Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
M-Tanzanaia mwenye phd, umri miaka karibu 60 aibu huko ughaibuni kufanya kazi MCDolnad, na kubangaiza bangaiza, nini kuogopa kurudi nyumbani?

kufagia fagia maofisi ya watu na kuja hapa kutukana watoto wa viongozi, aibuuuuuuuuuuuuuu!
 
Kama Adam Kigoma Malima anaharibu, kitu ambacho nakubaliana nacho asilimia mia moja ni wazi kuna umuhimu wa kuangalia kwa umakini suala zima la urithishaji nguvu za kisiasa (reduplication of elite) katika nchi yetu.

Ama unaesemaje Mzee ES?

Anyone wa kumsaidia Mzee Es the Senior in the House?
 
Wakitaka wakashitaki hata kwa shetani - Sitta
Asema hatishwi kufikishwa mbele kamati ya CCM

na Mwandishi Wetu

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, amesema hatishwi na hatua ya Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima (CCM), kuufikisha mgogoro aliouamua bungeni kati yake na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.

Malima aliamua kulifikisha suala hilo kwa Katikbu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Spika, aliyewaita ofisini kwake kwa ajili ya upatanishi.

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Sitta alisema hatishwi na hatua hiyo ya Malima na kwamba ni haki yake kama mwanachama wa CCM kuchukua hatua aliyoichukua, kama anaona ndiyo muafaka.

“Niliyatoa maamuzi yale kwa kujiamini. Sitishwi wala kubabaishwa, hata kama nitapelekwa kwa Makamba au kwa shetani,” alisema Sitta alipotakiwa na gazeti hili kutoa maoni yake kuhusiana na hatua za mbunge huyo.

Sitta alisema kuwa, anaamini ‘hukumu’ aliyoitoa ilikuwa ni sahihi na siku zote atasimama kuyatetea maamuzi yake. Alibainisha kuwa tayari amewaagiza maofisa wa Bunge kuweka katika maktaba ya Bunge nakala za kutosha za maamuzi yake, pamoja na ‘ansard’ za vikao vya Kamati ya Bunge ya Maadili, ambayo ilijadili tuhuma za Malima na Mengi.

Sitta alisema kwa kuwa anaamini alifanya maamuzi yale kwa kuzingatia sheria na kanuni, hana wasiwasi hata kama ataitwa na chombo kingine chochote kuyatetea maamuzi yake.

“Tangu nichaguliwe kuwa Spika, nimekuwa nikijitahidi kufuata kanuni na sheria kufanya shughuli zangu, sina wasiwasi kwani kila mara nahakikisha kuwa nafuata sheria na kanuni,” alisisitiza Sitta.

Hatua hiyo ya Sitta, inaweza kuonekana kuwa ni kujibu mapigo kwa wale wanaodaiwa kupanga njama za kutaka kuutumia mgogoro kati yake, Malima na Mengi, kumng’oa katika kiti cha uspika. Hatua ya Malima kuufikisha mgogoro huo kwa Makamba, iliwashangaza wengi, lakini ilikuja kubainishwa baadaye kuwa, kundi la watu fulani ndani ya CCM na serikali, wanautumia mgogoro huo kama kete yao dhidi ya Sitta kwa madai kuwa maamuzi yake, na jinsi anavyoliendesha Bunge, anakwamisha maslahi ya baadhi yao.

Aidha, inaaminika kuwa, hatua ya Malima kuamua kumkwepa Mwenyekiti wa wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Edward Lowassa, na katibu wa wabunge wa CCM, Ali Ameir Mohammed, ina lengo lililojificha la kumhujumu Sitta.

Uamuzi huo wa Malima kumshitaki Spika nje ya utaratibu wa Bunge, umetafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni kulidhalilisha Bunge kimamlaka. Wabunge kadhaa kutoka kambi zote mbili ndani ya Bunge, waliozungumza na gazeti hili, wameonyeshwa kushangazwa kwao na jinsi suala hilo linavyoendelea na kudai kuwa, kuna uwezekano mkubwa Malima anatiwa nguvu na kiongozi mmoja wa juu serikalini.

