Barua nzito kwa walimu wa sekondari.....!

Barua nzito kwa walimu wa sekondari.....!

yamoyoni mwangu

Senior Member
Joined
Oct 25, 2013
Posts
106
Reaction score
31
Watanzania wenzangu hasa wadau wa elimu nchini habari zenu.......!

Awali ya yote nipende kumshukuru mwenyezi mungu muweza wa yote kwa kunijalia afya njema, amani moyoni ili kuwaandikia waraka huu wa TAHADHARI, ONYO na ILANI kwa walimu wangu wapendwa hapa nchini.... najua mnafanya kazi kubwa ya kuwafunza wadogo zetu maadili mema.... kwani binafsi naamini mwalimu ni mlezi na mzazi vijana wetu.... HONGERENI KWA HILI......

Najua tasinia ya elimu nchini imekumbwa na changamoto nyingi ambazo zinakwamisha jitihada za maendeleo ya elimu nchini kwetu... naomba nikiri wazi kuwa kazi mnayoifanya walimu wangu wapendwa ni ngumu na imegubikwa na changamoto nyingi... hasa kwa kizazi hiki cha dot com poleni...

Wapendwa walimu wangu najua next week vijana wetu kidato cha nne wanaaza mitihani yao ya mwisho.... nakumbuka kipindi nasoma mimi wakati kama huu kwangu ulikuwa mgum sana wenye kila aina ya changamoto nyiingi... walimu wangu wapendwa najua kuna baadhi yenu huitumia chance kufanya ufusika mkubwa kwa wanafunzi (hasa waschana) mnaitumia nafasi hii kuwadanganya madada zetu et wanamitihan ya necta hivyo wafanye juu chini wawaone.... baada ya muda wa kazi hasa usiku et muwasovie maswali ya mitihani hiyo... kumbukeni mwanafunzi yeyote anamwamini sana mwalimu wake hivyo mnajua lazima watakuja tuu... wakifika huko mnawapa masharit ya kufanyanao ngono kwanza et muwape hiyo pepa... hata wanaokubali kufanya hivyo mwisho wa siku nawapa mitihani feki na mwisho wake wanafel vibaya na kuongeza rundo la division 0 mtaani..

Nayasema haya kwa uchungu mwingi kwani ninayo mifano hai mingi tu ya kutoshaa.. kwa macho yangu nimeshuhudia mabinti wengi wakipewa mimba na walimu wao kwa suala hilohilo.... tena mbaya zaidi walipata division 0 wakati najua wazi msingewapa hayo matango pori wangefanya vizuri kwani walikuwa na uwezo mzuri darasani..... natoa ilani kwa walimu wangu najua hata mwaka huu mmejipanga kufanya hivyo hivyo..... asabuhi ya leo mdogo wangu wa kike amenipigia simu et mwalimu wake wa history amemwambia amtafute kuanzia saa 2 usiku kuna maelekezo muhimu anataka kumpatia na kumtishia et asipofanya hivyo lazima atafeli tuu... mimi nitaanza na mwalimu huyu kama mfano kwa wengine bahati nzuri namba yake ya simu ninayo, na ninamufahamu vizurii.... sasa kama kuna walimu wengine wa muundo huu... mjipange vinginevyo mtafia segerea.....

SINA MENGI ZAIDI YA UTEKELEZAJI WA NILCHOKISEMA
Ahsanten kwa kuisoma thread hiii.....
 
Ndo big results now hiyo wala usipanic au unataka mdogo wako afeli??
 
Wanafunzi wa kike Wanapata mimba kwa sababu ya viherehere vyao. Mr JK.

Ila ukichunguza kwa makini utagundua jambo kwenye kauli hii hasa mijini.!!
 
Ndo big results now hiyo wala usipanic au unataka mdogo wako afeli??


Bora afeli tu kuliko kufanya upuuzi huu..... akifaulu kimagumashi huko advance na chuo itakuwaje....... kama mungu amempangia kufaulu atafaulu tu haina haja ya kutoa mwili wake kwa jitu zima kama lile..... nana hasira naee lazima aniambie kama huko alikosoma ndivyo walivyo mfunda....... MSHENZI HUYU....
 
Wanafunzi wa kike Wanapata mimba kwa sababu ya viherehere vyao. Mr JK.

Ila ukichunguza kwa makini utagundua jambo kwenye kauli hii hasa mijini.!!

Iwe mjini ama kijijini lazima kieleweke tuu na huyu MSHENZ ataniambia tuu we ngoja nimuweke kwenye 18 zangu ameniudhi sanaa.... JITU ZIMA... KATOTO BADO KADOGO KALE MASIKINI....
 
hao watoto wa kike ni changamoto kwetu kwani wengi wao wanajilengesha wenyewe.wiki hii nimeambiwa I love u....xema wengi wetu tunajitambua na tunawapenzi wetu.huo utapeli wa pepa wanaambiwa wanafunzi wa vijijini.Tupo kwenye Big Results Now.usimlazie damu huyo kalagabao.

We ngoja tu nimtengenezee mazingira then atajuta kinifahamu.....
 
Tabia ya rushwa iko damuni kwa watz wengi, mpk mwalimu aombe match maana yake ameona huyo bint anaelekea. Tuwafunze watoto wetu ujasiri kama wazungu(baadhi), hilo ni kosa ambalo bint anatakiwa kuambiwa na yeye alisimamie. Hakuna mwl atamgusa bint mwenye msimamo
 
Jambo la msingi ni kuwaweka watoto wawe na ufahamu na stadi za maisha zitakazowasaidia kukabiliana na changamoto. Binti huyo ni muelewa ndo maana akaona alisema kwa wazazi. Hongera binti
 
Back
Top Bottom