Mnyalu Junior
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 573
- 199
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Ministry of Education and Vocaional Training) pamoja na Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prime Minister's Office Regional Administration & Local Government Authority (PMORALG) ni moja ya wizara nyeti hapa Tanzania.
Ni sekta nyeti kwani zinagusa masula mengi ya jamii ya watanzania hususani masuala ya Elimu na Watumishi mbalimbali wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Linapokuja suala la MAWASILIANO na hizi wizara ndo kizungumkuti kinatokea. Wametoa sehemu ya kutuma maoni au maswali wakitaka uandike jina lako, Barua pepe (Email adress) yako, kichwa cha maoni yako na hatimaye maoni mahsusi. Wametoa pia barua pepe zao (Email adress), Anuani ya posta na namba zao za simu lakini ufanisi wake ni DUNI sana!
Kulingana na ulimwengu wa utandawazi matumizi ya barua pepe na simu ndio yenye kurahisisha mawasiliano zaidi. Ukija kwenye suala la gharama na ukizingatia namba za simu walizoweka ni za simu za mezani na ukizingatia idadi kubwa ya Watanzania tunatumia simu za mkononi basi njia ya EMAIL ndo yenye urahisi zaidi.
Barua pepe (email) ya Wizara ya Elimu ni: psmoevt@moe.go.tz na
Barua pepe (email) ya Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ni: ps@pmoralg.go.tz.
CHA KUSHANGAZA Ukituma email kwenye hizi wizara HAZIFIKI! Utarudishiwa ripoti: "DERIVERED FAILED PERMANENTLY"
Hivi karibuni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetoa habari yenye kichwa:
"Waraka wa Elimu Na. 3 wa Mwaka 2015 Kuhusu
Vigezo vya Udahiliwa Wanafunzi wa
Kidato cha Tano" ( 303.36 kB)
Nikiwa kama mdau wa Elimu nilitaka kufungua hiyo link nijue vigezo vya udahili wa wanafunzi kidato cha tano mwaka huu wa 2015 ukizingatia wametoa matokeo kwa mfumo wa Grade Poin Average (GPA)
Baada ya kufungua na kudownload file waliloambatanisha nilishangazwa kukutana na BARUA tofauti kabisa! Barua hiyo ina kichwa kisemacho:
"WARAKA WA ELIMU Na1 WA MWAKA 2013 KUCHANGIA GHARAMA ZA UKAGUZI WA SHULE"
Ndipo nilipojaribu kufanya mawasiliano PASIPO MAFANIKIO kwa njia ya email kwa wizara ya Elimu kuwataka wachunguze vizuri faili waliloambatanisha (attachment) na km limewekwa bahati mbaya basi waliondoe na kuweka faili sahihi.
Kwa yeyote mwenye mawasiliano mbadala au mwenye barua pepe itakayowafikia kwa haraka ANISAIDIE!