“Tumeshangazwa na hatua hiyo ya Malima, ambayo kimsingi ni kulidharau Bunge na tunachokitarajia sasa ni kuona mbunge huyo akiitwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ahojiwe sababu za kufanya hivyo,” alisema mbunge mmoja.

Wakati wabunge hao wakieleza kushangazwa na hatua hiyo, wanasema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu kuona hatua zitakazochukuliwa na viongozi wakuu wawili, Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Lowassa kwa mamlaka yake ya uenyekiti wa wabunge wa CCM.

Wabunge hao wanaamini kuwa, Lowassa ndiye atakayetakiwa kuwa mwangalifu zaidi katika kulishughulikia suala hili, kutokana na jina lake kuwa miongoni mwa watu wanaotajwa kuwa sehemu ya jambo lililomfikisha Malima kuchukua hatua hiyo.

Hata hivyo, alipoulizwa Bunge linaweza kumchukulia hatua gani Malima kutokana na kupeleka masuala yaliyojadiliwa ndani ya Bunge nje, alikwepa na kusisitiza kuwa atahakikisha kuwa anaendelea kusimama katika kanuni na sheria.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, katikati ya mzozo kati ya Mengi na Malima, jina la Lowassa liliwahi kutajwa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA). Kutajwa kwa jina la Lowassa, kulikuja wakati shauri kati ya watu hao wawili lilipokuwa likishughulikiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Ndesamburo ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe katika kamati hiyo, alitangaza kujitoa baada ya kudai kupata taarifa kutoka kwa Mengi zilizokuwa zikieleza kuwa, wajumbe takriban wote wa kamati hiyo ya Bunge walikuwa wamehongwa. Mbunge huyo wa Moshi Mjini, ambaye alizungumza hayo mbele ya waandishi wa habari, alikaririwa akisema Mengi alikuwa amemweleza kuwa, taarifa za wana-kamati hao kuhongwa alikuwa amezipata kutoka kwa Lowassa.

Habari nyingine ambazo Tanzania Daima imezipata hivi karibuni kabisa kutoka miongoni mwa wabunge wengine zinaeleza kuwa, hatua ya sasa ya Malima imezusha mijadala mikali ya chini kwa chini kwa siku kadhaa sasa, ambayo baadhi yake inayataja majina ya viongozi wengine kadhaa kuhusika.

Mbunge mmoja kijana wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini, alisema tayari kundi la wabunge wengine wa chama hicho, wameshaanza kujiandaa kumlinda Spika, ambaye wanamwelezea kuwa mwanasiasa asiyewabagua wabunge. “Sisi tunajua kabisa kuwa kile ambacho Sitta alikieleza mapema kabisa kuwa atakuwa ‘Spika wa Speed and Standard’ (Kasi na Viwango) kimekuwa ni kero kwa baadhi ya wana CCM ambao wanaiona hatua hiyo kuwa ni ya kujitafutia umaarufu na kwa kweli huo ndiyo msingi wa chuki dhidi yake,” alisema mbunge huyo.

Mbunge huyo alisema tangu habari zilipoanza kusambazwa kuwa Malima alikuwa amewasilisha barua ya malalamiko kwa Makamba kuhusu mzozo wake na Mengi, wabunge kadhaa wa chama hicho wamekuwa wakikutana ili kuweka msimamo wa pamoja kuhusu jambo hilo.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, miongoni mwa maazimio waliyoyafikia, ni kuhakikisha kuwa wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha Bunge linaheshimiwa, na Spika anapata fursa ya kutimiza wajibu wake pasipo kutishwa na mtu yeyote.

