa umuhimu, naomba kuleta naupokee malalamiko yangu binafsi kudhurumiwa fursa yaudhamini inayotolewa kwa washiriki wa Olimpiki kila baada yaolimpiki kwa utaratibu uitwao Olympic Scholarship. Kamati yaOlympic ya Dunia kila baada ya michezo ya Olympic hutoaudhamini wa fedha kwaajili ya walioshiriki michezo hiyo ilikuwasaidia kujiandaa kwa michezo ijayo.
Mimi nikiwa mshiriki wa Rio Olimpiki 2016 sikupata fursa yaudhamini huu ambayo ninaamini ilikua haki yangu. Utaratibuhuu ulianza tangu mwaka 2009 na ninaamini wachezaji wote wakitanzania walioshiriki Olimpiki kabla ya Paris Olimpiki 2024 hawakupewa fedha hizi ambazo ni haki yao.
Mwaka 2022 niliandika barua BMT kulalamikia hilo na ikazaamatunda kwani kuanzia Septemba mwaka huo wanariadhawatatu walioshiriki Tokyo Olimpiki 2021 walipata fedha hizo za ufadhili kwa kiasi cha dola za marekani 1500 kwa mwezi mpakamwezi wa nane walipoenda kushiriki Olimpiki.
Ninaomba ofisi yako isaidie kujua ye fedha hizi za Olympic Scholarship kwa wachezaji kabla ya Septemba 2022 zilikuazikienda kwa kina nani? Ninajua kua kabala ya kuanzia mwaka2017-2020 kipindi cha baada ya Rio Olympic ambayo mimi nimmoja wa washiriki kiasi cha dola 20,000 zilitolewa kwa TOC ili zisaidie wachezaji kujiandaa na Olimpiki inayofuata.
Katika fedha hizi mimi sijapata hata cent moja basi ninaombakujua ni wachezaji gani waliopata. Pamoja na fedha hizi badokuna fedha zingine nyingi ambazo matumizi yake yanapawakuhojiwa.
Nimeambatanisha jedwali la report ya fedha ambazoTOC imepokea kwa miradi mbalimbali kwa hatua zakomuhimu.
Kwa heshima naomba kuwasilisha, wako mzalendo na mpendamichezo.
Pia soma:
~ Wanariadha wasusia Karatu Festivals baada ya Henry Tandau kumuita Alphonce Simbu Msaliti
~ Suleiman Nyambui asema hakufurahishwa jinsi kina Simbu walivyotoswa Airport