“Sisi tumeshawishika kuamini kuwa, Sitta anaonewa na watu wenye malengo binafsi ya kumharibia kazi, na wanaotaka apoteze uhuru wake wa kimamlaka wa kuliendesha Bunge pasipo kuingiliwa. Tumejipanga kumlinda kwa hali yoyote na kuwa tayari kuwaangusha wale wenye nia mbaya naye,” alisema mbunge mwingine wa CCM anayetoka Kanda ya Ziwa.

Kundi la wabunge wa CCM linalojenga hoja za kuiua hoja hiyo ya Malima, limeorodhesha vifungu vya Katiba ya Jamhuri na kanuni za Bunge, ambazo wanaamini kuwa wakizitumia, wataweza kuikwamisha ajenda ya siri ya Malima ya kummaliza Sitta kisiasa.

Moja ya vifungu walivyotumia, ni sheria namba 3 ya mwaka 1988, iliyo katika Ibara ya 24 (D) ambayo inapinga kuhojiwa kwa mamlaka ya Spika na chombo kingine chochote nje ya Bunge.

Aidha, wabunge hao wamepanga pia kutumia kanuni namba 60 ya Bunge iliyo katika toleo la mwaka 2004, ambayo pia inatoa mamlaka kwa maamuzi ya Bunge kutohojiwa na chombo kingine cha nje.

Walipoulizwa sababu hasa za kufikia hatua hiyo, wabunge hao walisema taarifa walizonazo zilikuwa zikionyesha kuundwa kwa mtandao mpya ndani ya mtandao wa wana CCM, wenye lengo la kuhakikisha Sitta anawekwa katika mazingira magumu kabisa kikazi.

Wabunge hao ambao walifikia hatua ya kuwataja kwa majina baadhi ya viongozi wa CCM na serikali walio nyuma ya sakata zima la Mengi na Malima, walisema kumekuwa na mahusiano mabaya kikazi kati ya Sitta na baadhi ya viongozi serikalini.

Katika mazingira ya kutatanisha, tangu Ndesamburo atoe tuhuma nzito za rushwa, ambazo sasa zimewasilishwa katika Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takuru), si Lowassa wala Mengi waliowahi kujitokeza hadharani kutoa kauli.

Hatua hiyo wakati fulani ilisababisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilazimike kumwandikia barua Waziri Mkuu, Lowassa kikimtaka atoe tamko kuhusu kuhusishwa kwenye tuhuma za rushwa kwa wajumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge zilizotolewa na Ndesamburo.

Barua ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilbroad Slaa ya Januari 15, 2007, ilieleza kushangazwa na ukimya wa Lowassa pamoja na tuhuma hizo nzito zilizotolewa na Ndesamburo.

Jitihada za gazeti hili kuwasiliana ama na Lowassa mwenyewe au mwandishi wake wa habari, Said Nguba wakati huo ili kupata maoni yake kuhusu suala hili ziligonga ukuta.

Hata hivyo, ofisa mmoja wa juu serikalini, aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa jina, alisema Waziri Mkuu alikaririwa (wakati huo) akiyaelezea maneno hayo ya Ndesamburo kuwa yasiyo na ukweli wowote.

Alipotakiwa na Tanzania Daima aeleze hatua ambazo Lowassa amepanga kuzichukua dhidi ya suala hilo ambalo kauli yake inahusishwa, ofisa huyo alisema, vyombo vinavyohusika vitalishughulikia.

“Sisi tunajua ni kwa nini Ndesamburo kasema maneno hayo. Tunajua kila kitu kinachoendelea kuhusu jambo hili. Ni vyema tukanyamaza. Waziri Mkuu anajua anachofanya, hawezi akasema maneno ya namna hiyo. Ipo siku ukweli utabainika,” alisema ofisa huyo wa serikali alipotafutwa na Tanzania Daima.

Badala yake, ofisa huyo wa serikali alieleza pia kushangazwa kwake na ukimya wa Mengi ambaye ndiye aliyetajwa na Ndesamburo kumwambia maneno hayo, kuendelea kukaa kimya pasipo kutamka hadharani iwapo ni kweli alifikisha maneno hayo au la.

“Ninyi mnamtafuta Waziri Mkuu atoe tamko, mbona hatujasikia Mengi akisema hadharani ni kweli kuwa alimwambia Ndesamburo maneno haya? Si yuko na anapatikana, mbona amekaa kimya?” alihoji ofisa huyo.

Hata hivyo wakati wa kikao cha Bunge cha mwanzoni mwa mwaka huu, Sitta aliamua kulitolea uamuzi suala hilo kwa kufanya kile ambacho gazeti hili lilikielezea kuwa ni kushindwa kwake kumaliza mzozo kati ya Mengi na Malima.

Sitta akitumia falsafa yake ya siku zote; ‘Hekima za Spika’, alitangaza rasmi kuwaita ofisini kwake Dar es Salaam katika siku itakayopangwa, lengo likiwa ni kutafuta suluhu ya kudumu.

“Na kwa kuwa, busara zangu zinanituma kwamba, njia nzuri na iliyo bora ya kuyashughulikia na kuyamaliza malalamiko ya watu hawa wawili, ni kwa usuluhishi (reconciliation) kati yao,” alisema Sitta wakati akisoma maamuzi yake.

Sitta alisema, alikuwa amelazimika kufikia uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa, watu hao wawili, kila mmoja alikuwa ametenda kosa la aina fulani, tangu sakata hilo liibuliwe na Malima mwezi Agosti mwaka jana.

Maamuzi hayo yalitokana na malalamiko ya Mengi, aliyowasilisha kwake (Spika) Agosti 6, mwaka jana, akilalamika kwamba, Agosti 2, 2006, wakati akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo bungeni, Malima pamoja na mambo mengine, alishutumu matumizi mabaya ya Kituo cha Televisheni cha ITV pamoja na mmiliki wake ambaye ni Mengi.

Katika matamshi yake, Malima alikishutumu kituo hicho kwa kutumia muda mwingi kutangaza habari zinazomhusu mmiliki wake wakati kikitoa muda mchache kutangaza masuala ya kitaifa yanayowahusu rais na waziri mkuu.

Kwa maneno yake, Malima alisema: “Nimewahi kushuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano ana habari nzito kwenye taarifa ya habari ya saa 2:00, anapewa dakika moja na nusu, Waziri Mkuu anataka kuzungumzia njaa anapewa dakika moja na nusu. Watoto wa ‘Primary’ wanakuja kutoka Zanzibar kutembelea Kiwanda cha Coca-Cola wanapewa dakika 10.

“Mmiliki wa TV anakwenda kuongea na watoto wa madrasa Msasani kwa ajili ya kugombana na sheikh mmoja anapewa dakika 10.” Mengi aliyachukulia matamshi hayo kuwa shutuma dhidi yake na ITV zilizotolewa katika eneo ambalo hawezi kujitetea, na kwamba hazikuwa na ukweli wala msingi wowote.

Baada ya matamshi hayo ya Mengi yaliyotolewa na ITV na Radio One, Malima aliomba muongozo wa Spika kuhusu hatua stahili anazopaswa kuchukua yeye binafsi kama mbunge kuhusu matangazo ya IPP Media dhidi yake au hatua zinazoweza kuchukuliwa na Bunge, kwa niaba yake.

Baada ya kupitia hoja hizo kwa kulinganisha na sheria, taratibu na kanuni zilizopo, Sitta alibainisha kuwa, wote wawili walikuwa wametenda makosa. Kwa upande wa Malima, Spika alisema kuwa, mbunge huyo alikuwa amelidanganya Bunge, kwani takwimu alizozitoa kuhusu taarifa za habari za ITV hazikuwa sahihi.

Maamuzi hayo ya Sitta, ndiyo yaliyosababisha Malima afikie hatua ya kuandika barua kwa Makamba akiyapinga.

juu
 
Mikuki,
Hivi umejibiwa swali lako? Au tunasubiri Mwanakijiji apitie tena ansards zake?
 
Jasusi na Mikuki.. kitu pekee alichosema Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mhe. Mohammed Seif Khatib akijibu maswali mbalimbali ya wabunge ni kuwa

.....Kuhusu vyombo vya habari vya IPP vinavyoandika suala la NSSF na Quality
Group niseme kwamba sisi Serikali hatuwezi kuingilia ugomvi kati ya Manji na Mengi,ni wao wenyewe na Wabunge msipelekwe huko katika ugomvi ambao sisi hautuhusu. Sisi hatuwezi kuingilia ugomvi ambao si wetu, wenyewe wanajuana. Kila mmoja afanye anavyotaka mwenyewe. Kwa bahati nzuri wako mahakamani sasa hivi. Kwa hiyo, hatuna cha kuzungumza zaidi, lakini nizungumze la pili kuna mtu kazungumzi kuwa vyombo vya habari vya IPP vinatumia nafasi yake kumpaka matope mwenzake, hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria. Huwezi kutumia chombo chako cha habari kwa ajili ya maslahi yako mwenyewe. Labda nisome eneo ambalo sera inasema hivyo. (Makofi)

Kwa mfano kifungu 3 (2) cha Sera ya Taifa ya Habari ya utangazaji ya mwaka
2003 inasema hivi: “Chombo cha habari kisitumiwe kwa manufaa binafsi ya mmiliki au mtendaji, bali kitatumiwa kwa maslahi ya umma.” Kwa hiyo, natoa wito kwa wenye vyombo vya habari, tafadhari tumieni vyombo vya habari kwa maslahi ya umma siyo kwa yenu binafsi. (Makofi)

Niendelee, kuna wengine wanalalamika kwamba magazeti yanachafua majina
yao. Kuna Baraza la Habari, mtu yeyote ambaye kachafuliwa jina lake basi anatakiwa apeleke habari, ufafanuzi zaidi au ampeleke mtu mahakamani. Sisi tusingependa kuingilia mambo ya watu binafsi…… (Makofi)
 
Hili swala, naona wengi humu hamulielewi kwa kina, Ugonvi wa Adam na Mengi hapo Mh Adam ametumiwa na Manji hii haina ubishi na habari za ndani ni kuwa huyu jamaa kawanunua waheshimiwa wengi mpaka nyumba kubwa.
Mtafaruku wa huyu Manji kwa kuiuzia kampuni ya uma yale magodauni ambayo tathimini yake ilifanywa na Mwalimu mmoja wa UCLAS anaeitwa Bw Komu, amabapo hata jopo la waalimu wa hiyo taaluma ya Real estate management, walikuja juu kuwa amewatia aibu kwa sababu kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa hali ya juu, na hii ilikuwa ni sawa na professional misconduct, walimtaka huyu Komu ajieleze, na aweke wazi kuwa Chuo hakikuhusika.
Sasa mkuu wa chuo alilivalia njuga saana swala hili, unajua kilichotoke juzi juzi tu, kafukuzwa ukuu wa chuo kwa amri ya state house, kwa kisingizio eti hawapendi wachaga.
Kama kuna mtu anabisha naweza kuzishusha hapa mawasilianao yaliyokuwa yankwenda kati ya waalimu wa UCLAS, hata huu udhamini wa Manji kwa Yanga ni shikizo la mwenye minofu (VDG) kumtaka hizo pesa alizoiibia kampuni ya umma basi azipeleke kwenye misaada. Kazi ipo kweli kweli Jasusi upo hapo lakini, niendelee??????
 
yombayomba,
hebu fafanua kuhusu kufukuzwa kazi kwa Principal wa UCLAS. Kuna madai hapa jamboforums kwamba Manji anapigwa vita na wachaga. Sasa inaelekea mtaalamu wa UCLAS aliyemsaidia katika ku-asses hayo majengo yake ni mchaga.

Yaani maelezo yako ni tofauti, na yanapingana na "UKWELI" kama unavyoeleweka hapa JamboForums.
 
Joka Kuu,
Aliyefanya mahesabu ya Manji ni Bw Komu, ni mchaga hilo halina utatanishi kabisa.
 
Joka kuu
Aliyefanya mahesabu ya Manji ya kiubabaishaji kuwakamua walalahoi anaitwa Bw. Felician Komu
 
PM aliiona hili ndo maana akamtonya Mengi, kwa sababu sasa hivi karatu zinachezwa na Manji (Vandame) na RA, hawa jama hawagusiki ukitaka kujimaliza kisiasa na kibiashara waguse
 
Mzee ES senior,

Any "nyeti" from Dodoma? macho na masikio yako kwako mzee.
 
Eeh bwana ninajaribu kuzi-diggest hizo nyeti zako ambazo unatumia jina la Yombayomba,

Sikuzaliwa jana blaza endelea na hizo nyeti tunakusikiliza bro!
 
Yombax2 wrote

".....................Sasa mkuu wa chuo alilivalia njuga saana swala hili, unajua kilichotoke juzi juzi tu, kafukuzwa ukuu wa chuo kwa amri ya state house, kwa kisingizio eti hawapendi wachaga..........."

Huyu Principal unayemzungumzia ni yupi huyo? Prof Iddris Kikula au?, kama unamsema Kikula, huyu Prof. hakufukuzwa. ila baada ya muda wake kuisha, kapelekwa Chuo Kikuu Dom, pengine kama kuna yaliyotokea hapa karibuni ambayo yamenipita...........

Yombax2 hebu fafanua kidogo maelezo yako.
 
yombayomba,
hebu fafanua kuhusu kufukuzwa kazi kwa Principal wa UCLAS. Kuna madai hapa jamboforums kwamba Manji anapigwa vita na wachaga. Sasa inaelekea mtaalamu wa UCLAS aliyemsaidia katika ku-asses hayo majengo yake ni mchaga.

Yaani maelezo yako ni tofauti, na yanapingana na "UKWELI" kama unavyoeleweka hapa JamboForums.

Hapa hapana msaada ni biashara mzee wangu toa cha mbele nikukasimie msee wangu!
 
Yomba yomba said:
Sasa mkuu wa chuo alilivalia njuga saana swala hili, unajua kilichotoke juzi juzi tu, kafukuzwa ukuu wa chuo kwa amri ya state house, kwa kisingizio eti hawapendi wachaga.

Nadhani Yomba Yomba kasema uwongo hapa.

Kwanza, hivi ni nani alikuwa principal wa UCLAS jamani?

Baada ya profesa Mshana kuondoka pale UCLAS, nilikuwa namjua Profesa Kikula. Majuzi tu ametajwa kuwa yeye anakuwa VC wa Dodoma University, hii inaweza hata kuthibitika kwenye thread nyingine hapa JF inayohusu Dodoma University (siwezi kupata link yake sasa hivi). Je ni kweli Prof Kikula alifukuzwa kwa amri ya Ikulu kutoka principal ili kusudi Ikulu hiyo hiyo ije imteue kuwa founding VC wa Dodoma University?

This doesn't make sense.
 
Kitendo cha Spika kutumia uwezo wake kunyamazisha mjadala Bungeni ni kitendo ambacho lazima kionekane kwa mwanga unaostahili, yaani ni kitendo cha kimabavu, matumizi mabaya ya madaraka, na kinachopakana na tabia za kiimla. Inawezekanaje mtu mmoja kuamini kuwa ana uwezo wa kuwanyamazisha wawakilishi wa watu kuzungumzia jambo fulani kwa vile tu jambo hilo linamhusu yeye? Inakuwaje mlalamikiwa ndio akawa mkata shauri!!? Walisema ukistaajabu ya Musa, utaona ya Farao.

http://mwanakijiji.podomatic.com
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom